Hakuna cha introvert wala nini, ni watu wenye jeuri na kiburi wenye kuona sauti zao zina thamani sana

Hakuna cha introvert wala nini, ni watu wenye jeuri na kiburi wenye kuona sauti zao zina thamani sana

Introversion ipo karne na karne labda hilo neno ndio jipya tu na pia hivi karibuni watu wamejifunza sana kuhusu introversion kiasi cha wengi wao kujikubali na kuwa comfortable tofauti na zamani ambapo iliaminika kwa wengi kuwa introvert ni tatizo na binadamu by nature ni extrovert.

Karibu moja ya tatu ya watu duniani ni introverts.

Dunia ya leo kila mtu anajidai ni introvert, extroverts hawapo kabisa.

Mara ya mwisho lini umesikia mtu anadai yeye ni extovert? Hawapo. Sasa it's more of a trend.
 
Dunia ya leo kila mtu ni hao introverts, extroverts hawapo kabisa.

Mara ya mwisho lini umesikia mtu anadai yeye ni extovert? Hawapo. Sasa it's more of a trend.
Kabisa mkuu yana wanajifanya kama special fulani hivi, watu introvert wa ukweli ata hawez kujisema, Sema mbaali na hayo huyu wangu mimi anajeuri
 
Haiingii akilini unakaa na mtu anajifanya haongei, akijibu swali maneno machache kanyamaza, unaongea na mtu mambo ya msingi haongei, hii ni jeuri na kiburi hakuna kitu kingine, msijifiche kwenye muamvuli wa sijui introvert na nini nini, muache kiburi.
Tatizo lawama ziko pande zote, hata mtu msemaji sana kama Kiranga naye anaweza kushambuliwa kwa kiburi kwamba ni narcissist mjuaji wa kila kitu, anataka kuongea kila mara.

Kumbe ni mtu anayependa kubadilishana mawazo na wengine sana, na ana ji expose sana kwa kuongea sana na hivyo si mtu mwenye kiburi na kujiona.

Ukiwa mkimya sana --> Unajiona sana, ndiyo maana unaona watu wengine kama takataka, hutaki kusema nao.

Ukiongea kwa kiasi --> Una mapozi sana. Kuna sehemu nyingine hushirikiani na watu, unachagua sana watu wa kushirikiana nao na sehemu ya kushirikiana nao.

Ukiongea sana --> Unajiona mjuaji sana kila sehemu unataka kuongea wewe.

Huwezi kukosa lawama.

Kwa hiyo wewe kuwa unavyotaka kuwa, usiogope lawama.

Kwa sababu utakavyofanya vyovyote utalaumiwa tu, bora ulaumiwe kwa kufanya unachotaka kufanya kuliko kutaka kuwaridhisha watu halafu ukalaumiwa vile vile tu.
 
Mimi nafikiri kuna watu hua hawajiamini so mda wote wanatafuta approval ya society inayowazunguka. Sasa pale wanapokutana na wewe upo busy na mambo yako, ndio wanaanza kukuona unaringa, au sijui huchangamani.

Mfano mimi jana jioni nilikua nimekaa sehemu napata dinner huku nikifuatilia taarifa ya habari kwenye tv iliyokua kule mbele. Kama meza tatu kutoka nilipo kukawa kuna jamaa nae anaangalia hiyo hiyo habari. Sasa jamaa kila habari inayosomwa yeye anaanza kuniongelesha mimi kuhusiana na hiyo habari tena kwa kupayuka. "Aisee.... sasa hii itakuaje..? We unaona hili linawezekana? Hawa jamaa wanafanya ujinga kabisa..." Mara... "Aloo huyu mama kwakweli mi nimemkubali sana kwa hii hotuba... unajua kwenye hili swala la kukutana na upinzani......" Kidogo.... "Hawa Yanga wasipoangalia mi nakuhakikishia haki ya Mungu hata hiyo nafasi ya tatu wanaikosa...! Unajua hawa Yanga mechi walizobakiza......." "We unaona watachomoa pale..? Eeh? Hawachomoii.... tupinge!!"

Mimi kimyaa... nikawa naendelea kufuatilia habari kama simsikii vile.
Sema kwenye yanga hapo hajadanganya
 
Binafsi nainjoi sana kukaa ndani kwangu weekend au nikitoka kazini, pia nafurahi sana kuchati kwa simu na sio ana kwa ana yan kwa kuchat nachangamka sana ila uso kwa uso maneno hayanitoki kabisa.

Nafsi yangu haitulii napokuwa na watu wengi hasa ambao sijawazoea yani sina amani moyoni kabisa, siwez kuongea lolote mbele ya kundi la watu yan ukitaka kunifanya nizimie ni pale ukinitaja jina niseme kitu mbele za watu hata iwe ni kunisifia yan sipendi kusifiwa kitu mbele za watu.

Halii hii siipendi kwa kweli maana imefikia sehem naulizwa maswali ya ajabu kweli, nikisema nianze program za kuchangamka na kujichanganya na watu najikuta nafanya kwa siku mbili tu nakwama kuna muda najiskia nimechoka sana pale mtu anaponisemesha na mara nyingi kushindwa kujibu kabisa, lakini kwenye kuchat kwa simu sms bila kuongea niko vizur yan sichoki.

Hii hali siipendi na inaniharibia baadhi ya vitu.
 
Haiingii akilini unakaa na mtu anajifanya haongei, akijibu swali maneno machache kanyamaza, unaongea na mtu mambo ya msingi haongei, hii ni jeuri na kiburi hakuna kitu kingine, msijifiche kwenye muamvuli wa sijui introvert na nini nini, muache kiburi.
Sawa tutaacha!!
 
Haiingii akilini unakaa na mtu anajifanya haongei, akijibu swali maneno machache kanyamaza, unaongea na mtu mambo ya msingi haongei, hii ni jeuri na kiburi hakuna kitu kingine, msijifiche kwenye muamvuli wa sijui introvert na nini nini, muache kiburi.
Wanajikutaga Sana Hawa watuwatu
 
Raha ya utahira uwe mwehu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] tuvumiliane tuuuu Kama tunavyo wavumilia na makelele yenu
 
Back
Top Bottom