Kila ninapona hawa wanyama wanavuta mikokoteni huku wakicharazwa mijeledi, huwa naumia sana na kuona huu ni ukatili dhidi ya wanyama ila uliohalalishwa na mataifa kwa miaka mingi sana.
Kwanza ni lazima tujiulize kama hawa wanyama waliumbwa kufanya hizi kazi au ni sisi wanadamu ndio tunawalazimisha kutokana na shughuli zetu za kiuchumi na kijamii.
Na kwa wale wasomaji wazuri wa maandiko matakatifu,kuna mahala popote katika vitabu vitakatifu panapohalalisha wanyama hawa kutumikishwa namna hii?Kama hakuna, mamlaka haya wanadamu tumeyatoa wapi?
Ni wazi mambo haya yamekuwepo tangu enzi za mitume na manabii na pengine hata mitume na manabii hawa hawakuwahi kukemea hali hii.Lakini swali ni je, ni lazima kila jambo likemewe na mitume na manabii ndio tulione haramu?
Nafikiri wakati umefika kama ambavyo dunia iliungana kukosemesha biashara ya utumuwa, dunia sasa iungane kupiga marufuku matumizi haya ya kikatili dhidi ya wanyama.
Unamuon mnyama kachoka kupita kiasi, huku anatoa mapovu mdomoni lakini analazimishwa tu kusukuma mkokoteni kwa mijeledi tunasahau kabisa wanyama hawa nao wameumbwa kwa nyama na damu kama sisi na ndio maana Punda akichoka, hata umpige mijeledi hatembei/hainuki ila sio ng'ombe ataende huku akiumia.
Hata matumizi ya wanyama kama ng'ombe kutumika kama maksai ni ukatili tu kwa manufaa ya mwanadamu ila mnyama huyu hakuumbwa kutumika kwa shughuli za kilimo.
Kama ni jambo gumu, basi tupige marufuku matumizi ya ng'ombe kuvuta mikokoteni na tuache wanyama kama ngamia na Farasi tu kutumika kwa matumizi ya aina hii au yanayofanana na haya.
Matumizi ya Farasi huwezi kulinganisha na ya ng'ombe hasa katika nchi zetu hizi za dunia ya tatu ambako hata matunzo ya hawa wanyama ni duni kabisa.