Hakuna mjadala, Visungura vinaua nguvu kazi ya vijana, havina tofauti na viroba, serikali itoe tamko juu ya mauaji haya ya makudi

Hakuna mjadala, Visungura vinaua nguvu kazi ya vijana, havina tofauti na viroba, serikali itoe tamko juu ya mauaji haya ya makudi

Mnawapambania vijana lakini sijui Kama vijana wanatambua hili jambo.

Kweli vijana wamepoteza Nuru na wamebaki mifupa na wanakufa Sana

Lipo la kujifunza.
 
Hapana, visungura vinatangazwa kwenye radio na tv tena wakati wa taarifa za habari wakati wengi wanatizama. Hakuna sheria inayokataza pombe ila kuna muda wa kufungua bar. Sasa visungura ni portable. Mtu ananunua anaweka mfukoni anaenda kijiweni. Wengine wanauza hapohapo vijiweni. Kudhibiti ni ngumu kama watumiaji hawatajielewa.
Upo sahihi Ila serikali inauwezo wa kupiga marufuku pombe zote .
 
Wapo watakaosema kwamba hakuna anaelezimishwa kunywa hivyo visungura, fine, ila imetosha sasa. Vipigwe marufuku, pombe kali za kiwango hiki hazipaswi kuwa readily available kiasi hiki kama bigijii.

Waweke either kwa packaging ya ujazo mkubwa zaidi ili isizagae na kununuliwa hovyo kama karanga mitaani, au waweke kwenye packaging ghali zaidi ya chupa za kioo, sio hivi viplastiki wanapima kama mkojo na kuuza buku buku.., huu ni uuwaji kabisa..

Serikali ingieni mitaani muone kinachotokea kwa vijana hujo Arusha na kwingineko, hivi mmafurahi watoto wa wenzenu wanavyogeuka mazombi?!
Serikali haiwezi kupiga marufuku kwani vinatumiwa na chawa wa CCM wanaotumiwa kushangilia kwenye mikutano.
 
Daah hivi vidude ni hatari sana.
Tarehe 1/1/2024 sita isahau Tumempoteza mwamba kaenda na kitambi chake.
Kagonga visungura mixer Kilimanjaro.
Rest in peace Madiluu!
Shida kubwa zaidi pombe feki zinafyatuliwa sana mitaani.
K vant na Konyagi nazo pia kwa sasa ni hatari sana nyingi ni feki. Wenye viwanda pamoja na serikali wameshindwa kudhibiti pombe feki.
 
Dah, noma.

Umenikumbusha huku majuzi nimeshangaa tumekwenda kusherehekea kumaliza mwaka, kwenye Italian restaurant ya kishua, sasa kuna kijana mmoja mdogo kaja na mke wake.

Tumeanza kuagiza vinywaji, yule dada akaagiza some sort of martini drink, yule waiter akamuuliza atoe kitambulisho cha kiserikali kuhakikisha kuwa amefikisha umri wa kunywa pombe.

Yani hata restaurant ikiuza glasi ya wine kwa mtu ambaye hajafikia umri inapigwa faini ndefu. Madukani hupati pombe mpaka kwenye duka maalum lenye kibali cha kuuza pombe, na ukija kununua mtu unaonekana mdogo wanakuuliza kitambulisho wahakiki umri wako.

Inaonekana huko Tanzania watu hawajali mambo kama haya.
Sisi huku tunaandika tu 'hairuhusiwi chini ya miaka 18.
Kutoka hapo mtajua wenyewe!
 
Mimi mpaka kutishiwa mkuu.

Niliongea na jamaa mmoja mmiliki wa hilo dude nikamwambia kwanini usiweke jioni na upige marufuku watoto wa shule, akamiambia acha ujinga na ufanye yako.

Nikamwambia mamlaka husika sikizilliona ili utakuwa matatizoni, alichonijibu jamaa nilichoka, akaniambia mamlaka zote ni pesa, na hakuna wakunizuia.
Lile dude limesababisha had madogo hawasomi shule aloo sijui serikali haiangalii haya madude wengi wanaoenda pale miaka 12-17 sasa si umri wakuwa shule huo aisee hili swala wangeliangalia kinamna nyingine
 
Kuna wimbo mmoja wa Singeli jamaa anasema siku hizi wameacha viloba mambo ni Safari na Savanna, nikajua tumepiga hatua.

Kumbe kuna visungura?

Sasa visungura vikoje hivyoo?
Visungura ukinywa wiki tu mashavu yanakua kama ya paka shume.
 
Wafanyabishara na walevi watabuni kitu kipya.
Kwa ufupi mlevi akiwa na kiu ya pombe yuko tayari hata kulawitiwa ili tu apate pombe. Hata wakuweka kwenye chupa kubwa ya laki moja hawataweza kupunguza kasi ya ulevi katika jamii. Watachanga watalinunua hilo lichupa.
Dawa ni moja tu watu wampokee Yesu awaondolee kiu ya dhambi au serikali ipige marufuku aina zote za pombe.
Nchi yenye rasilimali zisizohesabika kutegemea Kodi ya pombe ni ujinga
 
Back
Top Bottom