Kenya 2022 Hakika hakuna cha kujifunza kutoka katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya

Kenya 2022 Hakika hakuna cha kujifunza kutoka katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya

Kenya 2022 General Election
Uchaguzi wa Tanzania, kama kweli upo, ni takataka kabisa na hakuna Afrika nzima. Eti RPC anafahamu wabunge wote na madiwani katika mkoa wake hata kabla ya tarehe ya uchaguzi..!!

Hata huyu IGP mpya aliyeteuliwa majuzi hapo alipo anajua woooote watakaokuwa 'washindi' wa viti vya ubunge, udiwani na urais katika uchaguzi wa mwaka 2025.

Pamoja na mapungufu yaliyopo kwenye uchaguzi wa Kenya lkn huwezi kulinganisha na uchaguzi wa Tanzania ambapo chama kinachoshiriki kwenye uchaguzi ndicho kinaandaa na kuusimamia huo uchaguzi na baadaye kinajitangaza kushinda kwa kishindo. Bure kabisa.
Ulitaka tumchague nani kama hakuna chama mbadala wa CCM? Unataka tuingize nani Ikulu zaidi ya mgombea wa chama tawala ? Upinzani wa Tanzania no hovyo tu.
 
Nikiwa napitia katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini niliona baadhi ya wanaharakati, wafuasi na viongozi wa vyama vya upinzani wakidai kuwa Tanzania inapaswa kujifunza kutoka uchaguzi Mkuu wa Kenya. Wakidai kuwa uchaguzi huo ni huru na wa haki.

Kwa ufuatiliaji nilioufanya katika uchaguzi huo kwa kweli sijaona hicho kinachodiwa kuwa uchaguzi huo ni huru na wa haki. Sioni kama kuna la kujifunza kutoka katika uchaguzi huo kwa sababu zifuatazo:-

#13/08/2022 Daniel Musyoka Msimamizi wa Uchaguzi wa Tume ya Uchaguzi (IEBC) aliripotiwa kutoweka na mpaka sasa haijulikani alipo.

#13/08/2022 iliripotiwa kuhusu uwepo wa dalili za wizi wa kura katika baadhi ya maeneo ambayo inadaiwa William Ruto amepata kura nyingi ambapo ilielezwa kuwa kura katika vifaa vya KIEMS hazilingani na idadi iliyopo katika Makaratasi.

#12/08/2022 iliripotiwa kuwa Maafisa wa Tume wameitisha Kikao cha Dharura baada ya sintofahamu kutokea katika Ukumbi wa kuhakiki kura za Urais, baada ya Kompyuta kuingizwa ukumbini kinyume na Taratibu.

#12/08/2022 iliripotiwa kuhusu msimamizi wa uchaguzi kukutwa na karatasi za kupigia kura katika kituo cha kuhesabia kura cha Jamhuri katika Jimbo la starehe.

#10/08/2022 iliripotiwa kuwa Polisi wawili na Raia mmoja walikutwa na karatasi za kupigia kura zenye tiki. Pia, Miongoni mwa vifaa vingine vilivyokutwa nao ni sahihi moja ya wapiga kura, Madaftari 2 ya matokeo ya Uchaguzi, pakiti mbili za karatasi za kupigia kura za Urais.

# Kubwa zaidi na la kusikitisha ni kwamba mpaka sasa Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) haijatangaza matokeo ya kura za Urais pasipo sababu za msingi huku siku zikizidi kwenda hii inatilia mashaka juu ya matokeo yatakayotangazwa kama yatakuwa na uhalisia.

Katika mazingira haya, kweli watanzania wenye akili timamu wanawezaje kuishauri serikali iige kinachotokea Kenya? Ni kweli kuwa viongozi wa vyama vya upinzani wataweza kusubiri wiki nzima bila kujua aliyeshinda?.

Kitendo cha Vyombo vya habari kutangaza matokeo kiliwafanya wanaharakati pamoja na viongozi wa vyama vya upinzani kuamini kuwa kufanya hivyo ndio uhuru na haki, tujiulize hiyo haki sasa iko wapi? Hivi hamuoni kuwa mlijichanganya kuwahi kuongea bila kufukiria mwisho wa mnachokisema utakuwa nini? Kutofikiria kwenu kumewafanya mkose la kuongea baada ya hali inayoendelea kujitokeza.

Hii ni ishara ya ukosefu wenu wa uweledi katika mambo makubwa yanayohusu uongozi wa nchi.
Wewe endelea kujifunza jinsi ya kukataa fomu za Wagombea wa upinzani na wote wakosee kujaza.
Wafundishe watoto wako jinsi ya kujificha chini ya meza wasipokee fomu za wapinzani wakiwa Wasimamizi wa uchaguzi.
Yule kijana wako mkubwa anayependa upolisi mwelekeze namna sahihi ya kukimbia na maboksi ya kura.
Wafundishe watoto wa jirani yako namna nzuri ya kupiga kura 3 Kituo kimoja bila kushitukiwa.
Huku Tanzania ndo kuna cha kujifunza achana na Kenya hawana lolote.
 
img-20220817-wa0009-jpg.2326316
 
Unataka nikuwekee Kisha wanifanyia kedi!!..huna wakubwa kwenu!!?..kaangalie kwenye makalio ya mama yako
Pole sana, kwa bahati mbaya wakati wa porojo uliishakwisha. Ni wazi kuwa huu ni wakati mgumu sana kwa wa aina zenu, wala matusi hayawezi kukusaidia. Ukijiruhusu kujifunza kukaa kwenye ukweli itakusaidia hata kujenga uwezo wa kutoa hoja zinazolindwa na vielelezo. AMEN
 
Pole sana, kwa bahati mbaya wakati wa porojo uliishakwisha. Ni wazi kuwa huu ni wakati mgumu sana kwa wa aina zenu, wala matusi hayawezi kukusaidia. Ukijiruhusu kujifunza kukaa kwenye ukweli itakusaidia hata kujenga uwezo wa kutoa hoja zinazolindwa na vielelezo. AMEN
Matusi kaanza Nani!!?..una kumbukumbu za ngiri!!?
 
Uchaguzi wa Tanzania ni kituko kama filamu za kihindi kwamba bajaji inashindana na V8 na inashinda!wanaopendelea uongo ndio huvutiwa.

Sent from my BBF100-6 using JamiiForums mobile app
 
Habari za weeknd wakuu..!

Kwa wale tunaoendelea kufuatilia uchaguzi wa majirani zetu naomba nitangulize pole zangu za dhati kwa wote kutokana na kile kinachoendelea.

Baadhi yetu tuliposema kwamba Tume ya uchaguzi na Mipaka Kenya (IEBC) inajiandalia bomu yenyewe kwa kuruhusu media kurusha matokea ya uchagzui huo wapo wana JF walikuja na na mapambio ya media freedom.

View attachment 2323548

Wengine mlikuja na miluzi mingi ya oooh....tujifunze kwa wenzetu...mara oooh kenya baba wa demokrasia...!! Kiko wapiiii?? hadi leo IEBC wanarukaruka na sarakasi za matokeo huku pande zote TEAM BABA (ODINGA) NA TEAM HUSTLERS (RUTO) zimeshaitangaza washindi kutokana na matokeo ya vyombo vya habari ...kwanza nchekee...ha ha ahaaa.

KWA MATUKIO HAYA NDUGU ZANGU NAWAAMBIA WAMESHAFELI...TUWAOMBEE TU WASIPIGANE MAANA HAYA YANAYOENDELEA HAYATAWAACHA SALAMA NA NATHUBUTU KUSEMA TANZANIA HATUNA CHA KUJIFUNZA KATIKA UCHAGUZI WA KENYA ILA IEBC INAPASWA KUJIFUNZA KWETU.
Kuna mtu nilimjibu kuna shida mkiletewa maendeleo bila ustaarabu ni shida.
Hiyo ni shida ya Kenya na nchi nyingine zenye mrengo wa kibepari na zilizojaza wakoloni wao! wakijiita wananchi.
Development without civilization is poisonous!
 
Hiki kinachoendelea kwenye uchaguzi wa nchini Kenya una mambo mengi sana yasiyowezekana Tanzania kwa Katiba na NEC ya sasa. Alafu mtu anaandika kuwa hakuna kipya cha kujifunza. Kweli?? Au ni kiburi za ujinga?
Hivi Tanzania maboksi ya kura yanaweza kupatikana for re-verifications? Hivi servers za NEC zimeshaweka matokeo 2015-2020 online? Je, ni genuine? au alotangazwa ndo alishinda?
Screenshot_20220901-143245.png
 
Hiki kinachoendelea kwenye uchaguzi wa nchini Kenya una mambo mengi sana yasiyowezekana Tanzania kwa Katiba na NEC ya sasa. Alafu mtu anaandika kuwa hakuna kipya cha kujifunza. Kweli?? Au ni kiburi za ujinga?
Hivi Tanzania maboksi ya kura yanaweza kupatikana for re-verifications? Hivi servers za NEC zimeshaweka matokeo 2015-2020 online? Je, ni genuine? au alotangazwa ndo alishinda?View attachment 2342069
Unahangaika na wapumuliwa migongoni Si utachoka bule

Sent from my Nokia 4.2 using JamiiForums mobile app
 
Wakili wa Ruto, Msomi Fred Ngatia amemaliza kila kitu. Kwamba fomu iliyopo kwenye server ya IEBC ni fake. Sasa kama ni fake na ipo kwenye server ilifikaje fikaje? Na kwanini iwe na jina la raia wa Venezuela?

Najua kuna Watanzania wenzangu hawapendi kinachoendelea sasa kule Kenya wakiamini uchaguzi ulishaisha. Lakini uhakika ni kuwa bado. Na hii kesi inarushwa live wenye nchi ya Wakenya waone!
Sisi NEC ikishatangaza ni final hata kama ushindi haueleweki! Oneni uchaguzi unavyowezs chakachuliwa!
Tuna mengi ya kujifunza!
Screenshot_20220902-221340.png
Screenshot_20220902-222204.png
Screenshot_20220902-222349.png
 
Back
Top Bottom