Hakuna mjadala, Visungura vinaua nguvu kazi ya vijana, havina tofauti na viroba, serikali itoe tamko juu ya mauaji haya ya makudi

Wapo watakaosema kwamba hakuna anaelezimishwa kunywa hivyo visungura, fine, ila imetosha sasa. Vipigwe marufuku, pombe kali za kiwango hiki hazipaswi kuwa readily available kiasi hiki kama bigijii.

Waweke either kwa packaging ya ujazo mkubwa zaidi ili isizagae na kununuliwa hovyo kama karanga mitaani, au waweke kwenye packaging ghali zaidi ya chupa za kioo, sio hivi viplastiki wanapima kama mkojo na kuuza buku buku.., huu ni uuwaji kabisa..

Serikali ingieni mitaani muone kinachotokea kwa vijana hujo Arusha na kwingineko, hivi mmafurahi watoto wa wenzenu wanavyogeuka mazombi?!
Hata waweke kwenye ujazo wa pipa, bado itapimwa tu kwa buku buku!! Hapo unasemaje?!
 
Dah, noma.

Umenikumbusha huku majuzi nimeshangaa tumekwenda kusherehekea kumaliza mwaka, kwenye Italian restaurant ya kishua, sasa kuna kijana mmoja mdogo kaja na mke wake.

Tumeanza kuagiza vinywaji, yule dada akaagiza some sort of martini drink, yule waiter akamuuliza atoe kitambulisho cha kiserikali kuhakikisha kuwa amefikisha umri wa kunywa pombe.

Yani hata restaurant ikiuza glasi ya wine kwa mtu ambaye hajafikia umri inapigwa faini ndefu. Madukani hupati pombe mpaka kwenye duka maalum lenye kibali cha kuuza pombe, na ukija kununua mtu unaonekana mdogo wanakuuliza kitambulisho wahakiki umri wako.

Inaonekana huko Tanzania watu hawajali mambo kama haya.
Hakuna anayejali.
Wao ilimradi watoto wao wapo Feza international na IST mliobaki huku mtajijua wenyewe.

Kwenye uzi wangu nimeelezea kijana kamchoma kisu mwenzake sababu ya hivi visungura.

Hali ni mbaya mtaani vijana wanakunywa pombe wanalala kwenye mitaro, hawafanyi kazi.

Mamalaka husika zipo tu hakuna wanalofanya.

Ishu ya madubwi ya wachina yamejaa mtaani watoto hawaendi shule wanaishia kucheza madubwi.

Hakuna Hakuna Hakuna hii nchi kila kitu shagarabagara.
 
Za kuambiwa changanya na zako

Ova
 
Kuna wimbo mmoja wa Singeli jamaa anasema siku hizi wameacha viloba mambo ni Safari na Savanna, nikajua tumepiga hatua.

Kumbe kuna visungura?

Sasa visungura vikoje hivyoo?
Yan ni SMART GIN, aloo ina logo ya playboy sasa ndio wanaita kisungura. Ndugu hii pombe ni elfu 2 vijana wanajibandika vitatu kwa 6 mambo wanalewa kabla hata hawajaliZa elfu kumi, madogo janja wa boda boda ndio vitu vyao hivyo…SERIKALI IINGILIE KATI
 
Hakuna anayejali.
Wao ilimradi watoto wao wapo Feza international na IST mliobaki huku mtajijua wenyewe.

Kwenye uzi wangu nimeelezea kijana kamchoma kisu mwenzake sababu ya hivi visungura.

Hali ni mbaya mtaani vijana wanakunywa pombe wanalala kwenye mitaro, hawafanyi kazi.

Mamalaka husika zipo tu hakuna wanalofanya.

Ishu ya madubwi ya wachina yamejaa mtaani watoto hawaendi shule wanaishia kucheza madubwi.

Hakuna Hakuna Hakuna hii nchi kila kitu shagarabagara.
Nimepiga sana vita dubwi alooh nimetukanwa sana daaah kwisha kaz vijana tz
 
Aisee ni hatari, ni vipombe vyenye very high alcohol levels, ambavyo vimefanywa so readily available kwa kuwekwa kwenye vichupa vidogo vya plastiki, wanauza sijui buku buku huko mtaani, vimesambaa na vinapatikana hovyo hovyo kama bigijii.., aiseee

Kuna kijana mmoja mtaani nilimuona sikuamini, kijana alikuwa kidari zamani, alikuwa na afya nzuri sana na mwenye muonekano mzuri, ila kwa sasa kabaki skeleton, kawa kama chizi muokota makopo, akiamka hadi anaenda kukala ni visungura , hata kula hali.., hivi hii serikali yetu haijali vijana namna hii.., mnataka hadi tuanze kutembea na mabango mabarabarani huku tukiimba na kulia, ?! Why??!
Juzi tu hapa tumezika dogo kitaa hekaheka za mwaka mpya kavigomga kinyama ...kazima...kwenda hospital wamechelewa kavuta....
 
Wapo watakaosema kwamba hakuna anaelezimishwa kunywa hivyo visungura, fine, ila imetosha sasa. Vipigwe marufuku, pombe kali za kiwango hiki hazipaswi kuwa readily available kiasi hiki kama bigijii.

Waweke either kwa packaging ya ujazo mkubwa zaidi ili isizagae na kununuliwa hovyo kama karanga mitaani, au waweke kwenye packaging ghali zaidi ya chupa za kioo, sio hivi viplastiki wanapima kama mkojo na kuuza buku buku.., huu ni uuwaji kabisa..

Serikali ingieni mitaani muone kinachotokea kwa vijana hujo Arusha na kwingineko, hivi mmafurahi watoto wa wenzenu wanavyogeuka mazombi?!
Acha kuharibu starehe za watu
 
Hakuna anayejali.
Wao ilimradi watoto wao wapo Feza international na IST mliobaki huku mtajijua wenyewe.

Kwenye uzi wangu nimeelezea kijana kamchoma kisu mwenzake sababu ya hivi visungura.

Hali ni mbaya mtaani vijana wanakunywa pombe wanalala kwenye mitaro, hawafanyi kazi.

Mamalaka husika zipo tu hakuna wanalofanya.

Ishu ya madubwi ya wachina yamejaa mtaani watoto hawaendi shule wanaishia kucheza madubwi.

Hakuna Hakuna Hakuna hii nchi kila kitu shagarabagara.

Halafu kwa nini inaongelewa smart gin wakati kuna zingine kama cuca, burudani na kiki ambazo ni kali zaidi kama gongo ??.

Ukweli ni kuwa hizi pombe zimeletwa kama mbadala wa viroba na hata zikipigwa marufuku, bado watu watahamia kwenye mataputapu

Hivyo, long term solution sio kuvipiga marufuku ila iangaliwe namna ya kudhibiti ubora lakini pia uwepo wa bear ambazo zitauzwa kwa bei rahisi maana ukikaa na vijana, ukawauliza sidhani kama wanazifurahia sanaa ila ndio njia iliyopo ya kujiboost kwa bei rahisi
 
Dah, noma.

Umenikumbusha huku majuzi nimeshangaa tumekwenda kusherehekea kumaliza mwaka, kwenye Italian restaurant ya kishua, sasa kuna kijana mmoja mdogo kaja na mke wake.

Tumeanza kuagiza vinywaji, yule dada akaagiza some sort of martini drink, yule waiter akamuuliza atoe kitambulisho cha kiserikali kuhakikisha kuwa amefikisha umri wa kunywa pombe.

Yani hata restaurant ikiuza glasi ya wine kwa mtu ambaye hajafikia umri inapigwa faini ndefu. Madukani hupati pombe mpaka kwenye duka maalum lenye kibali cha kuuza pombe, na ukija kununua mtu unaonekana mdogo wanakuuliza kitambulisho wahakiki umri wako.

Inaonekana huko Tanzania watu hawajali mambo kama haya.
Nobody cares mkuu

Na hapa wameongelea hizi pombe kali maana bado kuna sigara za 100 ambazo watoto wadogo haswa wa shule wanazitumia kwa sababu zipo cheap

Kiufupi hatuna udhibiti thabiti na jamii haina mfumo wa kuleana kama zamani. Kwa sasa mtoto wako anaweza kuwa muhuni, anavuta bhangi na kashindikana ila usijue peke yako mtaa mzima haswa ukiwa hujichanganyi na watu
 
Nimepiga sana vita dubwi alooh nimetukanwa sana daaah kwisha kaz vijana tz
Mimi mpaka kutishiwa mkuu.

Niliongea na jamaa mmoja mmiliki wa hilo dude nikamwambia kwanini usiweke jioni na upige marufuku watoto wa shule, akamiambia acha ujinga na ufanye yako.

Nikamwambia mamlaka husika sikizilliona ili utakuwa matatizoni, alichonijibu jamaa nilichoka, akaniambia mamlaka zote ni pesa, na hakuna wakunizuia.
 
Wapo watakaosema kwamba hakuna anaelezimishwa kunywa hivyo visungura, fine, ila imetosha sasa. Vipigwe marufuku, pombe kali za kiwango hiki hazipaswi kuwa readily available kiasi hiki kama bigijii.

Waweke either kwa packaging ya ujazo mkubwa zaidi ili isizagae na kununuliwa hovyo kama karanga mitaani, au waweke kwenye packaging ghali zaidi ya chupa za kioo, sio hivi viplastiki wanapima kama mkojo na kuuza buku buku.., huu ni uuwaji kabisa..

Serikali ingieni mitaani muone kinachotokea kwa vijana hujo Arusha na kwingineko, hivi mmafurahi watoto wa wenzenu wanavyogeuka mazombi?!
Hata visungura visipokuepo hao vijana wa hovyo watakunywa pombe chafu
 
Sijui hata ni kitu gani hicho, huu unaonekana ni mjadala wa wajuzi wa ulevi, jadilini mtuletee mapendekezo watu timamu tuone tunawasaidiaje.
 
Ningekuwa bosi wa mamlaka ya kudhibiti dawa za kulevya, hivi vinywaji vya kulevya na kuharibu afya na akili za wananchi ningezipiga marufuku bila kujali zinaingiza kodi kubwa. Kuber ilipigwa marufuku vijana wakahamia kwenye kubugia tumbaku kuendeleza ulevi wao, viroba navyo vilipigwa marufuku wakahamia kwenye kisungura, kinyau, high life na vingine vya aina hiyo, ulevi upo palepale
 
Dah, noma.

Umenikumbusha huku majuzi nimeshangaa tumekwenda kusherehekea kumaliza mwaka, kwenye Italian restaurant ya kishua, sasa kuna kijana mmoja mdogo kaja na mke wake.

Tumeanza kuagiza vinywaji, yule dada akaagiza some sort of martini drink, yule waiter akamuuliza atoe kitambulisho cha kiserikali kuhakikisha kuwa amefikisha umri wa kunywa pombe.

Yani hata restaurant ikiuza glasi ya wine kwa mtu ambaye hajafikia umri inapigwa faini ndefu. Madukani hupati pombe mpaka kwenye duka maalum lenye kibali cha kuuza pombe, na ukija kununua mtu unaonekana mdogo wanakuuliza kitambulisho wahakiki umri wako.

Inaonekana huko Tanzania watu hawajali mambo kama haya.
Uliondoka lini Tanzania?; Kweli hujui hali tunavyoishi bila utaratibu huku Africa? Huku hata kiduka cha kuuza nyanya mwenyewe kaficha kiboksi cha visungura anauzia mtu yoyote. Tena anagawa nusu nusu anauza buku buku.
 
Siamini kwamba watu wa juu huko hawaoni tatizo....

Kuna mahali rupia inapenyezwa wanaangalia pembeni.
Hapana, visungura vinatangazwa kwenye radio na tv tena wakati wa taarifa za habari wakati wengi wanatizama. Hakuna sheria inayokataza pombe ila kuna muda wa kufungua bar. Sasa visungura ni portable. Mtu ananunua anaweka mfukoni anaenda kijiweni. Wengine wanauza hapohapo vijiweni. Kudhibiti ni ngumu kama watumiaji hawatajielewa.
 
Back
Top Bottom