Hakuna Kiingilio!! Kichekesho na utapeli wa mialiko ya mikutano ya injili

Toeni fungu la kutosha, nasikia mwisho wa maisha yako ndio hazina utakayoikuta mbinguni. Kama hukuwa unatoa sadaka account yako mbinguni ni zero, utateseka na njaa huko mbinguni. Ngoja nikuimbie kawimbo "toa ndugu, toa ndugu, ulicho nacho, kwa kuwa bwana anakuona mpaka rohoni" kaeni kwa follen, mtu asibaki kwenye dawati.
 
kwamba wana lazimishwa kutoa

wao wana pewa neno na faida/hasara za kutoa sadaka wanatoa kwa mapenzi yao shida iko wapi
NENO? Mbona huyo mhubiri hakutajirika kwa kusikiliza NENO?? Yeye anakupa maneno halafu anataka pesa yako!!
 
Kama unataka kufuata maandiko peleka fungu la kumi Yerusalemu hekaluni. Kinyume na hapo umejitungia mafundisho yako mwenyewe kwamba kanisa ndio mbadala wa hekalu ambapo Mungu aliagiza sadaka zipelekwe. Wayahudi wenyewe waliopewa hilo agizo hawakupeleka fungu la kumi wala sadaka hata kwenye sinagogi ambayo wanatheolojia uchwara wanalifananisha na makanisa ya leo. Upumbavu tu na umbumbumbu wa kutokuijua imani ya kikristo na misingi yake. Wakimbieni matapeli.
 
Mbinguni kuna njaa?? Mbona hata hilo Agano jipya linasema wazi miili ya kule ni tofauti? Hazina inayoongelewa ni lugha ya picha. Maandiko mengi ukitasoma kwenye lugha mama za biblia ( Kiebrania, Kiaramayo na Kigiriki) utagundua tafsiri za lugha zingine zimechakachuliwa mno na kupoteza maana. Ni kama walivyokosa tafsiri ya Yesu kusema sababu pekee ya kumuacha mke wako ni uzinzi. Walikaa hapo Zanzibar kutafsiri biblia kwa Kiswahili wakakosa neno halisi la UNDUGU WA DAMU wakaweka Uzinzi!!!! Hatari na nusu!
 
Wapenda miujiza na upako, sijui kama watakuelwa.
wanapenda short cut
 
Sema Sasa Biblia imeruhusu walawi wale madhabahuni ila Hawa wa makanisa ya Marlboro au maturubali wamezidi aisee. They are purely business people... Na wanatumia maandiko vibaya kujinufaisha...
👇👇👇👇👇👇

1 Wakorintho 9:13-27​

1 Wakorintho 9:13-27 BHND​

BHNSUVNenoSRUV
Je, hamjui kwamba wanaotumikia hekaluni hupata chakula chao hekaluni, na kwamba wanaotoa sadaka madhabahuni hupata sehemu ya hiyo sadaka? Bwana aliagiza vivyo hivyo; wahubiri wa Habari Njema wapate riziki zao kutokana nayo. Lakini, mimi sikutumia hata mojawapo ya haki hizo. Na wala siandiki nijipatie haki hizo; kwangu mimi ni afadhali kufa kuliko kumfanya yeyote aone kwamba najisifu bure. Ikiwa ninaihubiri injili, hilo si jambo la kujivunia; hilo ni jukumu nililopewa. Na, ole wangu kama sitaihubiri injili! Ningekuwa nimeichagua kazi hii kwa hiari, basi, ningetazamia malipo; lakini maadamu naifanya ikiwa ni wajibu, hiyo ina maana kwamba ni jukumu nililopewa nitekeleze.


WATU WANASHINDWA KUELEWA KUWA TUNAAMBIWA SIKU ZA MWISHO WATATOKEA MANABII WENGI LAKINI WAONGO.
👇👇👇👇👇👇👇

Mathayo 24:4-28 BHN​

BHNSUVNenoSRUV
Yesu akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa na mtu. Maana wengi watatokea wakisema kila mmoja kwamba yeye ndiye Kristo nao watawapotosha watu wengi. Mtasikia juu ya vita na fununu za vita; lakini msifadhaike, maana hayo hayana budi kutokea, lakini mwisho wenyewe ungali bado. Taifa moja litapigana na taifa lingine; ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine. Hapa na pale patakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi. Yote hayo ni kama mwanzo wa maumivu ya kujifungua mtoto. “Kisha watawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifa yote yatawachukieni kwa sababu ya jina langu. Tena, wengi wataiacha imani yao, watasalitiana na kuchukiana. Watatokea manabii wengi wa uongo watakaowapotosha watu wengi. Kwa sababu ya ongezeko la uhalifu, upendo wa watu wengi utafifia. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokolewa. Ila, kabla ya mwisho kufika, hii Habari Njema ya ufalme wa Mungu itahubiriwa ulimwenguni kote kama ushuhuda kwa mataifa yote.
 
kaamua kutajirika kwa kutoa neno shida iko wapi
Huo ni utapeli. Neno kila mtu anaweza kutoa. Hao ni motivational speakers kwenye kichaka cha dini. Hakuna mtume wala nabii hapo upuuzi mtupu
 
Mwamposa amewekeza kwenye kucheza na Akili za watu.

He is an Entrepreneur.
 
Kwani wao ni walawi? Mtu ana shamba ekari kumi ni mlawi? Walawi ni wana wa Lawi, moja ya watoto wa Yakobo ambao walipoingingia nchi ya Kanaani Mungu hakuwapa sehemu ya ardhi kama wale kabila zingine 11. Hawa walipewa ukuhani ili wahudumu hekaluni tu kwa hiyo wale kabila zingine waliagizwa kutenga sehemu ya kumi ya mapato yanayotokana na ardhi waliyopewa walete hekaluni ili wana wa Lawi wapate mahitaji yao. Siku hizi matapeli wamejinyakulia maandiko hayo kuwaahadaa wasiojua ili kujinufaisha.
 
Gharama za uendeshaji wa mkutano huo kama watu hawatalipia kwa njia ya sadaka, nani atagharamia?
Jamii yetu watu wanaupeo mdogo sana
Hawafikiriagi zile gharama za mkutano
Yaani tunawatu wanaopenda vya bure sana na mbaya zaidi anayeongea hivyo ni mwanaume na anafamilia
 
Reactions: K11
Usafiri kutoka Riverside hadi kanisani kwa malisa ni bure halafu fikiria kanisani wanauza maji lita moja tsh 2000 mo energy 1000 juice 2000 check akili hiyo wakati wa kurudi Riverside ni kwa gharama zako
 
Yap ndio maana nasema, haya makanisa ya Sasa na watumishi wa Sasa wanatumia Hilo gepu vibaya......

Infact mtumishi wa Mungu anatakiwa asiwe na kazi au biashara ingine kama wito wake ni kuhubiri neno la Mungu maana huwezi kuwatumikia mabwana wawili. Mungu na pesa...

Lakini Hawa wa kisasa Wana Hadi mabodigadi, ndege, misururu ya magari na majumba kibao.... Useless kabisa
 
Jamii yetu watu wanaupeo mdogo sana
Hawafikiriagi zile gharama za mkutano
Yaani tunawatu wanaopenda vya bure sana na mbaya zaidi anayeongea hivyo ni mwanaume na anafamilia
Hapo ndioi utapeli unapopenyeza. Asilimia tisini ya hao unaowasemea ni matapeli. Mbona nimekupa mfano wa mtume Paulo au hukuelewa? Acheni kuwaibia raia kwa kisingizio cha dini. Yesu mwenyewe kuna wakati alikosa kodi ikabidi Petro akatafute sarafu kwenye tumbo la samaki. Jama ni kukusanya sadaka Yesu ndiye angekuwa na ukwasi wa kutosha maana mafundisho na miujiza yake ilikuwa kabambe siyo haya mazingaombwe ya wahubiri wa leo.
 
acha kuwafanya watu misukule kwakujiweka kati, kila mtu ana maumivu ya kutokurizika na maisha yake
 
Katiba ya Tanzania inahimiza uhuru wa kuabudu
Hakuna uhuru usiokuwa na mipaka. Kwa hiyo katiba inaniruhusu hata kuchinja watu kutoa kafara kama imani yangu inanitaka kufanya hivyo? What are you taking about? Nikianzisha leo ibada inayowataka waumini kufanya ibada na maandamano mitaani wakiwa uchi wa mnyama katiba bado itaniruhusu kwa sabababu imetoa uhuru wa kuabudu???
 

Mpaka waseme hakuna sadaka ndiyo tutawaelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…