chai ya rangi
JF-Expert Member
- Mar 7, 2026
- 1,042
- 3,095
hata yeye mwenyewe ShesRise_1 hawezi
watu wote waelewe mapema kwamba kuna baadhi ya mioyo ikikutana, hata dunia ikijaribu kuzitenganisha hushindwa.
Mimi na yeye hatukuunganishwa na bahati, wala maneno matupu ya mapenzi ya kupita. Kuna namna macho yake yalivyoutambua moyo wangu kabla hata majina yetu hayajazoeana.
Yeye si mwanamke wa kawaida kwenye maisha yangu.
Ni utulivu wangu katikati ya vurugu, ni mwanga wangu kwenye siku zenye giza, ni sauti ambayo moyo wangu huisikia hata akiwa kimya.
Na kama ulimwengu ni bahari yenye mawimbi mengi, basi yeye ndiye ufukwe ambao moyo wangu uliamua kupumzika milele.
Hakuna umbali utakaoweza kufuta hisia hizi.
Hakuna maneno ya watu yatakayoweza kuyeyusha kilichojengwa na mioyo miwili iliyochaguana kwasababu mapenzi yetu hayaishi kwenye macho pekee baki huishi ndani kabisa ya nafsi.
Na yeye…
tayari amekuwa sehemu ya pumzi zangu.