Kwa wengine hawawezi kuelewa ila huwa kuna wakati mtu unatamani uwe mcheshi pia, uwe free kuongea popote hasa kwenye watu n.k ila shida ni kwamba unajikuta huwezi unajaribu ndio ila unaishia salamu na story kidoogo na kwa ufupi sana.
Wakiongezeka tu watu unajikuta unakaa kimya unabaki kusikiliza.
Mfano kama mimi naweza jichanganya kwa watu ila sasa kuchangia zile mada ndio shida.
Utaongea kidoogo muda mwingi uko kimya.
Mimi ni mtu ambae kama siko kazini basi nipo home naangalia muvi,nasoma vitabu, nafuatilia documentaries n.k
So unajikuta ni either ukomae nao mwisho wakuone unawachora maana huchangii lolote kila siku au uwaboe na story za muvi kila siku.
Either way watakuona ni huchangamani nao tu.
Hata mapumziko huwa nawaza kwenda mbugani huko najisikia amani sana mazingira ya vile.
Huwa tunaongea sana na tuna utani wa kutosha tu lakini kwa watu wachache sanaa tuliowazoea and trust me napata shida mno kumzoea mtu kiasi cha kuwa free around them.
Kwa ufupi niseme tu we were created hivyo tulivyo and we have big heart na ni viumbe fulani tuko very real, ni vile tu jamii inashindwa kutuelewa.