Utawasikia kwenye mialiko yao redioni, kwenye TV na vipeperushi watangaza mialiko uende kwenye makusanyiko yao wanasema hakuna kiingilio, kiingilio ni bure! Ukifika huko unahubiriwa habari za kutoa sadaka na madhara utakayopata kama hutoi! Unachotoa kinaingia kwenye mfuko wa mhubiri na mke/mume wake. Hivi taifa langu Tanzania nani amewaloga kuingia kwenye ujinga wa wa kuwaamini hawa matapeli? Tuwafundishe kiasi gani mpate kuelewa???