Hakuna jambo nzuri kama kuwa huru, usikubali kuwa Mbuzi wa kafara

Hakuna jambo nzuri kama kuwa huru, usikubali kuwa Mbuzi wa kafara

What is Uhuru? Baba yako akikutuma Ikakataa huo utaita Uhuru? Rais wako ukimtukana huo itaitwa Uhuru? Kila kitu kina mpaka, Uhuru una Mipaka mingo zaidi kwa sababu Uhuru duniani ni zero sum game, yaani Uhuru wako maana yake si Uhuru kwa mwingine. Uhuru wa France kutajirika na Umeme wa nuclear toka Burkina Faso ni upungufi ihuti kwa Burkina Faso. Uhuru wa kumtukana Rais ni kukosa Uhuru yeye Rais. See what I mean?
 
Ama kiumane wafe wengi ili ukombozi upatikane au watu wote watulie ili umasikini na unyonyaji uendelee.

Kuwa vuguvugu ndo anapotea mmoja mmoja, mwisho wa siku wanapotea wote halafu hamna kilichofanyika zaidi ya kuacha familia ikikulilia.

Mtoa mada nakuelewa sawa.
Kuna watu wanategemewa na wanatokea familia masikini; hufanya kuwaiga wengine kushupaza shingo na kujifanya hero, kumbe walioigwa wanafanya vile kimkakati na kimaelekezo ya kisiasa. Mwisho wa siku muigaji anapotea kwa kukosa msaada.

Kama huna wa kukupigania ni heri ukabaki tu.
 
Unafikiri uko salama , watu hawafanani nchi ikioza kila mtu ameoza , embu fikiria unacheza salama hutaki kujihusisha na siasa alafu unasikia mwanao wa kumzaa amefuatwa kwake amechukiliwa na watu wasiojulikana, dada amefilwa kwa sababu ameenda kusikiliza kesi ya rafiki yake mwanasiasa au baba ako amekutwa amekufa ametupwa porini kwa sababu ni mwanachama wa chama fulani au kanisa unalosali limefungiwa kwa sababu mchngaji wenu anakosoa serikali … kumbuka umecheza salama lakini yote haya yamekukuta …UNACHUKUA HATUA GANI?
 
hayamaanishi ccm wakitoka ndo maisha yamefika paradiso, mapungufu yapo lakini ya kimaisha, wakina trump wanachapwa mpaka sniper tunaelewa tu
Sio kwamba watu wanachukia ccm Bali Watu wanataka Ile freedom ya kuweka Leo chadema, kesho ACT, kesho kutwa ccm, hii italeta hamasa Kwa chama kinachokuwa madarakan kufanya kweli ili kibaki ktk Dora, kuliko kuwa na chama kimoja ambacho hata kikiaribu wanajua kesho watarudi hii ndio haifai.
 
Siasa Ni maisha. Ushiriki usishiriki itakuathiri one way or another. Tushiriki kikamilifu ili Kujenga jamii iliyo bora. Unaweza kushiriki kwa kuchagua viongozi au kuchaguliwa kama kiongozi. Uchaguzi ndio unaoamua hatima ya maisha tunayoishi kama taifa. Viongozi Bora huletwa na wachaguzi makini. Kuogopa siasa Ni uoga usiokuwa na Msingi unaotokana na dhana dhanifu na dhaifu kuwa siasa Ni machafuko. Siasa sio mbaya. Dunia yote inatumia siasa katika kuweka nchi/taifa kwenye uthabiti.
Pia, dhana kuwa kama huwezi kuchangiwa na nduguzo usishiriki siasa, Ni dhana potofu. Huwenda ushiriki wenu ukaleta nafuu na wakapatikana ndugu wenye kipato kwenye familia yenu kufuatia sera za kiuchumi zotokanazo na chama unachishiriki kukiweka madarakani.
Think again.

Shiriki kikamilifu Kujenga taifa, shiriki kwenye siasa. Jitokeze kugombea, kusikiliza sera za wagombea, na mchague au chaguliwa kiongozi ulete maendeleo kwa ndugu zako na taifa kwa jumla.
 
Ama kiumane wafe wengi ili ukombozi upatikane au watu wote watulie ili umasikini na unyonyaji uendelee.

Kuwa vuguvugu ndo anapotea mmoja mmoja, mwisho wa siku wanapotea wote halafu hamna kilichofanyika zaidi ya kuacha familia ikikulilia.

Mtoa mada nakuelewa sawa.
Kuna watu wanategemewa na wanatokea familia masikini; hufanya kuwaiga wengine kushupaza shingo na kujifanya hero, kumbe walioigwa wanafanya vile kimkakati na kimaelekezo ya kisiasa. Mwisho wa siku muigaji anapotea kwa kukosa msaada.

Kama huna wa kukupigania ni heri ukabaki tu.
Ahsante Kwa kunielewa

Lissu yupo mahabusu,lakini nina uhakika familia yake iko vizuri

Mbowe aliwahi kukaa mahabusu,
Nina Imani familia yake haikutetereka

Gwajima kajificha lakini I hope family itakuwa sawa tu.

Swala lipo kwa wenzangu na Mimi ambao kukaa mahabusu halafu ukaambiwa dhamana ni laki tano unaweza fia hukohuko
 
Sio kwamba watu wanachukia ccm Bali Watu wanataka Ile freedom ya kuweka Leo chadema, kesho ACT, kesho kutwa ccm, hii italeta hamasa Kwa chama kinachokuwa madarakan kufanya kweli ili kibaki ktk Dora, kuliko kuwa na chama kimoja ambacho hata kikiaribu wanajua kesho watarudi hii ndio haifai.
Dora ni nini
Mbona kama wewe ni mweupe
 
Salaam jamiiAfrica.

Unataka kuwa huru?

Unataka kuwa na Amani?

Unataka watoto wako uwalee na wafurahie uwepo wako?

Unataka kufaidi mema ya Dunia,japo asilimia 0.01?

Jitenge na siasa,kaa mbali na wanasiasa.

Acha kuiongelea siasa.

Kaa kimya fanya mambo yako ,usifanye vitu Kwa kutafuta sifa,

Wewe siyo
Nelson Mandela,
Kwame Nkrumah,
John Okello,
Che Guevara,

Wewe ni mtoto wa masikini, wazazi wako wanakutegemea,na wanahitaji msaada wako pengine.

Kama familia yako hata ikiungana haina uwezo wa kuchanga pesa inafika milioni 5, bro/sister achana na siasa.

Ni rahisi watu kukusifia na kukuona Shujaa lakini ni ngumu wao kujitokeza wakawa na misimamo kama yako,

Ni rahisi mno watu kukupigia makofi na kukupa michango ya bukubuku na kukutanguliza front huku wakikuita mwamba , Shujaa,mwanaharakati na majina mengi ya kinafiki ,na wewe ulivyo na kichwa maji unajiona Samora Machel.

Wakuu pambaneni na maisha,
Sote tunajua,vitu na miundimbinu mingi ni dhaifu,bidhaa na materials bei ghali,Ajira hazitoshi pamoja na mengi lakini tunakaa kimya Kwa hatima ya vizazi vyetu

Asalaam Aleykum jamiiy'aa
Siasa ndio inaongoza kila kitu. Kujitenga na siasa ni sawa na kuwa mtumwa kwenye nchi yako. Siasa inaajiri, inajenga shule, hospital,barabara, inaleta maji na umeme, siasa inasimamia bei ya mazao. Mtu mjinga tena mjinga sana ambaye anaweza kujitenga na siasa.
 
Ahsante Kwa kunielewa

Lissu yupo mahabusu,lakini nina uhakika familia yake iko vizuri

Mbowe aliwahi kukaa mahabusu,
Nina Imani familia yake haikutetereka

Gwajima kajificha lakini I hope family itakuwa sawa tu.

Swala lipo kwa wenzangu na Mimi ambao kukaa mahabusu halafu ukaambiwa dhamana ni laki tano unaweza fia hukohuko
Hakuna dhahabu bila kupita kwenye moto.
Kuna muda lazima uumie kidogo ili uweze kupata maisha huru.

Kizazi kisichowajibika kinazaa mashoga, malaya na machawa
 
Kama sio mwanasiasa achana na siasa ila kama ni mwanasiasa basi farakana na siasa ila kama maovu yamejitokeza kemea
 
Salaam jamiiAfrica.

Unataka kuwa huru?

Unataka kuwa na Amani?

Unataka watoto wako uwalee na wafurahie uwepo wako?

Unataka kufaidi mema ya Dunia,japo asilimia 0.01?

Jitenge na siasa,kaa mbali na wanasiasa.

Acha kuiongelea siasa.

Kaa kimya fanya mambo yako ,usifanye vitu Kwa kutafuta sifa,

Wewe siyo
Nelson Mandela,
Kwame Nkrumah,
John Okello,
Che Guevara,

Wewe ni mtoto wa masikini, wazazi wako wanakutegemea,na wanahitaji msaada wako pengine.

Kama familia yako hata ikiungana haina uwezo wa kuchanga pesa inafika milioni 5, bro/sister achana na siasa.

Ni rahisi watu kukusifia na kukuona Shujaa lakini ni ngumu wao kujitokeza wakawa na misimamo kama yako,

Ni rahisi mno watu kukupigia makofi na kukupa michango ya bukubuku na kukutanguliza front huku wakikuita mwamba , Shujaa,mwanaharakati na majina mengi ya kinafiki ,na wewe ulivyo na kichwa maji unajiona Samora Machel.

Wakuu pambaneni na maisha,
Sote tunajua,vitu na miundimbinu mingi ni dhaifu,bidhaa na materials bei ghali,Ajira hazitoshi pamoja na mengi lakini tunakaa kimya Kwa hatima ya vizazi vyetu.

Asalaam Aleykum jamiiy'aa
dah unafundisha watu uoga na umaskini pole sana
 
Uko Sawa kabisa huwezi kupigania watu wasiojitambua
 
Ushauri mzuri coz wajuvi wa mambo walisha sema ni mchezo mchafu Kuna chuki,visasi na mbaya zaidi kwenye ulimwengu huu nchi yoyote ile yenye serikali hakunaga demokrasia .

Lkn pia Kila mtu yupo duniani kwa kusudi maalumu wengine wapo kutuburudisha mfano wasanii, wengine kutetea ndo Hawa wanaharakati,wengine kutulinda nk. Ili kusudi la Mungu litimie
 
Ahsante Kwa kunielewa

Lissu yupo mahabusu,lakini nina uhakika familia yake iko vizuri

Mbowe aliwahi kukaa mahabusu,
Nina Imani familia yake haikutetereka

Gwajima kajificha lakini I hope family itakuwa sawa tu.

Swala lipo kwa wenzangu na Mimi ambao kukaa mahabusu halafu ukaambiwa dhamana ni laki tano unaweza fia hukohuko
Mwanasiasa yupo kwaajili ya maslahi yake binafsi na ya familia yake.
Haiwezekani kutenganisha siasa na ubinafsi.

Hata leo chama cha upinzani kikichukua nchi hakuna mabadiliko yatakayofanyika.
 
Mi nadhani kikubwa ni kufanya siasa za kiistaarabu,kuacha matukano,kubishana kwa hoja na sio kudhalilisha watu na kutoa shutuma zisizo za kweli,
Unaweza kumtukana mtu,ukashughulikiwa na chawa wake hata bila ya yeye kujua,siasa ni mchezo wa hatari mno,ukitaka kufanya siasa za shari,jipange kwa lolote
 
Back
Top Bottom