Hakuna Kiingilio!! Kichekesho na utapeli wa mialiko ya mikutano ya injili

Umenena vema. Kazi ipo kuwaelimisha raia na kuitaka serikali ikomeshe huu utapeli. Ni aibu mno hata mataifa mengine yanapoangalia ujinga huu unaoendelea kwetu. Tunakuwa ni watu tusiojitambua.
 
Reactions: rr4
Kuingia ni bure,ila kama unahitaji kubalikiwa kwa baraka zinazotokana na utoaji lazima utoe sadaka,kama uhitaji baraka hizo,wewe ingia bure toka bure bila baraka,ni kama lock up ya polisi utaingia bure ukihitaji uhuru toa kitu kidogo uwe huru au komaa hivyohivyo bila kutoa kitu kidogo uozee lock up.
 
Upumbavu mtupu. That is a stupid analogy uliyotoa wala haina uhusiano kabisa na mambo ya imani.
 
nenda na usitoe simple!!!kwan unalazimishwa??
 
Mungu akusamehe maana hujui utendalo.
 
Mahubiri ya miujiza, mafanikio ni kuhubiri wizi
Na mamlaka zinawaangalia tu. Huwa najiuliza au wanawaogopa? Sielewi kwa kweli. Basi tuseme tu kutapeli kwa jina la dini RUKSA ili tujue moja.
 
Huyo anatetea asichokijua ama la ni miongoni mwa wavivu wanaonufaika na sadaka..mitume walihubiri neno na kutenda miujiza mikuu na ya ajabu...watu walileta sadaka nyingi lkn ziligawiwa kwa wahitaji na masikini, haya matapeli ya kileo yamejilimbikizia mali na ukwasi huku waumini wao wengi wako na umaskini uliotopea...
 
Sio wote Huwa wanatoa.
Kutoa ni hiyari Yako.
Hawakushikii Bakora ili utoe.

Msitake kuonekana mna Akili Kwa kujadiri hoja zisizo na maana.
 
Hayo matapeli yameacha kuhubiri juu ya upendo na kusaidia wenye mahitaji, yatima na wajane...badala yake wanashindana kufanya makongamano ya kuvuna sadaka huku yakijilimbikizia mali na ukwasi mkubwa...ni wapi mitume wa Y esu walijenga magorofa na kuwa na misafara ya magari ya kifahari na mabodigadi?
 
nenda na usitoe simple!!!kwan unalazimishwa??
Niende kufuata nini? Maana hata mafundisho ya maandiko matakatifu hakuna huko. Huko hujifunzi historia ya imani yenyewe, wala fafanuzi ( Hermeneutics) za biblia, wala lugha za biblia. Niende kufanya nini?? Kupoteza muda kuhubiriwa sadaka?? Stupid!
 
sasa hapo kosa ni la wahubiri au ujinga wa hao wakristo

kwa nini ww usingeqnzisha kanisa lako ufundishe neno kwenye context ili uwaondoe ujinga??
 
Sio wote Huwa wanatoa.
Kutoa ni hiyari Yako.
Hawakushikii Bakora ili utoe.

Msitake kuonekana mna Akili Kwa kujadiri hoja zisizo na maana.
Kwa nini basi mafundisho yao yamejikita kwenye kutoa tu. Hawafundishi hata elimu ya biblia na hostoria ya ukristo ni KUTOA KUTOA KUTOA basi!!
 
Mungu akusamehe maana hujui utendalo.
Mungu yupi? Huyo wa kwako wa fungu la kumi na sadaka maalum au Mungu YHWH???? Acheni kuliangamiza taifa letu kwa uchu wenu wa pesa. Time has come to awaken our nation. Imetosha upuuzi wenu.
 
Ndio maana naiomba serikali yetu ilitupie jicho suala hili. Ni utapeli umekuwapo miaka mingi bila kushughulikiwa. Taifa linafanywa la mazezeta. Ni aibu.
 
sasa hapo kosa ni la wahubiri au ujinga wa hao wakristo

kwa nini ww usingeqnzisha kanisa lako ufundishe neno kwenye context ili uwaondoe ujinga??
Hawataki neno halisi wanataka miujiza tu basi. Huko makanisani wanaenda kufuata miujiza siyo kumjua Mungu.
 
Ndiyo shida ya hawa wanaojiita wakristo wasiojua hata robo ya biblia. Kazi yao kwenda kusomewa mistari ya biblia ya kutoa sadaka. Hovyo kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…