Haki za wanyama: Serikali ipige marufuku wanyama kama ng'ombe kuvuta mikokoteni

Haki za wanyama: Serikali ipige marufuku wanyama kama ng'ombe kuvuta mikokoteni

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,828
Reaction score
165,667
Kila ninapona hawa wanyama wanavuta mikokoteni huku wakicharazwa mijeledi, huwa naumia sana na kuona huu ni ukatili dhidi ya wanyama ila uliohalalishwa na mataifa kwa miaka mingi sana.

Kwanza ni lazima tujiulize kama hawa wanyama waliumbwa kufanya hizi kazi au ni sisi wanadamu ndio tunawalazimisha kutokana na shughuli zetu za kiuchumi na kijamii.

Na kwa wale wasomaji wazuri wa maandiko matakatifu,kuna mahala popote katika vitabu vitakatifu panapohalalisha wanyama hawa kutumikishwa namna hii?Kama hakuna, mamlaka haya wanadamu tumeyatoa wapi?

Ni wazi mambo haya yamekuwepo tangu enzi za mitume na manabii na pengine hata mitume na manabii hawa hawakuwahi kukemea hali hii.Lakini swali ni je, ni lazima kila jambo likemewe na mitume na manabii ndio tulione haramu?

Nafikiri wakati umefika kama ambavyo dunia iliungana kukosemesha biashara ya utumuwa, dunia sasa iungane kupiga marufuku matumizi haya ya kikatili dhidi ya wanyama.

Unamuon mnyama kachoka kupita kiasi, huku anatoa mapovu mdomoni lakini analazimishwa tu kusukuma mkokoteni kwa mijeledi tunasahau kabisa wanyama hawa nao wameumbwa kwa nyama na damu kama sisi na ndio maana Punda akichoka, hata umpige mijeledi hatembei/hainuki ila sio ng'ombe ataende huku akiumia.

Hata matumizi ya wanyama kama ng'ombe kutumika kama maksai ni ukatili tu kwa manufaa ya mwanadamu ila mnyama huyu hakuumbwa kutumika kwa shughuli za kilimo.

Kama ni jambo gumu, basi tupige marufuku matumizi ya ng'ombe kuvuta mikokoteni na tuache wanyama kama ngamia na Farasi tu kutumika kwa matumizi ya aina hii au yanayofanana na haya.

Matumizi ya Farasi huwezi kulinganisha na ya ng'ombe hasa katika nchi zetu hizi za dunia ya tatu ambako hata matunzo ya hawa wanyama ni duni kabisa.
 
Ni process, with time it ll all dissapear. when we have tractors other means of doing farming.

Europe use horse power for centuries.
 
Huruma isiishie hapo tu ikiwezekana kabisa tupige marufuku uchinjaji wa ng'ombe maana kila maisha yana thamani

Vingunguti sometimes zinaangushwa ng'ombe 1k kwa siku moja, huu ni ukatili
 
Huruma isiishie hapo tu ikiwezekana kabisa tupige marufuku uchinjaji wa ng'ombe maana kila maisha yana thamani

Vingunguti sometimes zinaangushwa ng'ombe 1k kwa siku moja, huu ni ukatili
No wonder na sisi wanadamu magonjwa kama corona na mengineyo yaliyowahi kutokea siku za nyuma na kupukutisha wanadamu hulipuka na kutushambulia ili ku-control population ya mwandamu duniani .

Dunia ikiwa over populated, maisha ya ndege na wanyama kama ng'ombe, nguruwe, mbuzi,kondoo, na wanyama wengine wa kufugwa yanakuwa hatarini zaidi.

Kumbuka kila kitu hakipaswi kuzidi kiwango.Hivyo, hata population ya mwanadamu ikiwa ni tishio kwa ustwahi wa viumbe wengine na dunia kwa ujumla, Mungu/Nature huleta magonjwa ya mlipuko na majanga mengine ya asili ku-control human population- wanadamu tunaweza tusilione hili na hata kusadiki.
 
Hii mada ikiwa serikali itaipuuza, basi ujue itakuja kutumika kama ajenda ya kuitoa CCM madarakan hapo 2025, Wapinzani wakikosa hoja huwa wanakuja na viroja.
 
Binadamu ni mtawala wa kila kitu
Ni kweli binadamu ni mtawala wa kila kitu, lakini utawala wa binadamu kwa hivi viumbe ni wa laana, tuliambiwa na Mungu tukavitawale hivi viumbe lakini chakushangaza vyenyewe havitutii.

Mungu alivyomfukuza Adamu bustani ya Eden alimwambia utaonja mauti na vizazi vyako, na hiyo dhambi sisi wanadamu tumeirithisha kwa hivyo viumbe, jiulize; iweje kosa la kula tunda la mti wa kati wafanye Adam na Hawa lakini adhabu yake ya mauti iende mpaka kwa hivyo viumbe? jibu ni sisi wanadamu ndio tumeviponza hivyo viumbe, vinatuogopa, vinatuona kama mashetani.

Hivyo basi, viumbe vikituona vinaiona hiyo laana ya mauti kwetu tuliyoachiwa na Mungu, ndio maana japo kuku unamfuga, lakini ukitaka kumchinja mpaka umkimbize umkamate ndio umchinje, na utamchinja akiwa analia muda wote mpaka anapokata roho, the same kwa mbuzi na viumbe wengine..

Kama mamlaka ya kuvitawala hivi viumbe kwetu yangekuwa ya kitakatifu, basi tungekuwa na uwezo wa kuviita na vikatutii tukavifanya tunachotaka bila shida, hata kwa wanyama wakali kama Simba na Chui, nao tunalalamika wanatushambulia lakini ukweli ni kwamba wanajua wakituchelewesha tutawamaliza sisi, hivyo wanaamua kujihami mapema kwa kutuwahi sisi.
 
Ni kweli binadamu ni mtawala wa kila kitu, lakini utawala wa binadamu kwa hivi viumbe ni wa laana, tuliambiwa na Mungu tukavitawale hivi viumbe lakini chakushangaza vyenyewe havitutii....
Uko vzr mkuu😃😃😃😃inawezekana ikawa kweli ulichosema
 
.......uko vzr mkuu[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]inawezekana ikawa kweli ulichosema
Ukiweza kuingia kwenye maandiko ya biblia kwa ndani utaweza kuyachambua na kuzitambua siri zilizomo ndani ya maandiko hayo kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
 
Sheria ya kutowapiga wanyama na ukatili wowote upo kisheria na unapigwa faini
Ila kwa sasa naona halifuatiliwi sana
Nakumbuka hii sheria ilikuwa chini ya mkoloni
Hata mzee wangu alikuwa na kibali cha kuwakamata na kuwapeleka polisi na kulipishwa faini ( hii ni miaka ya nyuma sana)
Kwa kweli nikiona mtu anachapa ng’ombe au punda huwa sinyamazi na huwa nawakaripia sana na kuwapa fundisho na kuwaambia hao ndio wanawapa ugali
 
MTOA POST UTAKUWA NA MATATIZO YA MSONGO WA MAWAZO ......binadamu ni mtawala wa kila kitu
Kila kitu kina misingi yake,nidhamu yake,njia zake na haki zake katika kukitawala,huwezi kua katili kisa wewe ni mtawala wa mnyama fulani.
 
Sheria ya kutowapiga wanyama na ukatili wowote upo kisheria na unapigwa faini
Ila kwa sasa naona halifuatiliwi sana
Nakumbuka hii sheria ilikuwa chini ya mkoloni
Hata mzee wangu alikuwa na kibali cha kuwakamata na kuwapeleka polisi na kulipishwa faini ( hii ni miaka ya nyuma sana)
Kwa kweli nikiona mtu anachapa ng’ombe au punda huwa sinyamazi na huwa nawakaripia sana na kuwapa fundisho na kuwaambia hao ndio wanawapa ugali
Binafsi huwa naumia sana kuona jinsi hawa wanyama wanavyotumikishwa.
 
Back
Top Bottom