Haki za wanyama: Serikali ipige marufuku wanyama kama ng'ombe kuvuta mikokoteni

Bado hujawa civilised.
 
Waruhusu tutumie nyati au tembo
 
Mie naona kwa kuwahurumia wanyama serikali ipige marufuku kula nyama kabisa. Wanyama wote wa kufugwa waingizwe mbugani hifadhi za taifa, na tunze na kuwapeleka mbuga mpya ya Chato
 
Kuna shirika linaitwa TAPO kama sikosei la kutetea wanyama lipo Dar karibu na Kisutu ndiyo kazi yake
 
Inatakiwa wafundishwe namna ya kuwatumia hao wanyama na siyo kuwatesa
 
Nyie ndo mtatuletea ushoga na hizi haki zenu, ng'ombe kuvuta mkokoteni unataka apewe haki, hata ukimchinja umekiuka haki yake ya kuishi, binadamu kuvuta mkokoteni naye haki yake ya msingi imeminywa. Tafuta kwanza haki yako kabla ya kutafuta haki ya ng'ombe. Alafu baadae mnalalamika hoo mabeberu wanataka kutuua wakati mnaiga kwao kila kitu. Ukifuata hizi haki kila unachofanya kuna haki umevunja, kitanda cha mbao kuna haki ya mti umeikiuka, ukila samaki amenyimwa haki ya kuishi. Ndugu haki duniani ......
Pia hakuna mnyama aliumbwa kwa ajili ya kilimo
 
Inatakiwa wafundishwe namna ya kuwatumia hao wanyama na siyo kuwatesa
Hakuna mfugaji anayeweza kutesa wanyama wake mwenyewe.

Hivi unajua gharama ya kumpata hata huyo ng'ombe mmoja mpaka akafikie hatua ya kufanya kazi ?
 
Kwenye maandiko ya MUNGU anasema Ni haramu kumchinja mnyama anayefanya KAZI Hadi ajifie mwenyewe KWA maradhi.
 
Vipi dada zetu kubeba ndoo za maji kichwani.

Vipi chinga kubeba buli la kahawa siku nzima

Vipi kusimama kwenye dala dala kwa masaa 2?
 
Haki za Wanyama. Wanyama wana Haki ya Kuishi. Hivyo wasichinjwe.
 
Nimekumbuka kisa kimoja. Miaka ya zamani nilishakamatwa na askari kisa tumeunganisha tolori la kubebea maji kwenye carrier ya baiskeli. Sasa yule askari akadai kuwa Ni kosa, inabidi viwe vimesajiliwa. Hahaha adhabu aliyonipa ni kumwaga maji dumu zote nne. Hawa ng'ombe ilikua kawaida tu kubebeshwa maji. Sometimes wanapeleka nyumba za askari wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…