Hakika Mungu yupo na Watanzania. Ogopa Sana nchi ambayo watu wake si wepesi wa kuingia mtaani

Tangu lini ccm imeanza kutokuwa na shida?
Kwahiyo Mungu anavumilia utawala wa Kagame huko Rwanda bado hajashindwa kuvumilia?
kwani ni lini ulinisoma nikisema kuwa CCM ina shida? aliyekuwa na shida ni Magufuli.
Kagame hafanyii propaganda kwenye dini na Mungu. Magufuli aliwatumia viongozi wa Dini kujipigia kampeni za uchaguzi, kusifia utawala wake, na aliwatisha viongozi kwa kuwapora passport na kuwatukana kupitia vibaraka wake kama akina Musiba, kukejeli viongozi wa dini wanapotoa ushauri na hata kuwaita hawana imani, yaani alijifanya kuwa kiongozi mkuu wa dini. Hii ni kufuru kubwa ambayo sidhani kama Kagame anaifanya
 
Watanzania hawana tofauti na watu wengine wala mataifa mengine. Bado hawajafikishwa mahali wakaingia mitaani. Hata ambao wameishaingia walijikuta mitaani. Nadhani sababu kubwa si upole wetu au ujinga kama wengine wanavyodhani. Bado Tanzania ni nchi tajiri katika nchi nyingi duniani. Hebu linganisha kiwango cha maisha chetu na majirani zetu ambao umaskini ushawatafuna hadi kwenye mfupa.
Hehehe
 
Legacy ya kubambikia watu Kodi na kupora Mali zao imetemwa Jana hadharani.
Mama ameliona hilo, nadhani analiweka sawa. Ila kakosea sana kumweka Mwigulu Nchemba pale wizarani, yeye ni mmojawapo wa watu wasiopenda utangamano wa nchi hii. Ni sehemu ya waliokuwa wana terrorize raia, alipokuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi. TRA kwa sasa iko chini yake, unadhani ataacha ku terrorize walipa kodi kwa kutumia nyenzo zilizopo?
 
Kwamba nchi nyingine zote juu ya uso wa dunia zenye machafuko, ina maana watu wake hawaombi amani kwa Mungu??
 
kwani ni lini ulinisoma nikisema kuwa CCM ina shida? aliyekuwa na shida ni Magufuli.
Kagame hafanyii propaganda kwenye dini na Mungu. Magufuli aliwatumia viongozi wa Dini kujipigia kampeni za uchaguzi, kusifia utawala wake, na aliwatisha viongozi kwa kuwapora passport na kuwatukana kupitia vibaraka wake kama akina Musiba, kukejeli viongozi wa dini wanapotoa ushauri na hata kuwaita hawana imani, yaani alijifanya kuwa kiongozi mkuu wa dini. Hii ni kufuru kubwa ambayo sidhani kama Kagame anaifanya
Kama si ccm basi Magufuli asingekuwa mtawala wa hii nchi, ni ccm ndio iliyohakikisha kuwa Magufuli lazima awe mtawala wa hii nchi kihalali au kiharamu ila wewe huoni tatizo hapo.

Nimekuuliza utawala wa Kagame huko Rwanda Mungu bado anauvumilia?Au Mungu yeye hawezi kuvumilia viongozi wa dini wakinyanyaswa tu ila viumbe wake wengine hata wakiwa wanauliwa kabisa yeye kwake sio ishu?
 
CCM ilikosea hawakujua Magufuli angekuwa mnyama vile ila kumtoa isingewezekana sababu ndio walishampa power. Ni kama CHADEMA walivyokosea kwa Lowassa au ACT kwa Membe, so vyma vya siasa vinakosea pia
Si nimeshakujibu kuhusu Kagame? au hujasoma jibu langu vizuri?
 
Hawakujua angekuwa mnyama vile kwa viongozi wa dini tu au kwa watu wote pamoja na wao ccm? ccm hawakuwahi kusema kuwa walikosea kwa Magufuli hakuna hata kiongozi mmoja aliyeamua kuachia madaraka kwa kutokukubaliana na anayoyafanya Magufuli,l eo hii ndio tuona baadhi ya wana ccm wakieleza mambo ambayo yapo kinyume na iliyokuwa misimamo ya Magufuli kama si unafki ni nini na unaachaje sasa hapo kuona ccm ni tatizo?

Suala la Kagame ulichokijibu sicho nilicho kuuliza,mimi nakuuliza Mungu anavumilia utawala wa Kagame huko Rwanda? kwa sababu anayoyafanya Kagame huko Rwanda yanajulikana ndio nauliza kwamba Mungu anaweza kuyavumilia kwa sababu hayahusu viongozi wa dini?
 
Kuendelea kumtegemea MUNGU kwa makosa na matatizo yenu wenyewe kwa wenyewe ni uthibitisho kuwa akili zenu aidha ni ndogo sana, dhaifu, za kinyonge au hazipo sawa sawa kuweza kuleta mabadiliko chanya...
 
Hawakujua angekuwa mnyama vile kwa viongozi wa dini tu au kwa watu wote pamoja na wao ccm? ccm hawakuwahi kusema kuwa walikosea kwa Magufuli hakuna hata kiongozi mmoja aliyeamua kuachia madaraka kwa kutokukubaliana na anayoyafanya Magufuli,l eo hii ndio tuona baadhi ya wana ccm wakieleza mambo ambayo yapo kinyume na iliyokuwa misimamo ya Magufuli kama si unafki ni nini na unaachaje sasa hapo kuona ccm ni tatizo?

Suala la Kagame ulichokijibu sicho nilicho kuuliza,mimi nakuuliza Mungu anavumilia utawala wa Kagame huko Rwanda? kwa sababu anayoyafanya Kagame huko Rwanda yanajulikana ndio nauliza kwamba Mungu anaweza kuyavumilia kwa sababu hayahusu viongozi wa dini?
sasa wangemkosoa Magufuli unajua ambacho kingewakuta? Viongozi wa Dini wenyewe kama akina Kakobe waliponea kufilisiwa sembeuse wanasiasa wenzake? uliona Nyalandu kilichomkuta kwa kumtembelea tu Tundu Lissu hospitali?

kwani Kagame anafanya nini haswa, labda unajua kitu ambacho mimi sijui
 
Wana ccm walikuwa wanamsifia kabisa na walikuwa wanafanya hivyo kwa manufaa yao binafsi wala sidhani kama walitishiwa kwa kulazimishwa kumsifia,kwahiyo watu hawamkumkosoa sio kuogopa atawadhuru bali ni kwa sababu za kulinda masilahi yao binafsi wengi wana maovu yao hivyo kwa kuyalinda hayo ndio hulazimika kukaa kimya au kusifia kabisa,hiyo ndio ccm mkuu ila ajabu wewe huoni kuwa ni tatizo.

Kagame mtu ambaye alikuwa anaambiwa anamfundisha Magufuli udikteta sidhani kama nina haja ya kuelezea mambo ya Kagame.
 
Na sasahivi tunaanza maombi ya kuwang'oa wote waliopata nafasi pasipo mpango wa Mungu!
Yaani tunaamuru viti viwatapike tu hakuna namna! Mwenyewe washaelewa sbb wanajua walikovipata.
 
Wana ccm walikuwa wanamsifia kabisa na walikuwa wanafanya hivyo kwa manufaa yao binafsi wala sidhani kama walitishiwa kwa kulazimishwa kumsifia,kwahiyo watu hawamkumkosoa sio kuogopa atawadhuru bali ni kwa sababu za kulinda masilahi yao binafsi wengi wana maovu yao hivyo kwa kuyalinda hayo ndio hulazimika kukaa kimya au kusifia kabisa,hiyo ndio ccm mkuu ila ajabu wewe huoni kuwa ni tatizo.

Kagame mtu ambaye alikuwa anaambiwa anamfundisha Magufuli udikteta sidhani kama nina haja ya kuelezea mambo ya Kagame.
Siasa ndivyo zilivyo. walikuwa wanamifia kwa maslahi yao ndiyo, na wanasiasa wote ndivyo walivyo, wasingemsifia hata ubunge wao wasingeutetea. vyama vyote vya siasa husifia viongozi wao hata kama wanafanya vibaya, kinyume na hapo ujiuzulu na uhamie chama kingine.
na jiwe alihakikisha hakuna mwana CCM anayeweza kuhama chama na akafanikiwa kwa kutumia nyingi kuhujumu upinzani

Wewe unasema Kaga,me mbaya ukiambiwa utaje ubaya wake unadai kuwa wanasema ndiye alimfundish Magufuli udikteta? hao wanaosema hivyo maneno yao ndio ukweli au?
 
Back
Top Bottom