Haki za wanyama: Serikali ipige marufuku wanyama kama ng'ombe kuvuta mikokoteni

Kwanini ngamia na farasi watumike ila ng'ombe wasitumike au ngamia siyo wanyama ?

Halafu unaposema tusitumie wanyama kufanyia hizo kazi hiyo mikokoteni tutakuwa tunakufunga wewe ?
 
Kwanini ngamia na farasi watumike ila ng'ombe wasitumike au ngamia siyo wanyama ?

Halafu unaposema tusitumie wanyama kufanyia hizo kazi hiyo mikokoteni tutakuwa tunakufunga wewe ?
Tukufunge wewe.
 
Mimi naumizwa na ukatili wa kufanya settup wanyama wafugwao kwa wanyama hatari wa mwituni.kuna crip nyingi za mtindo huu ili kupata watazamaji wengi mtandaoni." View"

Mfano wanamseti mbwa kw kumtupia mnofu mtoni na wanajua kabisa kuna Mamba,masikini mbwa bila kujua hatari iliyopo mbele yake anaingia mtoni anakumbana na gharika la Mamba.

Nyingine unakuta wanakwenda hifadhini wanamshusha mbwa apambane na simba dume.
Kuku na cobra
Mbuzi na chatu n.k

Huwa naumizwa sana na huu ukatili
 
Kwanza Utuambie Hiyo Serikali ipi unayo Ipa hayo maoni
Ya Mropomaji Au ipi
Wapuuzi nyie
 
Ila kweli kuna watu wanawapiga hao wanyama hadi huruma. Unakuta ng'ombe akienda shamba kulima anapigwa viboko visivyo na idadi.
 
Wagogo wanaongoza kwa ukatili wa wanyama.

IDX murder documentaries: kipengele cha mahusiano na wanyama huwa kinatumika sana kutengeneza basis of murder investigation. Ukiona mtu anamfanyia ukatili mnyama mpaka kumuua au kumjeruhi vibaya awe mbwa, paka au ng'ombe bila huruma basi huyu mtu ni very likely kumfanyia ukatili huu huu mwanadamu.

Wazungu wanaona mbali sana, mtoto anafundishwa tabia ya kuwapenda wanyama tangu utotoni, ukiacha mtoto aendelee na ukatili kwa wanyama huko mbeleni atauhamishia kwa mwanadamu kwasababu ameshazoea kumwaga damu
 
Ni ajabu sana watu wanashindwa kuelewa kuwa hawa wanyama ni viumbe hai na si mashine au mitambo ya kufanyia kazi.

Tatizo serikali imelala kuhusu hili labda mpaka siku tupate mtawala au waziri mwenye dhamana na mifugo ataeamua kulivalia njuga swala hili.

Wazungu walistaarabika miaka mingi sana kwahiyo sio wenzetu katika mambo mengi tu likiwemo la kuthamini wanyama.
 
Ng'ombe tunawafuga kwa kazi kuu tano.
1. Kutulimia.
2. Kuuza tupate kipato.
3. Kupata maziwa na kitoweo.
4. Kutupatia mbolea.
6.ni kutupatia mahari za kuolea.

Kama hutaki wafanye hayo hapo juu fuga wakwako utakaokuwa unawalisha majani na kufurahia kuwatazama tu.
 
Kila ninapona hawa wanyama wanavuta mikokoteni huku wakicharazwa mijeledi, huwa naumia sana na kuona huu ni ukatili dhidi ya wanyama ila uliohalalishwa na mataifa kwa miaka mingi sana.
Kwenye mijeledi hapo ndo tatzo, Mimi nafikiri mfugo awe na Uhuru ukimfunga yoki akikataa kwenda usimlazimishe mtoe tu, atakae taka kwenda aende, ni kama zege tu mbona tunapiga daily😄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…