Hakuna mkoa mzuri wa kuishi kama Mbeya hapa Tanzania

Kigoma,Ukerewe,Bukoba Kuna Ziwa vipi mbona watu hawajakaa? Mtwara na Tanga Kuna bahari Kwa nini pulling factor ya bahari haijawavuta?😁😁

Acha porojo sababu nilizokupa ndio za kitaalamu.
Sababu za kihistoria.
Mfano Kigoma imezungukwa na nchi zenye vita muda wote nani ataenda kuwekeza? Serikali haikujenga barabara mapema, mkoa upo pembezoni sana. Kutoka tabora mpaka kigoma mapori makubwa sana hakuna mwingiliano.
Kusini haikukuwa na barabara nzuri kama mbeya. Tanga ni jiji hivyo lina hadhi sawa na Mbeya, Tanga inashindwa na Dar na pwani as a pulling factor, kwa sababu ni karibu hivyo Dar inawavuta zaidi kuliko Tanga, Kuna mambo mengi sana ktk kukua kwa miji.
Ni sawa ba kusema lwa nini Tunfuma inakua kuliko Mbalali.
Hivi Mbeya usipolima na kuwa mchuuzi wa mazao utafanya ishu gani nyingine,.
Fursa ya mipaka inatimiwa na wageni zaidi kuliko wenyeji.
Vitu vingi vinasafirishwa kwenda mikoani badala nje ya mipaka, kwa hio Mbeya imekuwa njia panda ya wageni badala uwe fursa kwa wanambeya.
Kaskazini wanajitahifi zaidi kusafirisha mazao kenya kuliko kusini.
Tujadili ktk mtazamo chanya sio hasi maana hii mikoa tunaishi wote, hivyo maendeleo ni ya wote.
 
Hata kama shida ni simu,lakini jaribu kufanya editing mkuuu
 
Una matatizo makubwa sana,Kwa hiyo pale Jijini watu wote ni wachuuzi wa mazao hakuna biashara zingine au siyo?

I tired of your nonsense.
 
Me nilishauri kwa Watumishi Mkuu ingawa hata wasio watumishi.

Ukishakuwa na uhakika wa chakula hata utafutaji mwingine inawezekana
 
Mbeya ina mandhari nzuri kwa kuishi but upatikanaji wa hela ni mgumu pia miundombinu kama barabara bado sana ukitaka uichukie mbeya ni kipindi cha kiangazi utapachukia kwa kweli
 
Mbeya ina mandhari nzuri kwa kuishi but upatikanaji wa hela ni mgumu pia miundombinu kama barabara bado sana ukitaka uichukie mbeya ni kipindi cha kiangazi utapachukia kwa kweli
Upatikanaji wa hela ni mgumu? Wapi pesa zinapatikana kirahisi watu waende Waka make life?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…