Hakuna mkoa mzuri wa kuishi kama Mbeya hapa Tanzania

Mkuu, sioni tofauti kubwa sana ya ujenzi holela baina ya Mbeya na Mwanza.
Kama ilivyo Mbeya, Mwanza ina maeneo mengi ambayo mpangilio wake ni holela.
 
Vyote hivyo viko centralized,ingekuwa hivyo ungekuta Mikoa yote imepangwa..

Ukisema Mbeya haijapangwa Sasa Mwanza utasemaje? Dar Je?
 
Kila mkoa uko njema sana kwa kuishi hata mbeya fresh punguzeni chuki humu .
 
Bajaji nyingi Sana kule

Hakuna migahawa mizuri mjini hakuna

Watu wa mbeya ni wastaarabu Sana huwezi lala njaa kule labda uamue unaweza anza na mmama mmoja Kansani unaenda kwingine unawasalimia tu 😂😂 utakaribishwa chakula watakupa na ndizi au karanga uende nazo Hafu fresh tu hawana noma

Wadada wa mbeya sura za baba zao ila makalio Sasa aisee 😂😂😁😍😍
 
Pesa zingeonekana. Mwanza huitaji kuitetea kila kitu kinajionesha. Kwa nini mbalali haibadiriki kama watu wanahela.
Mbeya ina watu wengj wenye vishughili shughuli.
Acha mzaha basi,Mbarali ipi ambayo haibadiliki?

Unazungumzia Mwanza,hivi ukiacha Mwanza Mjini Kuna Wilayani gani huko Mwanza inaweza fanana na Wilaya yeyeote ya Mbeya ikiwemo Mbarali?

Kwamba ukienda Kwimba au Ukerewe Kuna mzunguko wa hela? 😁😁😁

Acha vichekesho Mkuu ,tofayya Mbeya na Mwanza ni kwamba maendelea ya Mbeya yamesambaa Wiakaya zote na huko Mwanza Yako hapo Mjini na sababu kubwa ni kwamba Wilaya za Mbeya Zina fursa ya kuvutia watu kuishi huko huko badala ya kukimbilia mjini..

Na hii sifa sio ya Mbeya tuu Bali Mikoa yote ya Nyanda za Juu Kusini unlike Mikoa mingine ambako maendelea Yako concentrated kwenye Miji mikuu Yao..
 
Kwa Sasa usajili wa Bajaji umesitishwa hivyo zitapungua na kuwa replaced na usafiri wa Umma yaani daladala.
 
Kwahiyo kumbe unafanya comparison Kati ya Mwanza na Mbeya?
Nimeishi Dar, Sumbawanga,Singida,Arusha,Babati,Songea,Mwanza,Mpanda,Mbeya,Njombe nk..hapo sijataja sehemu nilizofika na kuishi Kwa mda mfupi kama wiki au Kupita tuu.
 
Naunga mkono hoja. Pia watu wake wana utu na ni waaminifu. Wanawake wa Mbeya ni kivutio kikubwa zaidi kisichotajwa sana... wamejaliwa makalio ya dunia nzima. Mimi niko mbioni kuweka makazi huko. Mbeya hakuna stress. Kuna unafuu na kibiashara pamekaa poa sana kutokana na connection yake na Malawi & Zambia.
 
Tanzania yote ni nchi nzuri sana duniani kama ulikuwa hujui, tembea kila mkoa, nchi takatifu sana hii, ina kila kitu, Mungu katupendelea sana.
Upo sahihi kila ukanda una jambo zuri.
Ila climatically mbeya ni ni 1.
Watanzania wengi hatujajua kutumia fursa adimu walizoziona mababu zetu.
Huwa naamini kuwa a Bantu man was very intelligent man whenn it come to land, they were very selective. A father of Bantu was geneous! walituchagulia maeneo mazuri sana ya kuishi tofauti na Nilotics, Kush, Khoi walichagua kuishi jJangwani na kwenye nyika.
Wabantu ndio wanamiliki maziwa makuu ya Afrika na Dunia, wanaishi ktk mabonde mazuri na mito mikubwa, waluweza kimiliki wanyama wa pori na wa kufugwa.
Tukumbuke kuwaenzi babu zetu wametuachia urithi mkubwa sana.
 
Nimeishi Dar, Sumbawanga,Singida,Arusha,Babati,Songea,Mwanza,Mpanda,Mbeya,Njombe nk..hapo sijataja sehemu nilizofika na kuishi Kwa mda mfupi kama wiki au Kupita tuu.
Okay


Kwahiyo ukaona Mbeya ni Bora kuliko kote
 
Vyote hivyo viko centralized,ingekuwa hivyo ungekuta Mikoa yote imepangwa..

Ukisema Mbeya haijapangwa Sasa Mwanza utasemaje? Dar Je?
Sijasema Dar, akileta mtu stori ya Dar tutoa mapungufu yao. Dar pamoja na mapungufu yao ila ule mji angalau unamuonekano wa jiji. Mwanza vilevile pesa inaonekana inafanya kazi. Mbeya ni jiji kubwa ila hakuna wenye pesa ndefu wakuweza kulifanta jiji liwe kama mwanza. Arusha dijawahi fika sipajui.
 
Hiyo mikoa maisha mdebwedo sana inawafaa wavivu na wajinga Maana hutumii akíli nyingi kuishi.

Tanzania ni DAR, ARU, MWZ na DDOM tu. Kwingineko tutakuja kutalii tu kipindi cha likizo kupanga natural air.
 
Sahihi kabisa, nafurahi kuwa hapa, huu mfungo Sasa hakuna shida sijui ya futar, vyakula vyote vinapatikana tena kirahisi, natarajia kubadili kabila ivi karibuni na jina langu jipya nitaitwa Mwaluswaswa!!
 
Kwani Mbeya Haina muonekano wa Mji?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…