Hakuna Kiingilio!! Kichekesho na utapeli wa mialiko ya mikutano ya injili

Hakuna Kiingilio!! Kichekesho na utapeli wa mialiko ya mikutano ya injili

Sasa hivi ni biashara ndiyo maana inahubiriwa kutoa sadaka. Yani si lutheran, si roman wala sijui agt kote wanahubiri sadaka tu na vitisho vya kutotoa sadaka kila siku.
Ni biashara kama biashara nyingine kwa sasa.
Kwa muono wangu kama serikali haitatupia macho suala hili taifa litaendelea kuangamia. Kila siku kuna nabii feki anaibuka. Hii si afya njema kwa taifa.
 
Utawasikia kwenye mialiko yao redioni, kwenye TV na vipeperushi watangaza mialiko uende kwenye makusanyiko yao wanasema hakuna kiingilio, kiingilio ni bure! Ukifika huko unahubiriwa habari za kutoa sadaka na madhara utakayopata kama hutoi! Unachotoa kinaingia kwenye mfuko wa mhubiri na mke/mume wake. Hivi taifa langu Tanzania nani amewaloga kuingia kwenye ujinga wa wa kuwaamini hawa matapeli? Tuwafundishe kiasi gani mpate kuelewa???
Mkuu, niliposikia kuwa nchi za kikomunisti hawataki kusikia neno dini nilikuwa nawaona wajinga sana. Lakini kinachoendelea Tanzania sasa hivi kimenifanya nibadili mawazo yangu. Halafu hayo mahubiri yenyewe: ajali nyingi za barabarani mwisho wa mwaka zinasababishwa na ''roho wachafu''. Bia kusahau hao wote wanaokusanyika kwenye hiyo mikesha wamekwenda pale ili shida zao zitatuliwe. i.e. kosefu wa ajira, magonjwa, kutopata wenza wa ndoa, uchumi mbaya..... Na CCM imeona ndiyo sehemu ya kuokota mijitu mijinga, inayodhani shida zao zainaletwa na mapepo.
 
Msingi wa Imani yoyote ni sadaka hata kama unaamini kwenye Mungu wa bahari unaweza ukatupa hata mbuzi baharini kama sadaka. Kikubwa sadaka itoke kwa mujibu wa maandiko ya Imani yako inavuotaka.

Tatizo tu waumini mnawaonea wivu viongozi wenu wa dini wakizitumia sadaka zenu, mtu anahudumia kanisa la watu 1000 kati Yao Kuna matajiri kama 50 hivi ambao wakitoa fungu la 10 tu (ambayo ni sadaka halali) zinapatikana zaidi ya 100m na ukiunganisha na za waumini wa kawaida plus sadaka za kawaida za jumapili na kongamano unakuta makusanyo ya kutosha ambapo zinatumika kwa maendeleo ya kanisa ikiwemo kumhudumia mchungaji na wengine wanaohudumia kanisa. Mchungaji akinununuliwa Land cruiser kwa hela ya kanisa ili awafikie waumini wake mnaleta nongwa wakati kanisa lina uwezo wa kumhudumia (nazungumzia kwa wale tu wanaotoa sadaka bila kulazimishwa na kutishwa bali kama maandiko yanavyotaka hivyo mtu akiwa na waumini wengi automatimatically hata mchungaji atahifumiwa vizuri)

N:B. Nimeandika sina maslahi yoyote na hapa nilipo sijawahi enda kusali mwaka wa tatu labda kama nitahidhuria msiba automatically unadhiriki Ibadan kwa kuwa ni shughuli ya jamii. TOENI SADAKA KAMA MAANDIKO YANAVYOTAKA, SIO UNAKUNJA MILIONI 2 KWA MWEZI ALAFU KANISANI UNAPELEKA BUKU 2 KILA J'PILI NA FUNGU LA KUMI UNATOA ELFU 50 )
 
Wanatishwa na vifungu vya maandiko ya biblia ambavyo aghalabu they are translalated out of context or they have have nothing to do with our modern society. Mtu anajiita mkristo muulize akutajie hata vitabu kumi tu vilivyo kwenye Biblia hawezi. Anaenda huko makanisani anasomewa mistari halafu mhubiri anaikunjakunja ili akukamate utoe hela.
hapo tatizo n muhubiri ama ni mfuasi
wewe mbona ujapigwa hela
kwa sababu una uelewa hao wasio na uelewa wacha wagharamie upumbavu wao
 
Taifa litapata uponyaji dini zikifutwa kwani huyu ni adui mpya mwenye nguvu aliyeongezeka kwenye maadui wa Mwl.Nyerere.Mungu kama intimidator(muogopeshaji) amewafanya mawakala wake waupige mwingi kwani watu wanahofu ya mungu.Na ukichunguza kwa makini utagundua kuwa serikali ipo nyuma yao kwa kificho ili kurahisisha kuwatawala watu.Ukombozi utatokana na wewe uliyejitambua.
 
Hivi hamjaona jengo lililoandikwa : Jumba la Ufalme la Mashahidi wa Yehova?
Nendeni hapo mambo ya sadaka na kuomba omba pesa hayapo.
Kwa kweli hawa nawasifu japo Theology yao bado nina shida nayo kwenye vipengelele vichache. Wao wana sanduku mahali ukitaka kuweka chochote tumbukiza humo. Husikii kabisa mambo ya pesa sijui sadaka yakiongelewa. Big up Mashahidi wa Yehova kwa hili.
 
wananchi wanalazimishwa kutoa hizo sadaka mkuu
Tusipotibu huu ugonjwa tutaliangamiza taifa. Sasa hivi kuna watu hawafanyi kazi wanasubiri miujiza. Usiku kucha kubwabwaja sala ndeeeeefuu ambazo ni machukizo tu mbele za Mungu.
 
Kwani umelazimishwa?
Mbona wanaotapeliwa kwenye utapeli mwingine pia hawalazimishwi lakini serikali inawatia adabu hao matapeli? Unaongea kwa akili timamu au? Kwa hiyo kama hukulazimishwa basi tapeli hana hatia?? Are you serious??
 
Kwani umelazimishwa?
Ukifanya mapenzi na msichana mwanafunzi wa shule ya msingi hata kama hukumlazimisha utapata mvua 30 gerezani. The same applies here acheni kutetea uovu.
 
Kutoa ni lazima Ila utoe sehemu sahihi
Dini iliyo safi ni kuwasaidia yatima, wajane na wote wenye uhitaji na kujiweka mbali na dhambi. Hayo ya kutoa pesa makanisani wala hata kwenye biblia ya kikristo ( Agano Jipya ) hayapo. Mtume Paulo aligiza tu kutoa mchango mara moja kwa mwezi kuwasaidia waumini masikini waliokuwa kule Yerusalemu. Wala hakuna mahali popote Agano Jipya utakuta mambo ya fungu la kumi(zaka). Hilo lilipaswa kupelekwa hekaluni na baada ya jemadari Tito kuliharibu hekalu mwaka 70CE mambo hayo hayakuwepo tena. Siku hizi utawasikua hawa matapeli wanaita pale wanapohubiria upuuzi wao eti ni "madhabahu". Madhabahu ni mahali pa kutolea sadaka za kuteketeza. Sasa unaambiwa upeleke hapo pesa zako! Ni vichekesho kwa kweli.
 
Gharama zao atagharamia Mungu,au wafanye kama wametoa sadaka tu,

Wao si wanawaombea waumini wao kwa Mungu ili wafanikiwe? kwanini hao wachungaji nao wasisubiri kufanikiwa kupitia Mungu huyo huyo badala ya kuwakamua waumini ambao wengi wao ni masikini?
Wanajua ni usanii tu maana hakuna kati ya hao wahubiri alikuwa milionea kwa kusikiliza huu ujinga wanaouhubiri
 
Mkuu, niliposikia kuwa nchi za kikomunisti hawataki kusikia neno dini nilikuwa nawaona wajinga sana. Lakini kinachoendelea Tanzania sasa hivi kimenifanya nibadili mawazo yangu. Halafu hayo mahubiri yenyewe: ajali nyingi za barabarani mwisho wa mwaka zinasababishwa na ''roho wachafu''. Bia kusahau hao wote wanaokusanyika kwenye hiyo mikesha wamekwenda pale ili shida zao zitatuliwe. i.e. kosefu wa ajira, magonjwa, kutopata wenza wa ndoa, uchumi mbaya..... Na CCM imeona ndiyo sehemu ya kuokota mijitu mijinga, inayodhani shida zao zainaletwa na mapepo.
Naona aheri Ukomunisti kuliko huu upumbavu unaoendelea kwetu
 
Msingi wa Imani yoyote ni sadaka hata kama unaamini kwenye Mungu wa bahari unaweza ukatupa hata mbuzi baharini kama sadaka. Kikubwa sadaka itoke kwa mujibu wa maandiko ya Imani yako inavuotaka.

Tatizo tu waumini mnawaonea wivu viongozi wenu wa dini wakizitumia sadaka zenu, mtu anahudumia kanisa la watu 1000 kati Yao Kuna matajiri kama 50 hivi ambao wakitoa fungu la 10 tu (ambayo ni sadaka halali) zinapatikana zaidi ya 100m na ukiunganisha na za waumini wa kawaida plus sadaka za kawaida za jumapili na kongamano unakuta makusanyo ya kutosha ambapo zinatumika kwa maendeleo ya kanisa ikiwemo kumhudumia mchungaji na wengine wanaohudumia kanisa. Mchungaji akinununuliwa Land cruiser kwa hela ya kanisa ili awafikie waumini wake mnaleta nongwa wakati kanisa lina uwezo wa kumhudumia (nazungumzia kwa wale tu wanaotoa sadaka bila kulazimishwa na kutishwa bali kama maandiko yanavyotaka hivyo mtu akiwa na waumini wengi automatimatically hata mchungaji atahifumiwa vizuri)

N:B. Nimeandika sina maslahi yoyote na hapa nilipo sijawahi enda kusali mwaka wa tatu labda kama nitahidhuria msiba automatically unadhiriki Ibadan kwa kuwa ni shughuli ya jamii. TOENI SADAKA KAMA MAANDIKO YANAVYOTAKA, SIO UNAKUNJA MILIONI 2 KWA MWEZI ALAFU KANISANI UNAPELEKA BUKU 2 KILA J'PILI NA FUNGU LA KUMI UNATOA ELFU 50 )
Kwa mujibu wa maandiko gani ndugu? Ya kikristo au ya Kiyahudi? Usichanganye mafaili.
 
Back
Top Bottom