chai ya rangi
JF-Expert Member
- Mar 7, 2026
- 1,042
- 3,095
Hakuna umbali utakaoweza kufuta hisia hizi.hata yeye mwenyewe ShesRise_1 hawezi
watu wote waelewe mapema kwamba kuna baadhi ya mioyo ikikutana, hata dunia ikijaribu kuzitenganisha hushindwa.
Mimi na yeye hatukuunganishwa na bahati, wala maneno matupu ya mapenzi ya kupita. Kuna namna macho yake yalivyoutambua moyo wangu kabla hata majina yetu hayajazoeana.
Yeye si mwanamke wa kawaida kwenye maisha yangu.
Ni utulivu wangu katikati ya vurugu, ni mwanga wangu kwenye siku zenye giza, ni sauti ambayo moyo wangu huisikia hata akiwa kimya.
Na kama ulimwengu ni bahari yenye mawimbi mengi, basi yeye ndiye ufukwe ambao moyo wangu uliamua kupumzika milele.
Hakuna umbali utakaoweza kufuta hisia hizi.
Hakuna maneno ya watu yatakayoweza kuyeyusha kilichojengwa na mioyo miwili iliyochaguana kwasababu mapenzi yetu hayaishi kwenye macho pekee baki huishi ndani kabisa ya nafsi.
Na yeye…
tayari amekuwa sehemu ya pumzi zangu.
BABA MKWE AMEONGEAChukua hii umtag😂
Kikombe cha Sukari, Jua la Maisha Yangu
Kwenye jukwaa la maisha, urembo wako unang'aa,
ShesRise_1 mpenzi, nyota yangu ya kapu la baraka,
Kila unapochomoza,
giza langu lote linatoweka,
Wewe ni jua langu,
unaamsha ari na hamasa.
Mimi ni chai ya rangi, niliyepata mtamu wake,
Wewe ndio sukari yenyewe, ladha ya maisha yangu,
Bila wewe kubandikwa moyoni, mimi bado mchungu,
Tupike pamoja upendo,
udumu kwenye ulimwengu wetu.
Kwenye nyuzi za JF,
nakutafuta kwa hamu sana,
Macho yangu ya mtandaoni, yanatamani picha yako,
Sauti yako ya maandishi, inanikosha roho yangu,
Nataka dunia ijue,
wewe ndio chaguo langu pekee.Inuka mpenzi wangu (ShesRise_1), uangazie hii safari,
Shika mkono wa chai ya rangi,
tuelekee kwenye heri,
Mapenzi yetu yawe mfano, yasiishe kama uturi,
Niseme nini tena mrembo? Nakupenda kwa dhati ya moyo💖💖🔥.
Hisia ni jambo kubwa sanaHuku kujiamlia mambo sasa naona kumezidi 😸😌
Hapana kabisaSitostaajabu ikiwa muandika uzi na mtajwa kwenye uzi ni mtu mmoja huyo huyo.
Aise noma umenikumbusha mbali sana cheki hili swali,Kweli vijana wamevurugwa, nyege zinawafanya mjifunze fasihi kwa hali na mali.
Habari yako bro, hivi skuizi humu jf kuna Ke🤔Mkono mtupu aulambwi
jamiichek itakwambia "si kweli"Mbona minajua huyo ni Me...🤔