Mimi nilikua mshabiki mkubwa wa kiba hapo mwanzo, na nakiri nilikua simkubali Diamond kabisa, lkn ujio wa mara ya pili wa kiba baada ya kupotea kwa muda mrefu ulionyesha dhahiri amekuja kumkabili Diamond, maana alikua akipushiwa zaidi na watu wasiomkubali diamond, baada ya hapo matukio mengi yaliyotokea baada ya hapo likiwemo la mond kuzomewa Fiesta yalidhihirisha ujio wa pili wa kiba ulikua wa shari dhidi ya mond, baada ya mashabiki kumwambia yeye ni mkali kuliko mond, na hapa mm ndipo nilipomkataa rasmi Kiba na kuhamia kwa mond, washabiki walijitahidi kumbeba kila walivyoweza, ila mond anazidi kuchanja mbuga tena kwa kasi mara mbili ya mwanzo, tulipofika sasa Kiba amepoteza mashabiki wake wengi sana, na waliobaki wamechoka kumbeba, huku lengo la kumshusha mond likiwa halijatimia. hiki ndio kinachozidi kumchanganya kiba, matokeo yake anaongea vitu vya ajabu ajabu, amepoteza muelekeo hajui njia ya kupita ili amkute mond, maana yuko mbali sana, anachofanya ni kutafuta njia ya mkato ili amfikie, na hii si nyingine ni kujaribu kumshusha kwa kumchafua mbele ya mashabiki wa muziki, naiona hata hii njia ya mkato ikishindikana. Ally rudi nyuma tengeneza njia yako ili uende utakavyo, diamond kwa sasa muache tuu