- Thread starter
- #41
Si lazima ila kutoa sqhihi kuna faida zake. Rekebisha mawazo yako. SI LAZIMA!Kutoa ni lazima Ila utoe sehemu sahihi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Si lazima ila kutoa sqhihi kuna faida zake. Rekebisha mawazo yako. SI LAZIMA!Kutoa ni lazima Ila utoe sehemu sahihi
NENO? Mbona huyo mhubiri hakutajirika kwa kusikiliza NENO?? Yeye anakupa maneno halafu anataka pesa yako!!kwamba wana lazimishwa kutoa
wao wana pewa neno na faida/hasara za kutoa sadaka wanatoa kwa mapenzi yao shida iko wapi
Kama unataka kufuata maandiko peleka fungu la kumi Yerusalemu hekaluni. Kinyume na hapo umejitungia mafundisho yako mwenyewe kwamba kanisa ndio mbadala wa hekalu ambapo Mungu aliagiza sadaka zipelekwe. Wayahudi wenyewe waliopewa hilo agizo hawakupeleka fungu la kumi wala sadaka hata kwenye sinagogi ambayo wanatheolojia uchwara wanalifananisha na makanisa ya leo. Upumbavu tu na umbumbumbu wa kutokuijua imani ya kikristo na misingi yake. Wakimbieni matapeli.Msingi wa Imani yoyote ni sadaka hata kama unaamini kwenye Mungu wa bahari unaweza ukatupa hata mbuzi baharini kama sadaka. Kikubwa sadaka itoke kwa mujibu wa maandiko ya Imani yako inavuotaka.
Tatizo tu waumini mnawaonea wivu viongozi wenu wa dini wakizitumia sadaka zenu, mtu anahudumia kanisa la watu 1000 kati Yao Kuna matajiri kama 50 hivi ambao wakitoa fungu la 10 tu (ambayo ni sadaka halali) zinapatikana zaidi ya 100m na ukiunganisha na za waumini wa kawaida plus sadaka za kawaida za jumapili na kongamano unakuta makusanyo ya kutosha ambapo zinatumika kwa maendeleo ya kanisa ikiwemo kumhudumia mchungaji na wengine wanaohudumia kanisa. Mchungaji akinununuliwa Land cruiser kwa hela ya kanisa ili awafikie waumini wake mnaleta nongwa wakati kanisa lina uwezo wa kumhudumia (nazungumzia kwa wale tu wanaotoa sadaka bila kulazimishwa na kutishwa bali kama maandiko yanavyotaka hivyo mtu akiwa na waumini wengi automatimatically hata mchungaji atahifumiwa vizuri)
N:B. Nimeandika sina maslahi yoyote na hapa nilipo sijawahi enda kusali mwaka wa tatu labda kama nitahidhuria msiba automatically unadhiriki Ibadan kwa kuwa ni shughuli ya jamii. TOENI SADAKA KAMA MAANDIKO YANAVYOTAKA, SIO UNAKUNJA MILIONI 2 KWA MWEZI ALAFU KANISANI UNAPELEKA BUKU 2 KILA J'PILI NA FUNGU LA KUMI UNATOA ELFU 50 )
kaamua kutajirika kwa kutoa neno shida iko wapiNENO? Mbona huyo mhubiri hakutajirika kwa kusikiliza NENO?? Yeye anakupa maneno halafu anataka pesa yako!!
Mbinguni kuna njaa?? Mbona hata hilo Agano jipya linasema wazi miili ya kule ni tofauti? Hazina inayoongelewa ni lugha ya picha. Maandiko mengi ukitasoma kwenye lugha mama za biblia ( Kiebrania, Kiaramayo na Kigiriki) utagundua tafsiri za lugha zingine zimechakachuliwa mno na kupoteza maana. Ni kama walivyokosa tafsiri ya Yesu kusema sababu pekee ya kumuacha mke wako ni uzinzi. Walikaa hapo Zanzibar kutafsiri biblia kwa Kiswahili wakakosa neno halisi la UNDUGU WA DAMU wakaweka Uzinzi!!!! Hatari na nusu!Toeni fungu la kutosha, nasikia mwisho wa maisha yako ndio hazina utakayoikuta mbinguni. Kama hukuwa unatoa sadaka account yako mbinguni ni zero, utateseka na njaa huko mbinguni. Ngoja nikuimbie kawimbo "toa ndugu, toa ndugu, ulicho nacho, kwa kuwa bwana anakuona mpaka rohoni" kaeni kwa follen, mtu asibaki kwenye dawati.
Wapenda miujiza na upako, sijui kama watakuelwa.Utawasikia kwenye mialiko yao redioni, kwenye TV na vipeperushi watangaza mialiko uende kwenye makusanyiko yao wanasema hakuna kiingilio, kiingilio ni bure! Ukifika huko unahubiriwa habari za kutoa sadaka na madhara utakayopata kama hutoi! Unachotoa kinaingia kwenye mfuko wa mhubiri na mke/mume wake. Hivi taifa langu Tanzania nani amewaloga kuingia kwenye ujinga wa wa kuwaamini hawa matapeli? Tuwafundishe kiasi gani mpate kuelewa???
Huo ni utapeli. Neno kila mtu anaweza kutoa. Hao ni motivational speakers kwenye kichaka cha dini. Hakuna mtume wala nabii hapo upuuzi mtupukaamua kutajirika kwa kutoa neno shida iko wapi
Kwani wao ni walawi? Mtu ana shamba ekari kumi ni mlawi? Walawi ni wana wa Lawi, moja ya watoto wa Yakobo ambao walipoingingia nchi ya Kanaani Mungu hakuwapa sehemu ya ardhi kama wale kabila zingine 11. Hawa walipewa ukuhani ili wahudumu hekaluni tu kwa hiyo wale kabila zingine waliagizwa kutenga sehemu ya kumi ya mapato yanayotokana na ardhi waliyopewa walete hekaluni ili wana wa Lawi wapate mahitaji yao. Siku hizi matapeli wamejinyakulia maandiko hayo kuwaahadaa wasiojua ili kujinufaisha.Sema Sasa Biblia imeruhusu walawi wale madhabahuni ila Hawa wa makanisa ya Marlboro au maturubali wamezidi aisee. They are purely business people... Na wanatumia maandiko vibaya kujinufaisha...
👇👇👇👇👇👇
1 Wakorintho 9:13-27
1 Wakorintho 9:13-27 BHND
BHNSUVNenoSRUV
Je, hamjui kwamba wanaotumikia hekaluni hupata chakula chao hekaluni, na kwamba wanaotoa sadaka madhabahuni hupata sehemu ya hiyo sadaka? Bwana aliagiza vivyo hivyo; wahubiri wa Habari Njema wapate riziki zao kutokana nayo. Lakini, mimi sikutumia hata mojawapo ya haki hizo. Na wala siandiki nijipatie haki hizo; kwangu mimi ni afadhali kufa kuliko kumfanya yeyote aone kwamba najisifu bure. Ikiwa ninaihubiri injili, hilo si jambo la kujivunia; hilo ni jukumu nililopewa. Na, ole wangu kama sitaihubiri injili! Ningekuwa nimeichagua kazi hii kwa hiari, basi, ningetazamia malipo; lakini maadamu naifanya ikiwa ni wajibu, hiyo ina maana kwamba ni jukumu nililopewa nitekeleze.
WATU WANASHINDWA KUELEWA KUWA TUNAAMBIWA SIKU ZA MWISHO WATATOKEA MANABII WENGI LAKINI WAONGO.
👇👇👇👇👇👇👇
Mathayo 24:4-28 BHN
BHNSUVNenoSRUV
Yesu akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa na mtu. Maana wengi watatokea wakisema kila mmoja kwamba yeye ndiye Kristo nao watawapotosha watu wengi. Mtasikia juu ya vita na fununu za vita; lakini msifadhaike, maana hayo hayana budi kutokea, lakini mwisho wenyewe ungali bado. Taifa moja litapigana na taifa lingine; ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine. Hapa na pale patakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi. Yote hayo ni kama mwanzo wa maumivu ya kujifungua mtoto. “Kisha watawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifa yote yatawachukieni kwa sababu ya jina langu. Tena, wengi wataiacha imani yao, watasalitiana na kuchukiana. Watatokea manabii wengi wa uongo watakaowapotosha watu wengi. Kwa sababu ya ongezeko la uhalifu, upendo wa watu wengi utafifia. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokolewa. Ila, kabla ya mwisho kufika, hii Habari Njema ya ufalme wa Mungu itahubiriwa ulimwenguni kote kama ushuhuda kwa mataifa yote.
Jamii yetu watu wanaupeo mdogo sanaGharama za uendeshaji wa mkutano huo kama watu hawatalipia kwa njia ya sadaka, nani atagharamia?
Katiba ya Tanzania inahimiza uhuru wa kuabuduHuu upuuzi uishe. Tunaangamiza taifa
Yap ndio maana nasema, haya makanisa ya Sasa na watumishi wa Sasa wanatumia Hilo gepu vibaya......Kwani wao ni walawi? Mtu ana shamba ekari kumi ni mlawi? Walawi ni wana wa Lawi, moja ya watoto wa Yakobo ambao walipoingingia nchi ya Kanaani Mungu hakuwapa sehemu ya ardhi kama wale kabila zingine 11. Hawa walipewa ukuhani ili wahudumu hekaluni tu kwa hiyo wale kabila zingine waliagizwa kutenga sehemu ya kumi ya mapato yanayotokana na ardhi waliyopewa walete hekaluni ili wana wa Lawi wapate mahitaji yao. Siku hizi matapeli wamejinyakulia maandiko hayo kuwaahadaa wasiojua ili kujinufaisha.
Hapo ndioi utapeli unapopenyeza. Asilimia tisini ya hao unaowasemea ni matapeli. Mbona nimekupa mfano wa mtume Paulo au hukuelewa? Acheni kuwaibia raia kwa kisingizio cha dini. Yesu mwenyewe kuna wakati alikosa kodi ikabidi Petro akatafute sarafu kwenye tumbo la samaki. Jama ni kukusanya sadaka Yesu ndiye angekuwa na ukwasi wa kutosha maana mafundisho na miujiza yake ilikuwa kabambe siyo haya mazingaombwe ya wahubiri wa leo.Jamii yetu watu wanaupeo mdogo sana
Hawafikiriagi zile gharama za mkutano
Yaani tunawatu wanaopenda vya bure sana na mbaya zaidi anayeongea hivyo ni mwanaume na anafamilia
acha kuwafanya watu misukule kwakujiweka kati, kila mtu ana maumivu ya kutokurizika na maisha yakeToeni fungu la kutosha, nasikia mwisho wa maisha yako ndio hazina utakayoikuta mbinguni. Kama hukuwa unatoa sadaka account yako mbinguni ni zero, utateseka na njaa huko mbinguni. Ngoja nikuimbie kawimbo "toa ndugu, toa ndugu, ulicho nacho, kwa kuwa bwana anakuona mpaka rohoni" kaeni kwa follen, mtu asibaki kwenye dawati.
Hakuna uhuru usiokuwa na mipaka. Kwa hiyo katiba inaniruhusu hata kuchinja watu kutoa kafara kama imani yangu inanitaka kufanya hivyo? What are you taking about? Nikianzisha leo ibada inayowataka waumini kufanya ibada na maandamano mitaani wakiwa uchi wa mnyama katiba bado itaniruhusu kwa sabababu imetoa uhuru wa kuabudu???Katiba ya Tanzania inahimiza uhuru wa kuabudu
Utawasikia kwenye mialiko yao redioni, kwenye TV na vipeperushi watangaza mialiko uende kwenye makusanyiko yao wanasema hakuna kiingilio, kiingilio ni bure! Ukifika huko unahubiriwa habari za kutoa sadaka na madhara utakayopata kama hutoi! Unachotoa kinaingia kwenye mfuko wa mhubiri na mke/mume wake. Hivi taifa langu Tanzania nani amewaloga kuingia kwenye ujinga wa wa kuwaamini hawa matapeli? Tuwafundishe kiasi gani mpate kuelewa???