Hakuna mchezaji wa Simba anayeingia kikosi cha kwanza Yanga

Hapa umbumbumbuni anayeweza kucheza Yanga kidogo ni Kapombe kutokana na majeruhi ya Yao

Wengine wote labda waanzie bench
Sio kweli mzee, yule boka mwenye miguu kama ndege joni hamuwezi tshabalala,
Niambie una mudathiri na ngoma yupi unaanza nae..
Winger ya kushoto sababu utamtumia pacome basi mpanzu ataanzia nje ila tofauti na pacome hakuna wa kumuweka mpanzu nje..
Ukiwa na camara kisha una diarra itakubidi upige ana ana doo
Kibu anazidiwa vitu fulani na nzengeli, lakini ukimtoa nzengeli akaingia kibu mchakamchaka wake beki anaweza omba sabu
Huwezi kuanza na job, kisha yule hamza akae benchi ni big NO

Ni ahoua tu ambae hata uwanja wa mazoezini hapaswi kufika🤣

Ukisoma comment yangu, ungekuja na majibu tu kaka 🤣
 
Boka ana energy ya kupanda na kukurudi kukaba, ana skills zaidi ya Shabalala za kukaba
Ngoma mlinganishe na Aucho ndo wanacheza namba 6 wote
Hamza hawezi kumweka bench Job wala Bacca

Hapo Simba nitamchukua Kapombe
Na Balua binafsi huyu kijana namhusudu kipaji chake

Balua inatakiwa aje Yanga tumtoe Farid na Nkane
 
Basi km hayo ndio maamuzi yako.. Hata kwa aucho bado ngoma ni bora zaidi, ngoma anakuoffer vitu vingi zaidi ya aucho
 
Wachezaji wa Simba ambao kila timu inayojielewa inatamani kuwa nao.
1. Kibu Denis
2. Ellie Mpanzu
3. Shomari kapombe
4. Hamza
5. Fabrice Ngoma
6. Débora Mavambo

Kufungwa na Yanga haimaanishi Simba ni wabovu, it's a matter of mindset and timing.

Siamini kama hii Simba mnayoibeza ingekuwa group moja na
Al Hilal Omdurman
Tp Mazembe
Mc Alger
Isingefuzu kwenda quarter finals.
Unaweza kuwa na majina makubwa sana ila usifanye makubwa.
 
Basi km hayo ndio maamuzi yako.. Hata kwa aucho bado ngoma ni bora zaidi, ngoma anakuoffer vitu vingi zaidi ya aucho
Duuuh basi naheshimu mawazo yako kama unaona Ngoma ni bora zaidi ya Aucho
 
Hao hawanA hata hadhi ya kucheza CAFCL Sasa wangekutana nao wapi?
Labda wacheze nao friendly match
 
Kama Ngoma anacheza no 6, Yusuf Kagoma anacheza ngapi?
 
Niambie hapo unamtoa nani unamuingiza nani? Debora? Mzee wa Konyagi? Kitale? Mikwala? Ataiba?
Mpanzi? Ifike hatua tuwe na heshima na Soka.

View attachment 3289146
Hii timu anacheza GieSieMu tu hamna kitu hapo.

Kama unabisha, ipeleke kwenye michuano ya kimataifa ambako hakuna utopolo wa GieSieMu kisha ulete majibu hapa.

Jiepushe na wasio na akili japo mfike watatu
 
Yanga nzima haina mchezaji mwenye kiwango bora na mwendelezo kama Zimbwe Jr.
 
Ni kweli hakuna mchezaji wa simba anaeweza kuacha kucheza mashindano ya kimataifa aende Yanga akacheze ndondocup
 
Wakati Simba inaenda Misri kwa ndege, Uto wanaenda Tabora kwa basi huku wakipishana na maroli maeneo ya Chalinze, Dumila na Kibaigwa. Mafuta na maji yameshajitenga tayari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…