Haki ya Mungu nimejikuta namkumbuka Magufuli ghafla tu

Haki ya Mungu nimejikuta namkumbuka Magufuli ghafla tu

Mambo mengi tu mkuu hayaendi.

Ni kama vile Taifa limekosa dira.

Taifa limekosa kiongozi mwenye maono na kuyasimamia ili yatimie.

Kinachoendelea sasa ni kuchambana tu.

Sijui mwisho wa haya ni nini ila ipo haja ya kukalishana na kuelezana ukweli.

Hatuwezi enda kama vile hatuna vichwa.
 
Nimekuwa nikijitambukisha hapa kama mtoa huduma kwa jamii (sio tanesco) Hilo halina uficho, sasa basi hapa kibaruani enzi JPM akija mteja hata kama kavaa ndala moja nyekundu moja ya njano anahudumiwa fasta (unawaza labda ndio under cover wa Jiwe kaja kukagua utendaji kazi) sasa hivi mambo yamebadirika Sana, watu wanaenda chai kuanzia saa nne wanarudi saa sita, hata ukipishana nao kwenye korido huudumiwi!

Tujiulize Magufuli aliwezaje kuiongoza nchi kwa kasi ile??
 
Pole sana Mkuu... Hawa jamaa wa umeme ni miongoni mwa sekta zilizoanza kutoa huduma kwa kusuasua baada ya kifo cha jamaa....
 
Wakati wa Magufuli 2016 au 17 kama sijakosea nilipata loose connection kwenye mstimu nje ya nyumba ninayoishi, nikapiga emergency TANESCO na ndani ya robo saa wakafika na kurekebisha kisha nikawapa 15,000 kama ahsante, haki ya Mungu waliikataa


Leo tatizo limetokwa tena nikapiga simu wakasema mafundi wanakuja, nimesubiri weeee masaa yamepita nikaamua kwenda ofisini kwao nikawakuta mafundi wakaniambia nenda tunakuja, nikaondoka masaa yakapita tena hawajaja nikaenda tena nawabembeleza niwape hela wanirudishie huduma pia wanadengua labda kiwango hakitoshi

Kweli Magufuli alikuwa jembe
Na sidhani kama atatokea kama yeye tena
Pole mkuu
TANESCO
 
Kwani Magu si ni CCM? Na sasa bado ni CCM wanaongoza? NANI ALIKUAMBIA KUNA MTU ANAISHI MILELE? Ndio shida ya watu kuweka tegemezi kwa binadamu.
Mbona unachoongea hakiendan na post ya jamaa , chuki sio kitu kizur , naona unakomaa kumtafutia mazingira ya kuonekana mbaya
 
Mi nahisi magu pale ccm alipitia tu ila alikuwa na chama chake moyoni mwake, iweje yeye aweze wengine washindwe?
Unataka kusema viongozi hawayaoni haya tunayolalamikia?
Ukifuatilia hotuba zake ,inaonesha alikuwa anayaona mabaya kwa muda mrefu ila alisubir apate saut
 
Kama Magufuli angekuwa anashughulikia tu mafisadi ingekuwa sawa. Ila pia wakati wa serikali au awamu yake kulikuwa na ukatili mkubwa sana na watu hasa waandishi wa habari walikimbia na uchaguzi haukuwa huru. Kwa sababu hiyo, haijalishi ni lipi zuri alifanya, Kwa WENGI ANABAKIA KUWA KIONGOZI MKATILI SANA
Waandish wengi + vyama vya upinzan vingi wanatumika mkuu , inaitaj akili kuelewa haya mambo mkuu , Refer Russia kwann alitaka kumuua yule.mpinzan na kwann wazungu walimgombania kumtibu ? Je wananufaikaje nae ? Shukuru una amani ya kuandika utumbo humu jf ila wapo wenzio hawana hiyo nafasi
 
Mungu aiweke roho yake mahali salama.
Tunakupenda JPM wetu
 
Hata jambazi linaloua watu, akifa mke wake na watoto wake watamkumbuka. Huo ni mfano wa mtu mkatili.. kwamba akifa lazima kuna watakaomkumbuka. Kwa JPM, Sio kwamba kila mtu alifungwa akili na mawazo kama hivyo na JPM. Na sio kila mtu anamkumbuka.
Ana ukatili gan kwa mfano ? kuwafukuza vyeti fake ? Hujui hao watu walivyokuwa wanajaza ndugu zao wasio na sifa kweny taasisi mbali mbali ? Na weny elimu wanatupwa nje daily wakihofia watazichukua nafasi zao , au kuwabana matajir wakwepa kodi ? hujui pia michezo ya hao matajiri , yaan kiufupi JPM alikuwa na vita kubwa mno na alifanya kila kitu kwa maslai ya taifa ,ndio kafanya vitu ambavyo ungeambiwa before ungesema ndoto za alinacha na ndio maana hoja kubwa dhidi yake ni kujenga airport Chato au kumsingizia watu wasiojulikana ( poor reasoning , wilaya inakosaje airport wakati wilaya nyingine zina airport )
 
We ni tahira kweli, TANESCO emergency Wala hawaitaji hela wakija kusolve tatizo kwako,we sababu ni boya ulijipendekeza kuwapa au unawachafua tu, TANESCO kitengo Cha emergency wapo vizuri Sanaa,labda kwa mengine hapo sawa
usimtukane mwenzio , ongea na mtu timamu , lete mifano hai ya ubora wenu / wao , mimi ni.muhanga wa huduma zenu mbovu , so namuungaa mkono jamaa
 
Alikopa trilioni 29 ndani ya awamu 1 na akawa anatuaminisha kuwa tuna uwezo wa kujitegemea, tuchape kazi.
Huoni ilivyotumika? Flyover kajenga bab ako ? Sgr ya mjomb ako? vituo vya afya kajenga bib ako? Au zile stend zenye hadhi ya kimataifa kajenga babuu yako ? pia madaraja bila kusahau salender na busisi kajenga bash ako? kafufua reli ya kaskazini au kuangalia tv mpk kwa mwenyekit ? kafufua kalakana la uundwaji wa meli kwa z.Viktoria na Z.Tanganyika , pia madege kaleta ya kutosha tusiyafaidishe makampuni ya wageni , bila kusahau kabiresha mashule , viwanja vya ndege , barabara na masoko makubwa mengi tu tz , HAYA NIAMBIE MKOPO WA HUYO KIBIBI CHAKO KIZEE UMEFANYA NINI ?
 
Huoni ilivyotumika? Flyover kajenga bab ako ? Sgr ya mjomb ako? vituo vya afya kajenga bib ako? Au zile stend zenye hadhi ya kimataifa kajenga babuu yako ? pia madaraja bila kusahau salender na busisi kajenga bash ako? kafufua reli ya kaskazini au kuangalia tv mpk kwa mwenyekit ? kafufua kalakana la uundwaji wa meli kwa z.Viktoria na Z.Tanganyika , pia madege kaleta ya kutosha tusiyafaidishe makampuni ya wageni , bila kusahau kabiresha mashule , viwanja vya ndege , barabara na masoko makubwa mengi tu tz , HAYA NIAMBIE MKOPO WA HUYO KIBIBI CHAKO KIZEE UMEFANYA NINI ?
Jibu swali kwa nini hakusema ni mkopo akasema ni pesa za ndani stupid
 
Itoshe kusema tu Magufuli alikuwa ni jembe
Lakini siyo kusema hudhani atatokea tena kama yeye.
Watanzania tuko 60M huenda kuna wazuri kuliko alivyokuwa yeye ni suala la Mda tu.!
Wazuri wapo ila kujitoa muhanga ndo hawapo , maana unakuwa unapambana na chama chako
 
Kipindi watu wanapotea aliambiwa na wanaharakati, baadhi ya wanasiasa na watu wenye mimba cha chuki vichwani vyao sababu ni yy.

Cha ajabu sasa watu wanatupwa wapo kimya.
Watu wanapotea kimya.

Kipindi kile kama kungekuwa na mgao wa maji, umeme, tozo nk humu JF na social networks wangemwandama sana. Ila cha ajabu sasa hivi kimya mpaka unahisi labda wanaishi Burundi.

Ila ukichunguza zaidi wanasiasa, wanaharakati always wapo kimaslai so Mwendazake aliibana mirija ya kuingiza pesa zao za magumashi.Sasa naona kimya walikuwa wanadai hawana uhuru wa kuongea, ila sasa hivi hawaongei, tozo kimya, mgao wa umeme na maji kimya, haya watu wanapotea kimya.

Cha ajabu nao wanasifia nchi imefunguka.
 
Tumpe mama nafasi. Anahujumiwa na Sukuma Gang.

Subirini awamalize wahujumu mambo yatakaa mwendo mserereko
Kwan hao sukuma gang ndo wanazuia asimalizie yale ma fly over? au zile barabara za brt ? au sgr ? Ccm imebakia na watu wapumbav sn siku hz , sijui wamepigwa dawa , sitak kuamini buk 3 inatosha kumtoa utimamu wake
 
Back
Top Bottom