Hakuna mjadala, Visungura vinaua nguvu kazi ya vijana, havina tofauti na viroba, serikali itoe tamko juu ya mauaji haya ya makudi

Mnawapambania vijana lakini sijui Kama vijana wanatambua hili jambo.

Kweli vijana wamepoteza Nuru na wamebaki mifupa na wanakufa Sana

Lipo la kujifunza.
 
Upo sahihi Ila serikali inauwezo wa kupiga marufuku pombe zote .
 
Serikali haiwezi kupiga marufuku kwani vinatumiwa na chawa wa CCM wanaotumiwa kushangilia kwenye mikutano.
 
Daah hivi vidude ni hatari sana.
Tarehe 1/1/2024 sita isahau Tumempoteza mwamba kaenda na kitambi chake.
Kagonga visungura mixer Kilimanjaro.
Rest in peace Madiluu!
Shida kubwa zaidi pombe feki zinafyatuliwa sana mitaani.
K vant na Konyagi nazo pia kwa sasa ni hatari sana nyingi ni feki. Wenye viwanda pamoja na serikali wameshindwa kudhibiti pombe feki.
 
Sisi huku tunaandika tu 'hairuhusiwi chini ya miaka 18.
Kutoka hapo mtajua wenyewe!
 
Lile dude limesababisha had madogo hawasomi shule aloo sijui serikali haiangalii haya madude wengi wanaoenda pale miaka 12-17 sasa si umri wakuwa shule huo aisee hili swala wangeliangalia kinamna nyingine
 
Kuna wimbo mmoja wa Singeli jamaa anasema siku hizi wameacha viloba mambo ni Safari na Savanna, nikajua tumepiga hatua.

Kumbe kuna visungura?

Sasa visungura vikoje hivyoo?
Visungura ukinywa wiki tu mashavu yanakua kama ya paka shume.
 
Wafanyabishara na walevi watabuni kitu kipya.
Kwa ufupi mlevi akiwa na kiu ya pombe yuko tayari hata kulawitiwa ili tu apate pombe. Hata wakuweka kwenye chupa kubwa ya laki moja hawataweza kupunguza kasi ya ulevi katika jamii. Watachanga watalinunua hilo lichupa.
Dawa ni moja tu watu wampokee Yesu awaondolee kiu ya dhambi au serikali ipige marufuku aina zote za pombe.
Nchi yenye rasilimali zisizohesabika kutegemea Kodi ya pombe ni ujinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…