Hakika Uchawi Upo: Nimeutumia kwenye Kesi yangu mahakamani na Nimeshinda

Hakika Uchawi Upo: Nimeutumia kwenye Kesi yangu mahakamani na Nimeshinda

Amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu na moyoni amemwacha Mungu...

Hapo unaona umeshinda kesi...

Ila umeweka agano na mganga litakutesa kizazi na kizazi...
Naomba ufafanuzi juu ya suala la kumtegemea mwanadamu kwa maana ukiajiriwa unategemea mwajiri akulipe Je, huko sio kumtegemea mwanadamu?
Au kuahidiwa Jambo hususani msaada wa kitu fulani, Je huko Nako sio kumtegemea mwanadamu,
Au kumtegemea daktari katika matibabu
 
Wapo mashekhe na wachungaji wanaofanya wallet za waumini zao ni migodi yao ya pesa.

Weka hii akilini....
Naona kiuka misingi ya waaminicho wapo kila Kona ya duniani.

Ila pia wanaotenda sawasawa na Imani zao zitakavyo pia WAPO.

#YNWA
Uwepo wa Manabii wa Uwongo, ndo kigezo cha wewe kujitetea na kusema Sitaki Kumtegemea Mungu mimi nitategemea waganga??

Hakika Ujinga huo unakutafuna hata sasa.
 
The point is Mil 8 NILIIPATA Tena na gharama ya kesi nililipwa.
Total nilikusanya kama Mil 10.

ULITAKA niwaachie Hakimu na Mshtakiwa wanipige dili?

Bro ushawahi tapeliwa kweli au ndio MOTIVATIONAL SPEAKER anayekwambia jiajiri huku yeye katumwa na Sido (Mwajiri wake) kukufundisha wewe kujiajiri?

#YNWA
Mimi sikuhukumu kwa lolote, chochote ulichofanya kiwe kizuri kiwe kibaya sio mada yangu.
My point ni Acha kumtegemea Mwanadamu, Anza kujifunza kumtegemea Mungu muumba wetu.
 
Naomba ufafanuzi juu ya suala la kumtegemea mwanadamu kwa maana ukiajiriwa unategemea mwajiri akulipe Je, huko sio kumtegemea mwanadamu?
Au kuahidiwa Jambo hususani msaada wa kitu fulani, Je huko Nako sio kumtegemea mwanadamu,
Au kumtegemea daktari katika matibabu
Kwa nijuavyo mimi ni katika roho ndio maana anasema moyoni amemwacha Mungu. Na automatically ukimtegemea moyoni ni katika ulimwengu wa nyama itafuatia.

Mambo mengine tumeumbwa kutegemeana
 
Mimi sikuhukumu kwa lolote, chochote ulichofanya kiwe kizuri kiwe kibaya sio mada yangu.
My point ni Acha kumtegemea Mwanadamu, Anza kujifunza kumtegemea Mungu muumba wetu.
Nguvu ya kushinda alikuwa nayo ila hakujua namna ya kuipata toka kwa chanzo ambaye ni Mungu. Huyo mganga hiyo nguvu anaipata toka kwa Mungu ni kwamba amemwaminisha mhusika kuwa anaweza na akaweza kwa nguvu ya Mungu iliyopo ndani yake.

Ni kujifunza na kumrudishia utukufu Mungu kwani yeye anachotaka ni moyo wa shukrani tu.
 
Naomba ufafanuzi juu ya suala la kumtegemea mwanadamu kwa maana ukiajiriwa unategemea mwajiri akulipe Je, huko sio kumtegemea mwanadamu?
Au kuahidiwa Jambo hususani msaada wa kitu fulani, Je huko Nako sio kumtegemea mwanadamu,
Au kumtegemea daktari katika matibabu

Kwa nijuavyo mimi ni katika roho ndio maana anasema moyoni amemwacha Mungu. Na automatically ukimtegemea moyoni ni katika ulimwengu wa nyama itafuatia.

Mambo mengine tumeumbwa kutegemeana
Nadhani utakua umeelewa, majibu uliyopewa.
Ni kumtegemea Mungu kiroho (akilini)
roho huyo ndie atakwambia nenda hospital fulani utapata huduma nzuri,
kula chakula hiki kinafaa kwa mwili wako.

Mwanadamu unatakiwa kumtafuta Mungu kiroho, roho ilianza kutengenezwa ndipo mwili ukafata kutengenezwa
 
Nguvu ya kushinda alikuwa nayo ila hakujua namna ya kuipata toka kwa chanzo ambaye ni Mungu. Huyo mganga hiyo nguvu anaipata toka kwa Mungu ni kwamba amemwaminisha mhusika kuwa anaweza na akaweza kwa nguvu ya Mungu iliyopo ndani yake.

Ni kujifunza na kumrudishia utukufu Mungu kwani yeye anachotaka ni moyo wa shukrani tu.
Hakuna kitu kama hicho.
Ukisema hivo unamaanisha Shetani/ibirisi hayupo.
Na shetani ndio anataka hivo wewe utambue kua yeye ndie Mungu na umtumikie kwa kudhani ndie Muumba wako kumbe ni uwongo na mwisho wa siku utahukumiwa pamoja nae.
 
Nguvu iliyopo ni moja.

Isipokuwa mtu anachagua aitumie vipi. Ni sawa na nguvu ya umeme unaweza kuchagua kuitumia kwa mambo mbalimbali.

Shida au shetani yupo rohoni/ kichwani/moyoni/ mwa mwanadamu. Kivipi? Tabia, imani. Ndio maana ukitanguliza kanuni ya upendo/nuru katika chaguzi shetani hana nafasi ya kupendekeza jambo na utachagua nuru au itaongozwa na nuru au ukweli huo kuchagua. Kinyume cha hapo utatafuta waganga mpaka wote.

Nguvu ni moja.
 
Uwepo wa Manabii wa Uwongo, ndo kigezo cha wewe kujitetea na kusema Sitaki Kumtegemea Mungu mimi nitategemea waganga??

Hakika Ujinga huo unakutafuna hata sasa.
Sijamtegemea mganga.
Ila mganga huomba kwa Mungu.

Kama alivyo Mchungaji na shekhe.

Iko hivi ......

Hata babu zako wa ukoo wako walitumia matambiko miaka hiyo ila walikuja wazungu wakawaambia "Wanazingua" ndipo tukamezeshwa Imani za wageni.

Ila nikwambie tu babu zako...
Waliomba milimani mvua ikaja,
Wakaomba matibabu yakaja,
Wakaomba mavuno kipindi cha njaa yakaja.

RESPECT AFRICAN RELIGION.

#YNWA
 
Hebu kaa mbali na sisi bwana...
Wew ulijuaje kwamba ulishinda sababu ya uchawi ?

Wakati mwingine mkumbukeni basi Allah kuwa yupo hata kama hamuamini uwepo wake

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Sijamtegemea mganga.
Ila mganga huomba kwa Mungu.

Kama alivyo Mchungaji na shekhe.

Iko hivi ......

Hata babu zako wa ukoo wako walitumia matambiko miaka hiyo ila walikuja wazungu wakawaambia "Wanazingua" ndipo tukamezeshwa Imani za wageni.

Ila nikwambie tu babu zako...
Waliomba milimani mvua ikaja,
Wakaomba matibabu yakaja,
Wakaomba mavuno kipindi cha njaa yakaja.

RESPECT AFRICAN RELIGION.

#YNWA
Huu ndo ujinga ambao mnatumia kujitetea nao.

Unajua ni jinsi gani watu waliteseka kwenye utawala wa machifu??
Walipokosa mvua, unajua gharama zilizowapata hadi kuja kupata hiyo mvua?? na kwanini mvua ilikosekana.

Ukiambiwa uongozwe ma chifu wewe na uvae kaniki utakubali???
usishadadie ujinga na huku Unatumua smartphone ya mzungu.

Unasema mganga anamuomba Mungu na miungu unadhani inaabudiwa na nani??
au unataka kujitoa akili kuwa hakuna miungu?

Sikulazimishi Kuachana Na waganga.
Lakini iko wazi, wote mnaokwenda kwa waganga ndio walogaji wakubwa kazi kurudisha maendeleo nyuma ya watu wasio na imani.
kesho utaenda kutafuta utajiri kwa waganga, kesho kutwa utaenda kumzindika demu wako, then utaenda kutafuta mvuto wa mapenzi, utachanjwa chale na kulishwa mavi na waganga hadi uchakae uwe na sura kama mbuzi kabanwa kunya 🤣🤣🤣
 
Hakuna utawala ambao hujawahi semwa vibaya.
Ukiambiwa uongozwe ma chifu wewe na uvae kaniki utakubali???
usishadadie ujinga na huku Unatumua smartphone ya mzungu.
Maendeleo yasikufanye uone yako ni mabaya ila waliokuletea ndio mazuri.
Unasema mganga anamuomba Mungu na miungu unadhani inaabudiwa na nani??
au unataka kujitoa akili kuwa hakuna miungu?
Mganga anamuomba Mungu yule yule ambae Mchungaji na shekhe wanamuomba.
Sikulazimishi Kuachana Na waganga.
Lakini iko wazi, wote mnaokwenda kwa waganga ndio walogaji wakubwa kazi kurudisha maendeleo nyuma ya watu wasio na imani.
kesho utaenda kutafuta utajiri kwa waganga, kesho kutwa utaenda kumzindika demu wako, then utaenda kutafuta mvuto wa mapenzi, utachanjwa chale na kulishwa mavi na waganga hadi uchakae uwe na sura kama mbuzi kabanwa kunya 🤣🤣🤣
Kila sehemu wapo wabaya...
Kwenda kanisani kuomba ni kuzuri ila ukienda kwasababu ya kutafuta mademu SI VIZURI.

Kwenda kwa mganga kama nilivyokwenda si vibaya ila ukienda kwasababu ya kuloga sio vizuri.

Hujawahi ona mtu anatumia Quran kusoma albadili, ina maana uislamu ni mbaya?

Halafu mwisho utaandika nimtegemee Mchungaji kunisalia au shekhe kunipigia kisomo.

Yaani unaamini yaliyoletwa ni Bora kuliko tuliyokuwa nayo..!!

NB:
Wapo...
Mashekhe wajinga
Wachungaji wasiojielewa
Waganga washenz*

#YNWA
 
Iko hivi....
Wapo wachungaji matapeli NADHANI UNAWAJUA,
wapo mashekhe waongo NADHANI UMEWASIKIA,
Wapo Waganga matapeli NDIO HAO ULIOKUTANA NAO,

Kifupi kila jambo na taaluma kuna waongo wasiojua nini wanafanya na WENYE UJUZI WAO.

#YNWA
Nimekutana na mganga tena hao fake hapo nimeweka bayana sikutaka hata kujihusisha na mganga nime declare kabisa waganga kwangu hawawezi kuwa sehemu ya kunitatulia matatizo, sema ndiyo hivyo tumetofautiana namna ya kutatua matatizo kila mtu ana approach zake base on his/her beliefs
 
Yap.

Ni wilaya ya Rukwa.
Imemegwa kutoka wilaya ya Sumbawanga kipindi kile cha kuanzisha Wilaya ya mikoa mipya.

Kama sijakosea ilianza 2014 na makao makuu yalikuwa Sumbawanga mjini.

Magu alivyopiga biti kila halmashauri iende kwake ndio Kalambo ikaenda Matai, hivyo makao makuu ya Wilaya/Halmashauri yapo Matai.

Na inapakana na Wilaya ya Momba (Mkoa wa Songwe).

Kufika Matai Kuna boda unapitia Momba (Kasinde, mpakani na Zambia - Gari unapandia Tunduma) na Kuna boda la kawaida unapitia Sumbawanga mjini (gari unapandia Sumbawanga mjini).

#YNWA
Mkuu naomba connection kunamtu kateleza na thaman ya mistubishi outlinder na nipo rukwa
 
Eeh bwana eeh ni yule yule Mr. Liverpool A.K.A bingwa wa EPL na bingwa wa NBC PL (Mwananchi).

NB:-
Naleta uzi huu si kwa lengo la kutangaza biashara au vipi ila ni KUTOA USHUHUDA WA MAMBO YA DUNIA..!!

FLACK BACK
Mwaka jana mwezi wa 4 nililetewa idea ya biashara na bosi fulani hivi wa huku town nilipo.

Akasema mtaji ni Mimi kuchangia Mil 5 tu ili niwe mshiriki wa hiyo biashara.
Nilimuita ofisini na tukaandikishiana na kumkabidhi hela.

Trip ya kwanza alileta mzigo kamili, tukauza na kupata faida ya mil 4, tukagawana na ule mtaji ikawa nimerudisha mil 7.

Mweki wa 8 ukanifata Tena, akasema safari hii nitoe mtaji mkubwa ili tukapige mshindo mkubwa.

Tukakabidhiana Mil 8.

Zilipita siku, nikawa nikipiga simu hapokei, na nikipiga kwa namba ngeni ananijibu yupo kijijini nisiwe nashaka.

THE PROBLEM
Kwenye mwezi wa 10 mwaka jana, nikiwa kwenye mihangaiko mjini nikamuona.
Ghafla ile na yeye kuniona akakimbia.
Mmmh kichwa kikawaza ""Nishatapeliwa, maana aliniambia yupo kijijini anakusanya mzigo ila nimemuona mjini, na nilivyomuona kanikimbia""

Ikabidi niende kwake usiku, nikamkuta mkewe nikamueleza.
Mkewe akawa ananipa hopeee

ila imefika mwezi wa 11 mwaka jana mkewe nae ananijibu shit ""mlipo kabidhiana hela tulikua wote""

Nikamtafuta rafiki yake, huyu rafiki mwanzo alikua kama ananisaidia hivi ila nae baadae akageuka.

Kufika January, nikaona kimbilio ni polisi.
Kufika Polisi mpelelezi wa jalada langu akaniambia ""Huyu ana marafiki wengi mapolisi, usikubali muelewane hapa, siku za huko mbele atakuzingua nenda mkaelewane mahakamani""

Maana hata siku anaitwa polisi alikua anasalimiana na polisi wengii kishkaji.

Nikafungua kesi mahakama ya mwanzo ""Kosa la kujipatia hela kwa njia za udanganyifu""

Shauri langu likatembea mara Tano (kila wiki mara moja).
Jalada likafungwa.

Likafunguliwa lake.
Kipindi chotee cha kesi hakua na shida wala wasiwasi.

Siku ya kwanza ya upande wake, alisema ""Nilimpa pesa kwa kumsaidia na sio biashara""
Akatoa ushahidi na maneno kibaoo (na hata sijui ushahidi ule aliupata wapi).

Tukaitwa mara ya pili kwenye jalada lake.
Wakaja mashahidi hata nilikua siwajui (mashahidi wa mchongo).

Dah nilivyotoka siku ile nikaona hapa naelekea kushindwa hii kesi.

Ikabidi nimtafute yule askari mpelelezi anishauri.
Dah huyu ndio alinichosha, asiniambie kumbe jamaa anajua mpaka na mume wa hakimu wa kesi yetu.

Yaani nilidata..!!

Kuna siku nipo na enjoy na pisi moja, ikaniona Nina mawazo.
Ikaniuliza nikamuhadithia.

Akaniambia ""Naomba nikusaidie"" nikamjibu sawa.
Usiku ule tulikula starehe asubuhi akaniachia namba ya babu mmoja hivi, kwamba nimtafute nimueleze shida zangu.

Nikampigia babu tukaongea.
Akaniambia niende kwake.

Nikapanda gari (nauli 1000 tu) mpaka kwake.
Babu akanifanyia Mandingo ya kienyeji na kunipa dawa fulani hivi kaifunga kwenye karatasi.

Akasema ""Ukiwa unaenda mahakamani iweke mfuko upande wa kulia, ukingia ukumbi wa mahakama ibadilishe weka mfuko wa kushoto na mtu yoyote akianza kuongea uwe unaiminya dawa"

Siku ya mahakama (siku ya 3 ya jalada lake) ikawadia.
Ikawa akiongea hakimu, shahidi au mdaiwa wangu BASI NAMINYA DAWA.

Eeeh bwana eeh nyie ""Uchawi upo"".
Hakimu akanipa nafasi kuuliza shahidi wa mshtakiwa, eeh wale mashahidi si wakawa wanaropoka tu.

Kuna mmoja ile nimemuuliiza swali nikaminya dawa nikasikia ""Huyu mshtaki hata simjui ndio kwanza namuona Leo""
Mara ""Hata sijui hapa nilikuja kufanya nini""

Upande wake mdaiwa/mshtakiwa ukaisha.
Jalada likafungwa....

Tukatajiwa tarehe ya hukumu.

Dah nikampa taarifa babu.

Babu akaniita Tena.

Akafanya mandingo yake na kunipa dawa ya kuoga, nioge asubuhi (alfajiri) siku ya hukumu.

Siku ya hukumu ikawadia, nikatekeleza masharti.
Kwenda mahakamani ""Hukumu imehahirishwa"" ikapangiwa siku nyengine.

Nikampa taarifa babu.
Babu akaniita. Babu akachukua matunguli kachekii nikasikia ""Wanatutania hawa, Hawajui haki ya mtu hailiwi kijinga?""

Babu akanipa dawa nyengine, ya kuoga siku ya hukumu na kuweka mfukoni. Nikasikia babu ananiambia ""Wakitoka hapa basi wao nomaa""

Siku ya hukumu nikaoga na kuwahi mahakamani.

Kesi yetu ikaitwa.
Hakimu, mimi na mshtakiwa tupo pamoja ukumbini.

Wakati hakimu anasoma hukumu mimi nikawa naminya ile dawa kalii ya babu.

Niliminyaaa kama mara 5 nikaona hakimu kiti hakikaliki, akainuka akatoka.
Kakaa kama dakika 2 akarudi tena ukumbini.

Kusoma hukumu NIMESHINDA na natakiwa kurudishiwa pesa zangu.

Jamaa akahukumiwa kufungwa miezi 3 jela na 6 kifungo cha nje.

Ile kujitetea nikaona hakimu anampunguzia na kumpa miezi 6 kifungo cha nje na arudishe pesa zangu ndani ya mwezi.

Dah nikatoka kwa furaha mahakamani.

Nikamtafuta babu, babu akanipa siku ya kwenda nikiwa na kuku wawili (majogoo) na mchele kilo 5.

Kufika ile siku nikaenda, wale kuku babu akawafanyia mandingo na kuwachinja.

Ubwabwa wa kuku ukapikwa, wakaalikwa watoto tuuu wa majirani waje kula.

Walivyomaliza kula, ile jioni babu akaniita ndani ya ofisi.

Malipo yake akasema 30,000/= niweke chini ya mkeka halafu niondoke nisigeuke nyuma mpaka nikimaliza eneo la nyumba yake.

Mimi sikugeuka nyuma kabisaa mpaka nikapotelea mitaani kwenda stendi ili nirudi home.

Dah hayo ndio yakawa malipo ya Kazi ya babu.

Eeh bwana eeh UCHAWI UPO na UNAFANYA KAZI.

#YNWA
Kwa kulipa 30,000 na hayo masharti umeshaingizwa kwenye maagano ya giza. Bado kuna gharama utazilipia zaidi ni swala la muda tu!
 
Hakuna utawala ambao hujawahi semwa vibaya.

Maendeleo yasikufanye uone yako ni mabaya ila waliokuletea ndio mazuri.

Mganga anamuomba Mungu yule yule ambae Mchungaji na shekhe wanamuomba.

Kila sehemu wapo wabaya...
Kwenda kanisani kuomba ni kuzuri ila ukienda kwasababu ya kutafuta mademu SI VIZURI.

Kwenda kwa mganga kama nilivyokwenda si vibaya ila ukienda kwasababu ya kuloga sio vizuri.

Hujawahi ona mtu anatumia Quran kusoma albadili, ina maana uislamu ni mbaya?

Halafu mwisho utaandika nimtegemee Mchungaji kunisalia au shekhe kunipigia kisomo.

Yaani unaamini yaliyoletwa ni Bora kuliko tuliyokuwa nayo..!!

NB:
Wapo...
Mashekhe wajinga
Wachungaji wasiojielewa
Waganga washenz*

#YNWA
uislamu ni mbaya ndio, pigia mstari.
🤣🤣🤣🤣🤣 acha kujitetea mshirikina wewe.

na nimekukataza kujitetea kwa kusema kuna wachungaji na manabii wa uwongo.

umedanganywa mganga anatumika na Mungu.

endelea kuwa na shingo ngumu, tuone utafika wapi.

Yaishe hutaki kuacha, komaa na ushirikina wako, toa kafara sana utatoboa tu.
 
Fungua macho uelimike.

1. Si lazima utoe kafara ili usaidike.
Kwenye scenario yangu, NILITOA KAFARA NINI?

2. Na infact ULITAKA NIDHULUMIWE?

3. Unaposema uislamu ni mbaya kwasababu ya ukristo wako, huku umerithi hiyo Imani kutoka kwa wazazi na kutoka kwa wazungu (wamishioneri).
Hivi unajua ungezaliwa na muhindi muda huu ungekuwa una mwabudu "Krishna"?

#YNWA
 
Back
Top Bottom