Binadamu ni mtawala wa kila kitu
Ni kweli binadamu ni mtawala wa kila kitu, lakini utawala wa binadamu kwa hivi viumbe ni wa laana, tuliambiwa na Mungu tukavitawale hivi viumbe lakini chakushangaza vyenyewe havitutii.
Mungu alivyomfukuza Adamu bustani ya Eden alimwambia utaonja mauti na vizazi vyako, na hiyo dhambi sisi wanadamu tumeirithisha kwa hivyo viumbe, jiulize; iweje kosa la kula tunda la mti wa kati wafanye Adam na Hawa lakini adhabu yake ya mauti iende mpaka kwa hivyo viumbe? jibu ni sisi wanadamu ndio tumeviponza hivyo viumbe, vinatuogopa, vinatuona kama mashetani.
Hivyo basi, viumbe vikituona vinaiona hiyo laana ya mauti kwetu tuliyoachiwa na Mungu, ndio maana japo kuku unamfuga, lakini ukitaka kumchinja mpaka umkimbize umkamate ndio umchinje, na utamchinja akiwa analia muda wote mpaka anapokata roho, the same kwa mbuzi na viumbe wengine..
Kama mamlaka ya kuvitawala hivi viumbe kwetu yangekuwa ya kitakatifu, basi tungekuwa na uwezo wa kuviita na vikatutii tukavifanya tunachotaka bila shida, hata kwa wanyama wakali kama Simba na Chui, nao tunalalamika wanatushambulia lakini ukweli ni kwamba wanajua wakituchelewesha tutawamaliza sisi, hivyo wanaamua kujihami mapema kwa kutuwahi sisi.