Hakuna kitu kinaleta Stress kama kuota Mvi au upara halafu bado hujajipata

Mimi kila siku huwa nasema wewe ni kilaza. Unajua mtu aliyeanzisha KFC? Unajua alikuwa na miaka mingapi wakati anaanza? Wacha kukatisha vijana wa Tanzania tamaa. Kufanikiwa hakuna umri, kuna watu wanapiga mpaka miaka 80 ndiyo kinaeleweka.

Kilaza ni wewe ambaye upeo wako upo chini.
Unapotaja miaka 80 unajua Life Expectancy ya Watanzania?
Kwenye ukoo wenu ni wazee wangapi wamefikisha miaka 80?

Ukijadili hoja na mimi hakikisha wiki nzima umekunywa maziwa Fresh ili akili iwe active.

Wéwe unazungumzia Exceptional ndio únashikilia bango
 
Hongera sana mkuu
H
 
Kwani hakuna watanzania wanapitisha miaka 80? Na hata kama hakuna hivi ulichoandika huoni ni ujinga mtupu na unafanya watu wakate tamaa baada ya umri fulani?
 
Ila kuna raha yake umri ukiendana na mipango yako, mfano ulipanga ukifika miaka 30 uwe na Kiota chako, Mke na Mtoto alafu unafikisha miaka 30 hivyo vyote unavyo hapo upara, Mvi, Mikunjo Usoni na ije tu... ila sio ulivyopanga vyote umefanikiwa kufikisha miaka 30 tu hapo Utosi lazima upate moto kimtindo
 
Kwani hakuna watanzania wanapitisha miaka 80? Na hata kama hakuna hivi ulichoandika huoni ni ujinga mtupu na unafanya watu wakate tamaa baada ya umri fulani?

Ñimekuuliza unajua life expectancy ya Tanzania NI ngapi?
Pili nikakuuliza kwenye ukoo wenu ni wangapi wametoboa hiyo miaka 80?

Tatu unajua nguvu kazi ya nchi ipo katika umri upi na upi?

Nne, unajua ni kwa nini kwenye kipengele cha kuomba kazi kuna kipengele cha umri?
Tano, unajua ni kwa nini mtu anatakiwa kustaafu akiwa na miaka 60?

Sikatishi mtu tamaa kwa sababu hata mimi naweza kuwa mhanga, kinachojadiliwa hapa ni uhalisia, ukweli uliowazi.

Sasa wewe unataka maneno matamu ya uongo ili kudanganya Watu wasichukue hatua?

Mimi ni Kilaza Mkuu.
 
Kuna case nyingi nimekutana nazo kuhusu vijana wanaokufa mapema huku wameacha mali .

Wazazi wao hupenda kuhoji huyu mtu Hana mtoto , hamumjui mwanamke aliyezaa nae kwenye pita pita zenu .

Kulikuwa na case Moja 18 yrs old tunduma huko alikufa kijana Kwa ajali ya boda boda , tulifika msibani mama mtu alikiwa akilia sana , huku akilalamika umeniacha peke yangu , hujaniachia mtoto /mjukuu all of sudden akaja Binti ni mjamzito akasema alikuwa na mahusiano na kijana wao , somehow alirelieve That momma's pain . Mpaka naondoka Binti alipokea malezi ya hadhi ya kifalme .. Mpaka anajifungua ..

Nikaconclude kama Taikon /namesake ulivyosema mafanikio makubwa ni kuwa na familia
 
Hapa dawa inakuwa double kiki na visungira tu baasi.haha
 

Case study ni Kanumba
 
Sijui kama anaelewa Life expectancy ya Tanzania ni ngapi, wazee wanaofikisha miaka zaidi ya 80 ni wachache sana.

Yeye anataka maneno yakutiwa Moyo, atoke kwenye Comfort Zone apambane aache ujinga ashukuru Mungu anapata sehemu yakukumbushwa na kutiwa hasira ya kujipanga na kupambana upya. Jamaa huyo ni kihiyo.
 
Hili bandiko lako linafanya vijana wakate tamaa, find something else to lift them up.
 
Kwani hakuna watanzania wanapitisha miaka 80? Na hata kama hakuna hivi ulichoandika huoni ni ujinga mtupu na unafanya watu wakate tamaa baada ya umri fulani?
Ukate tamaa, embu toka kwenye hiyo Comfort Zone unayo ikumbatia, Watanzania tunapenda kuwa polished sana ukweli hamtaki kuambiwa.

Wewe unaona ni sawa kijana ana miaka 35 yupo kwa baba na mama kula ugali wa shikamoo, ataweza kuwa na familia, mtoto na maendeleo.
 
Hili bandiko lako linafanya vijana wakate tamaa, find something else to lift them up.
Hakuna watu watoke kwenye Comfort Zone wapambane kama unakata tamaa ni wewe. Mtibeli katoa andiko bora la kufunga mwezi Januari.
 
Hakuna watu watoke kwenye Comfort Zone wapambane kama unakata tamaa ni wewe. Mtibeli katoa andiko bora la kufunga mwezi Januari.
Mvi na upara vs maendeleo mkuu. Havina uhusiano wowote, kuna wanaanza kuwa na hizo vitu at 25, vipi nao wakate tamaa kuwa tayari mvi/upara umeota huku hawana kitu.

Be logical mkuu.
 
Mvi na upara vs maendeleo mkuu. Havina uhusiano wowote, kuna wanaanza kuwa na hizo vitu at 25, vipi nao wakate tamaa kuwa tayari mvi/upara umeota huku hawana kitu.

Be logical mkuu.
Sasa kama havina uhusiano iyo habari ya kukata tamaa inakuja wapi

Stress ni predisposition factor ya ku Lower body immunity na hormonal change hivyo inapelekea nywele kunyonyoka na kupata upara mapema na pia kama huna maisha mazuri lishe mbovu na mvi zitakuja pia. Kwa hiyo vina mahusiano na kukosa maendeleo/ ajira kwa vijana inayosababisha persistent stress mtu anaingia kwenye pombe kali and staffs like that body immunity inakuwa shaked, hormonal imbalance n.k

Genetic mnapenda kuisingizia sana, wenye familia za namna hiyo ni chache sana haziendani na ongezeko la sasa la mvi na vipara vya mapema.

Mimi ninakubali sio kwamba nimefanikiwa kwa kila kitu ila nakubaliana na jambo, najipanga vizuri ili nisizidi kupoteza muda kwenye ujana uzee uwe worse zaidi.

Elimu ya sasa hivi imetengeneza watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri (reasoning) au ndio extended high school kama Jeneral Ulimwengu alivyosema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…