Hakuna mwanasiasa/Rais aliweza kupambana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na akashinda!

Aliye mshauri Mh Rais akae kimya huyo ndio asiyemtakia mema. Unakaje kimya wakati baadhi ya vipengele vya makubaliano ya awali vina ukakasi wa wazi kwa kila mwenye akili timamu kuelewa?

Unaweza kuupotezea waraka wa Maaskofu zaidi ya 30 unao elekezwa kwa namilioni ya wafuasi wao waliokatika kila nyanja ya maisha uijuayo wewe khalafu uwe bado na amani moyoni???, Mungu anahitaji mwenye haki wake mmoja tu kufanya naye kazi. Eliya mmoja aliangamiza makuhani 450 wa mungu baal chini ya Jezeebel???!! CCM na viongozi wenu someni maneno haya ya Biblia, Zaburi 33:16.
 
hawa jamaa wameletwa na Mungu, wametufumbua macho, pamoja na kwamba bado kuna watu wapo gizani na wengine macho wanayo ila hawataki kuona.
 
Sasa hapo shida ipo wapi ? Ukipigania haki na jambo lenye manufaa ya wengi eventually uta-prevail no matter wewe ni nani..., Lakini ukienda vinginevyo mwisho wa siku utaporomoka hata ukiwa nani....; There was a time Theocracy was an order of the day (ila ikafika wakati sehemu nyingi wakaona kinachosimamiwa ni cha wachache na sio kwa faida ya wengi) hivyo uongozi kama huo ulikufa kifo cha kawaida...

Ila Point nayosema na ya maana, kuleta mashindano yasiyo na tija na ubabe wa kitoto ni kupunguza uungwaji mkono....; tuzungumze ni nini kinachopiganiwa kwa wakati husika sababu hii nchi kuna vitu vinavyowagusa wote no matter Imani zao (Kwahio hata Shetani akigombania Haki ya wengi atashinda tu mwisho wa siku)

Post kama hii/ Maneno kama haya wala hayajengi zaidi ya kubomoa
 
hawa jamaa wameletwa na Mungu, wametufumbua macho, pamoja na kwamba bado kuna watu wapo gizani na wengine macho wanayo ila hawataki kuona.
Toa upupu wako mungu gani na ni wachoyo na wabinafsi yote hayo hawajapata mgao hawana lolote safari hii imekula kwao , raisi wetu kanyaga twende tumechelewa sana u know
 
Fafanua mkuu,Covid 19 Magufuli alikinzana na TEC kwenye upande upi wa Corona?
Alisema Corona hakuna Tanzania na akapiga marufuku kuvaa barakoa.Wakatoliki chini ya Fr.Kitima wakasisitiza kuwa Corona ipo na imewaua baadhi ya waumini,mapadre,maaskofu,masista hata mabruda na kuwasihi kuvaa barakoa hata kwenye mikutano ya Magufuri jambo ambalo hakupenda kabisa.Badala yake yeye aligeuka kuwa Papa wa kuwafokea viongozi hao na kuwaambia hawana imani.Unaona kilichotokea?Wakatoliki wanathamini afya na uhai wa waumini wao na ndio maana hata kwenye mkataba huu wa DP World wamejitahidi kuonya ila sisi bado tunawaona kama wanaingilia mambo ya serikali.Uzuri ni kuwa majibu ni hapa hapa duniani.
 
Toa upupu wako mungu gani na ni wachoyo na wabinafsi yote hayo hawajapata mgao hawana lolote safari hii imekula kwao , raisi wetu kanyaga twende tumechelewa sana u know
wachoyo wa nini sasa, wamekunyima ubwabwa? na mgao gani mliodanganywa kwamba maaskofu wa katoliki huwa wanapewa? ukitaka kuwapa hao rushwa nenda kaanze na papa. zote hizo ni propaganda mnadanganyana kwenye tv iman huko baada ya kushiba kalmati.
 
Kama Chifu Hangaya siyo?
Wewe mfano una elimu gani hata ya kumpita mkenya?🤣🤣

Mtu mzima halafu hujielewi !?


Ujinga na ukatoliki wenu ndo umemaliza elimu ya Tz ,kilichobaki ni kusambaza tamaduni zao ila hao maprofessor kama wote hawana kitu kichwani.
 
Hao jamaa wana siri zenu kibao na huwa mnarekodiwa pale mnapo ungama kwaiyo wale pedophiles kwa akili zako wako juu ya serikali na waislamu wote na walutheri

Kama hujui kuwa TEC inaongoza watu na serikali ni watu hao hao ambao wanaongozwa na TEC, basi huwezi pia kujua nguvu ya TEC ndani ya serikali inayotokana na watu ambao wanaongozwa na TEC!
 
ILIKUWA ZAMANI NA SIO ZAMA HIZI, AMBAZO WATANZANIA WANAJIELEWA NA KUJITAMBUA KWA ASILIMIA 100.
 
Baada ya DG Tiss kuondolewa au kubadilishwa ilifuata kulifumua na kulisuka upya baraza la mawaziri ikiwemo kutolewa cheo kipya cha naibu waziri mkuu ambacho hakiko kikatiba nilijua lengo kuu lilikuwa kuupoteza mjadala wa bandari.

Lakini naona ngoma bado iko palepale na waraka wa TEC unaendelea kusomwa kwenye makanisa yote.

Nadhani ni wakati sasa wa serikali kuachana na hili dubwana la DPW
 
Na serikali imesikia na imerudisha mpira kwapani DP na serikali wako mezani kurekebisha kile kinacholalamikiwa
 
Wewe mfano una elimu gani hata ya kumpita mkenya?🤣🤣

Mtu mzima halafu hujielewi !?


Ujinga na ukatoliki wenu ndo umemaliza elimu ya Tz ,kilichobaki ni kusambaza tamaduni zao ila hao maprofessor kama wote hawana kitu kichwani.
Nafanya kazi na Wakenya wananifahamu vizuri na kuniheshimu ila wewe mvivu,mchoyo na mla Rushwa unaona sina elimu na sifai.Nakwambia kwa huu Mkataba wa Hangaya na DP World siwezi kutulia labda kama shuleni nilienda kuhesabu makenchi.Lakini kama nilisoma somo la Historia vizuri na Elimu ya Siasa vizuri nitakuwa mpumbavu wa kiwango cha lami kukubaliana na yasiyokubalika na Watanganyika wenzangu.
 
 

Asante sana kwa majibu mujarabu yakiyoenda shule ya filosophia.

Tuendelee kuwaelimisha wale wasiojua nguvu za TEC nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…