Haki yangu kikatiba ya kushawishi/hamasisha wamuongezee muda Rais Magufuli

Haki yangu kikatiba ya kushawishi/hamasisha wamuongezee muda Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.

JERUSALEM 2006

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
527
Reaction score
596
5G3TVR.png

1. Katiba ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na marekebisho yake ya 30th April 2000 yananipa haki zote kama raia halali wa Taifa la Tanzania kuwa na mawazo huru juu ya jambo lolote ambalo halivunji sheria za nchi yetu.

Mimi kama Mtanzania tarehe 16 Februari 2020 nilianzisha uzi unaosema "KARIBU TUJIUNGE NA KUNDI LA MAGUFULI TENA 2025" na mjadala katika kundi hili ulikuwa unaendelea. Kwa bahata mbaya sana.

2. Katiba ya jamhuri ya Tanzania ( 1977) kuanzia ibara ya18 (UHURU WA MAONI) , ibara ya19 ( UHURU WA MTU KUSHIRIKIANA NA MTU MWINGINE) kwa pamoja zinasema

Ibara 18.1 Bila kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake,na kutafuta,kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru mawasilano yake kutoingiliwa kati.

Naomba nielezee ibara hii ya 18.1; ni kwamba nina uhuru wa kutoa mawazo yangu yoyote, katika chombo chochote ikiwemo Jamii Forums, bila kuingiliwa na yeyote.

Ibara 20.1 Kila mtu anastahili kuwa Huru, bila ya kuathiri Sheria za Nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanyika, na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyo anzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

Nia yangu ni thabiti, ni kuanzisha mchakato wa kubadirisha Katiba kwa kukusanya signatures zaidi ya million tano za wa Tanzania ili kuweza kukidhi matakwa ya kikatiba ya kumuongezea angalau muhala mwengine Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,

KAULI MBIO YETU NI.

"H.E President Magufuli is too valuable to retire, Tanzanians needs him now more than ever" " Mhe, Rais Magufuli ni wathamani sana kustaafu, Watanzania wanamuhitaji sasa kuliko kipindi kingine chochote"

MWISHO

Kama nilivyo quote vipengele vya katiba, basi naomba mawazo yangu yaheshimiwe. Situkana, sijapanga kuua, wala sija panga kuvunja sheria za Nchi, ninafuata taratibu zote ili kubarisha vipengere vya Katiba ambayo siyo Msaafu wala siyo Bibilia.
 
Upvote 3
1. Katiba ya Jamuhuri wa muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na marekebisho yake ya 30th April 2000 yananipa haki zote kama raia halali wa taifa la Tanzania kuwa na mawazo huru juu ya jambo lolote ambalo halivunji sheria za nchi yetu...
Mungu sio mwanadam, na ndio mwenye mamlaka yote, mwanadam huwezi mpangia japo weweza lazimisha, na ndivyo kifanyachwo na watu wachache KWA maslai binafsi, KWA kujua au kutojua, katika Jambo hili, acheni roho za watu mil 50 ziamue, juu ya Jambo hili nyeti, ila isiwe kakundi ka watu 100 kufanya mahamuzi ya roho mil hamsin,maana hakuna wa kuishi milele, mtapata lahana,na kuitafuta jihanam isiyo ya lazima,

Kumtukuza mwanadam katika kiwango kilichopitiliza nayo ni dhambi mbele za bwana. Endeleeni maana mwaiona leo yenu ilionjema , KWA upofu wa mda , kesho yenu ikiangaza mtakufa hamna huwezo wa jana,ndipo mtakapo Lia na kusaga meno.
 
1. Katiba ya Jamuhuri wa muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na marekebisho yake ya 30th April 2000 yananipa haki zote kama raia halali wa taifa la Tanzania kuwa na mawazo huru juu ya jambo lolote ambalo halivunji sheria za nchi yetu
SAWA, mradi na wengine wenye mawazo tofauti na yako nao wawe na haki hiyo hiyo kama uliyo nayo wewe.

Je, umekwishafikiria ni kwa vipi na nani atakayesimamia kwa HAKI kufikia uamzi wa mwisho kati ya makundi haya mawili yenye mitizamo tofauti?

Kama wewe ni mkweli na muumini wa kweli katika hiyo Katiba, bila shaka utakubaliana na matokeo bila shari kama upande wako utashindwa, na hamtajihusisha na hujuma ili mshinde kwa nguvu kama ilivyokuwa kwenye uchaguzi mkuu uliopita!

Au unasemaje, mkuu JJB.
 
Mkuu mie nimeandika kumtahadharisha rais wa sasa na watu mnaojaribu kujenga hoja ya kutaka abadili katiba ili arefushe muda wa kutawala,kwamba si wote wanaoonge hayo maneno wana nia njema kuna wengine ni kwa faida ya matumbo yao tu!
Hilo ndio jibu sasa mzee wa watu amesema akimaliza anapumzika , wanataka aendelee ili waweze kunufaika.

Naamini katika safu za uongozi alizopaga huyu mzee kuna watu hawatakuja kuzipata tena maisha yao yote. Na nindoto kwa wao kupata sasa hawa watu wataachaje kusifu na kuabudu?

Kizuri ninacho mpenda huyu raisi yeye mwenyewe anawachora tu, anajua huyu ananisifu kwaajili ya njaa na anawajua .

Mfano mzuri ni lile jengo walilotaka lijengwe chato fuatilia ile clip utajua namaanisha nini?
 
Nataka kukwambia tu kwa faida yako na watu wengine 9999 unaowatafuta . Watanzania ni watu wa amani sana.

Lakini kile watanzania wameifadhi mioyoni mwao ni kitu kingine kabisa...

Anachokifanya Mh. Raisi ndio kimepelekea azma hii.

1.Kuweka umeme zaidi ya vijiji elfu 10 ndani ya miaka mitano tu, wakati alikuta kuna vijiji 2000 tu vyenye umeme.

2. Kujenga miradi mikubwa ya nishati ikiwemo bwawa la nyerere lenye MW 2115 na mabwawa mengine madogo madogo.

3. Kujenga SG railway kwa rwli ya kati

4. Mtandao wa barabara za rami sasa uko kila mkoa na unaunganisha mikoa yote.

5. Hospitali na vituo vya Afya ndio usiseme.

6. Elimu Bure mashuleni.

Jamani, mambo ni mengi, na yote nimetaja ni maendeleo.

Sasa kama hauoni, na unaona biashara zinazofungwa ila huoni zinazofunguliwa basi unashida kubwa
 
Sawa bambushka

Hapa mada ni Mh. Rais aingezewe muda ili akamilishe miradi yote mikubwa aliyoianzisha
Mkuu watu wanapigania mfumo na mifumo thabiti siyo mtu kwa sababu, Mungu ndiyo anayeamua kesho zetu.

Mifumo thabiti ndiyo inayoendesha nchi siyo mtu mmoja.

Ashakumsi matusi, wala sisemi kwa ubaya vapuu, Mungu kachukua pumzi yake, kazimisha mshumaa, nchi lazima iende.

Tuachane na huu upuuzi wa 1 man show, hata kama kawatuma, mwambieni ukweli.
Hapo TISS mnatetea ugali wenu. Mnajua akiingia mwingine atawafumua fumua na mfumo wenu mtakuwa na maisha magumu.

Mtakuwa makarani wa masjala😂😂huko halmashauri za Ushetu, Malinyi na Ushirombo. Shubamiti

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Sasa Iyakuze na Twaweza wameingiaje hapa?

Kama kuna namna nimewagusa samahani, ila tubaki kwenye mada kuu.

Mhe. Rais aongezewe muda kwa kubadili katiba
Umezungumzia Approval rating ? Lazima uguse huko mada ni pana sana hii mkuu, hizo nimekupa reference tu.
 
Sawa, ila tubaki kwenye mada.

Magufuli tena 2025
<kuu hutuzidi sisi kwa uzalendo.
Uzalendo ni nchi si mtu.
Tulikuwepo wakati w Mwalimu na ilithibitika kuwa waliokuwa wandai Mwalimu aendeleeni wanufaika wa vyeo walivyopewa.
Mwalimu aliligundua hilo na akawalipua.
Nawe ni mnufaika , jitegemee, kun maisha zaidi ya ofisi.
 
Mkuu watu wanapigania mfumo na mifumo thabiti siyo mtu kwa sababu, Mungu ndiyo anayeamua kesho zetu.

Mifumo thabiti ndiyo inayoendesha nchi siyo mtu mmoja.....
Duh Bambushka yamekuwa hayo??

Kwa hiyo na China walio amua kumuongezea Raisi Chi, tuwaiteje?

One man show?
 
Anachokifanya Mh. Raisi ndio kimepelekea azma hii.

1.Kuweka umeme zaidi ya vijiji elfu 10 ndani ya miaka mitano tu, wakati alikuta kuna vijiji 2000 tu vyenye umeme...
Hivi hii miradi ameazisha yeye au ameikuta?
 
Umezungumzia Approval rating ? Lazima uguse huko mada ni pana sana hii mkuu, hizo nimekupa reference tu.

Iyakuze na Twaweza hawaingiliani na approval ratings za Mh. Rais, na wala sikumbuki ni lini waliwahi kufanya utafiti huo.
 
Uzalendo ni nchi si mtu.
Tulikuwepo wakati w Mwalimu na ilithibitika kuwa waliokuwa wandai Mwalimu aendeleeni wanufaika wa vyeo walivyopewa.
Mwalimu aliligundua hilo na akawalipua.
Nawe ni mnufaika , jitegemee, kun maisha zaidi ya ofisi.

Kwa hiyo tutaamini vipi kama na wewe haunufaiki na kubadilishwa kwa mamlaka ya juu?

Mimi siongelei maskahi binafsi,
its not about power sharing, its about the capabilities of leading a country with diligence and high discipline.

Over
 
Duh Bambushka yamekuwa hayo??

Kwa hiyo na China walio amua kumuongezea Raisi Chi, tuwaiteje?

One man show?
Maswahiba zenu wachina hawanihusu binafsi ninaongelea TANZANIA au ndiyo mnawakopi??

Yule waziri wao wa mambo ya nje, ndiyo alikuja kuwafundisha hayo??

Pigania mfumo nitakuja huko telegram, huu upuuzi wa 1 man show siusapoti.
Eti amejenga hiki kabomoa kile, kanunua hiki, blah blah, HANA HELA BINAFSI NI MUAJIRIWA, anatumia kodi zetu. Kodi kodi kodi za watanzania.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Mbona umekosea jina? Magufuri? Na umelirudia kosa hilo kote ulipoandika, kasoro heading.
Kosa hilo pekee linamwondolea sifa anayoitanguliza hapa ya kuwa "mfuata sheria."

Anakuja JF kufanya 'recruitment' kwa uchafu wake, halafu anasahau kuwa mtu anayemtaka kumbe ni watu wa majina mawili tofauti!
Sasa anataka watu wajiunge kwenye kundi lake wakampiganie nani hasa?
 
Kwa hiyo Magufuli amefanya mengi kuliko watangilizi wake akiwemo Baba wa Taifa? Mbona hao hamkusema waongezewe muda? Acha hayo mambo
 
Kosa hilo pekee linamwondolea sifa anayoitanguliza hapa ya kuwa "mfuata sheria."

Anakuja JF kufanya 'recruitment' kwa uchafu wake, halafu anasahau kuwa mtu anayemtaka kumbe ni watu wa majina mawili tofauti!
Sasa anataka watu wajiunge kwenye kundi lake wakampiganie nani hasa?

Hoja yako ni mufilisi, haina mashiko;

Umeelewa mada unataka kupindisha ukweli, yani herufi moja ndio ikitoe kwenye reli?

Duh
 
Unakaribishwa pia,
Jambo la msingi sheria za nchi ziheshimiwe bila kuathiri uhuru wa wengine
Hizo sheria za nchi unazozisema zinaruhusu Rais kuendela baada ya kumaliza mihula yake miwili? Au ni sheria za nchi ya Uganda unazungumzia?
 
Kwa hiyo Magufuli amefanya mengi kuliko watangilizi wake akiwemo Baba wa Taifa? Mbona hao hamkusema waongezewe muda? Acha hayo mambo

Kwa maoni yangu kafanya mengi kuliko watangulizi wake, kuhusu baba wa Taifa sijui,

Ila ninachojua; baba wa Taifa aliongezewa muda baada ya kufanya vizuri
 
Hizo sheria za nchi unazozisema zinaruhusu Rais kuendela baada ya kumaliza mihula yake miwili? Au ni sheria za nchi ya Uganda unazungumzia?

Tuko kwenye mchakato wa kuomba kubadili katiba, so hatujavunja sheria
 
Tanzania ina vitu vingi sana vya msingi vya kuzungumzia sio upuuzi wa kuongezea muda eti rais atawale milele wakti kuna watu kibao hapa na wanaweza kuongoza vizuri kabisa
Hakika Tz ina vitu vingi vya muhimu vya kujadili, ila ni wazi kwamba umuhihimu wa jambo lolote unatokana na jinsi jambo lenyewe lilivyokugusa.

Kwa jinsi unavyojibu hii mada kwa hisia inaonesha ni jinsi gani imekugusa. Hivyo basi, ni busara kusoma mawazo ya mleta mada pamoja na wengine wanaoendana naye kisha kupambana nao kwa hoja.

Hili jambo sio dogo na inaonesha linajengwa kimkakati. Unahitajika mkakati na weledi mkubwa kupambana na hii hoja. Kusema ufutwe hakutauondoa kwenye makusudi ya waliouanzisha.

Acha uwepo tujue kina chake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom