Tetesi: Hakuna Mbunge wa kuletea Jimbo maendeleo unlesss atumie pesa zake mwenyewe, Hizi Mindset ni za kijinga sana.

Tetesi: Hakuna Mbunge wa kuletea Jimbo maendeleo unlesss atumie pesa zake mwenyewe, Hizi Mindset ni za kijinga sana.

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
5,532
Reaction score
14,164
Maendeleo ya nchi yataletwa na sera nzuri za kitaifa sio za Jimbo moja la uchaguzi au Mbubunge pale Jimboni kwake.Hizi hadaaa zina tucost sana.

Hizi mindi set ndio hufanya wananchi mfano kule Vunjo walimchagua Kimei waki connect na CRDB Bank kwamba labda pesa za CRDB zitahamishiwa vunjo na raia watakuwa na maendeleo kama ilivyo CRDB Bank. Sasa mambo ni tofauti kabisa na wanajuta ila ni kwa sababu ya mind set zao za kijinga.

Kule Morogoro Abood ni tajiri ila maendeleo ya pale yanahitaji sera nzuri za Serikali kuu, na sio kugawa Mabasi kwenda misibani.

Singida waliwahi ongozwa na Mo wakiamini zile pesa zake zingehamia Singida na raia wangekuwa nanpesa kama alivyo Mo, lakini wapi shida ziko pale pale.

Yaani hii nchi ilivyo na rai wajinga huwa mgombea Ubunge anakuwa connected na pesa zake na wanamchagua wakiamini kwa sababu ni tajiri basi na wao watakuwa matajiri, kwa sababu ana pesa na wao watakuwa na pesa.

Marehemu Mengi mfano angeamua kugombea Ubunge angeshinda kwa asilimia 99 kwa sababu raia wangeamini kwa sababu zile pesa zake sasa zitakua pia ni zao raia na angegekuwa matajiri kama yeye.

Diamond anaweza kuwa Mbunge sio kwa sababu anajenga hoja hapana kwa sababu ana pesa au umarufu na wanazania sasa ule umarufu utakuwa coverted into maendeleo ya jimbo, hizi ndio akili zetu.

Babau tale alichaguliwa kwa sababu ya kuwa karibu na Diamond na raia walivyo wajinga wakazania itakuwa translated into maendeleo.
 
Natamani kila mpiga kuea afahamu KAZI ZA MBUNGE KWANZA
Ulichokiandika mtoa mada, ni turufu inayotumiwa na ccm kuwahadaa wananchi waliopo kwenye lindi la UMASIKINI NA kukata tamaa
 
Mleta maendeleo ni serikali kuu kupitia utekelezaji wa ilani ya chama kinachoongoza dola. Yale maneno ya wabunge "nitajenga daraja, barabara mara soko" pasina kuwaambia wapiga kura atajengaje ni hekaya tupu zile. Bahati mbaya kama ulivoandika mtoa mada uelewa wa wapiga kura wengi uko chini sana kung'amua hizi hadaa.
 
Back
Top Bottom