Utawasikia kwenye mialiko yao redioni, kwenye TV na vipeperushi watangaza mialiko uende kwenye makusanyiko yao wanasema hakuna kiingilio, kiingilio ni bure! Ukifika huko unahubiriwa habari za kutoa sadaka na madhara utakayopata kama hutoi! Unachotoa kinaingia kwenye mfuko wa mhubiri na mke/mume wake. Hivi taifa langu Tanzania nani amewaloga kuingia kwenye ujinga wa wa kuwaamini hawa matapeli? Tuwafundishe kiasi gani mpate kuelewa???
Mwaka 2017 nikiwa Nzuguni dodoma walipita mabinti2 na kijana mmoja wanagawa vipeperushi kuwa watakuwa na mkutano jpili ijayo. Walikuwa wanaenda nyumba kwa nyumba wanakualika then wanaacha vipeperushi vikitoa ratiba kamili kwaya zitakazo kuwepo pamoja na muhibiri ayenadiwa kuwa katoka ughaibuni huko.
Kipeperushi kile kilikuwa kinasema usafiri ni bure na chakula ni bure na kama haitoshi punde unapopanda kwenye gari lao unapewa 10k cash! Niliwaza sana bila kupata majibu nini maana ya hela hii halafu na chakula bure?
Basi siku ikafika wale mabinti wakapita tena mapema saa2 wanawakumbusha na kuwaambia magari yapo tiyari na yamefungwa mabango ya vitambaa. Nikasema wacha leo nami niende nikajionee hasa ile teni ya bure iwapo wasipo nipa nitarudia hapohapo stend nilioga nikavaa kisabato na saspenda zangu huyoo kituoni mkutano ulikuwa unafanyika mtaa jirani jina nimesahau unapita unakata kona pale ilipo shule ya martin luther inakuwa mkono wa kushoto unanyooka na barabara hiyo nayo ni lami pia.
Kweli nilipofika tu nikakuta wadada wengine wakaniribisha vizuri huku mmoja akinipa ile hela 10k mpyaa kabisa nikaichungulia kama ni og ama fake hadi wakacheka. Nikaitunza basi mimi sikuwa wa kwanza au wapili kwa muda ule na gari kama dk 8 ikajaa ikatupeleka mkishuka tu hivi chai ya maana.
Baadae kwaya zikaimba na nyimbo zikaibwa mahubiri ya kaanza hatimae wakuombewa wakaombewa.
ibada ikaisha tukarudi. Ukumbuke walikuwa wamechukua no za simu. na majina yetu mida ya saa1-2 nikapigiwa na mrembo mmoja sauti tamu kama ya watoa huduma wa voda.Nikaulizwa ibada yetu uliionaje uliopendezwa na kipi na ulikerwa na kipi? Nikasifia tukaongea hadi tukatoka kwenye maada ya mkutano tukaanza ulizana makazi yetu ya kudumu ni wapi then tukaagana.
Simu ziliendelea kupigwa kama kawaida na siku ya jmos ijayo walikuja tena vilevile wakihamasisha usafiri upo na chakula kipo na pesa mkononi ipo pia.
Kesho yake jpili nilienda tena kama kawaida sema yule mhubiri wao hakuwepo ila hela na vingine vilikuwepo kama kawaida. hadi nikatoka sikuwahi pata jibu kwanini walikuwa wanafanya hivi? sadaka nilitoa buku1 tu kila ibada ila muhamasishaji alikuwa anasema kadiri unavyotoa sadaka kubwa mungu anazidi kukubariki mara dufu. Kwangu mimi wala sikutishika.
Huwa najiuliza lengo la kanisa hili ilikuwa ni nini? makadirio kwa watu wale kama wote walipeqwa hela muhimu m7 ilisha ama zaidi hapo ni jpili moja tu achana na usafiri na chakula