Hakuna hata Jimbo moja lenye maendeleo, labda liwe na katiba yake na sera yake zake, ila sio kwa sera hizi. Wajinga tunahadaiwa sana

Mbona marekani IPO sawa je Unaona ni sahihi kuchukua mapato ya Kahama na shinyanga kutoka katika madini Ila wananchi wanabaki wanakunywa Maji ya na mifugo?
Usitazame maji na mafigo tu tazama na namna sekta ya afya inavyoboreshwa nchi nzima kwa pesa za madini za kanda ya ziwa.

Tazama namna kodi inavyotumika kujenga viwanja vya ndege nchi nzima.

Tazama namna SGR inavyokatiza kwa pesa ya kodi katika mikoa yenye rasilimali na isiyo na rasilimali.

Marekani ipo kama ilivyo kwa sababu za kihistoria, kumbuka hao hao viongozi waanzilishi wa USA walilazimika kununua ardhi kadri miaka ilivyokuwa ikipita ndipo wakaweza kuwa na taifa kubwa kwa sasa. Pia walifanya unyama wa kuuwa wenyeji waliozimiliki hizo ardhi.
 
Utalii unaongoza kwa kuleta mapato mpaka muda huu, huwezi kusikia pesa ya utalii inatajirisha mikoa ya Arusha na Kilimanjaro pekee.

Kuna mikoa haina rasilimali, ina maana isifaidike na utajiri wa nchi kwa sababu ya jiografia kutoipendelea?.
Natia neno hapa,kwa maoni yangu si majimbo tu ikiwezekana kila mkoa ule utumbo wake.
Mfano ,wa arusha kilimanjaro wajenge mkoa wao kwa kile wanachopata ktk utalii

Tanga nawao kodi watakazo kua wanakusanya ktk machungwa,mahind pia Na migodi yao waboreshe kwao

Moro goro pia mchele,migodi
Mtwara ufuta,korosho
Geita dhahabu Na mikoa mingine pia

Kazi ya serikali sasa iwe nikusimamia yale yoote yanayofanyika kweli iwe ni mlezi wakila kitu.
 
Ukiruhusu kila jimbo lijitegemee umeivunja mazima Tanzania. Pia haitaishi kwenye kurahisisha upatikanaji wa mapato itakwenda mbali na kuvunja umoja wa kitaifa.

Tutaanza kutazama na kujitambulisha kwa kanda tunazotoka badala ya utanzania wetu.

Kodi inayokusanywa hivi sasa inasomesha watoto wa kitanzania pale UDOM haijalishi wanatokea Iringa, Mtwara, Singida au Kasulu.

Kodi inayokusanywa muda huu inahudumia sekta nzima ya afya, bima zinazogharamia matibabu zinatibu watu wa Tandahimba, Newala, Rufiji na Mwanza vijijini bila kubagua.
 
Mkuu umezaliwa mwaka gani?
 
Mcheck Lucas Mwashambaa atakuonyesha,huku akibubujikwa machozi
 
Kuna kajimbo kamoja kule South Africa kanaitwa ""Orania"'. Wao wamea mua kujitenga na kuanza serikali yao wenyewe ya kizungu na hawamtaki mtu mweusi kwenye jimbo lao. Ukiangalia kanajiendesha vizuri tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…