Hakuna mwanaume mwenye mwanamke mmoja, mama usijidanganye

Hakuna mwanaume mwenye mwanamke mmoja, mama usijidanganye

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Haijalishi kuwa wewe ni dini gani, kabila gani, una kazi gani na cheo gani hapa duniani, mfumo wa uzazi wa mwanaume unafanana Na mifumo ya uzazi ya wanaume wengine wa viumbe vingine, hasa wale wenye uti wa mgongo (vertebrate) Na wanaonyonyesha (mamalia).

Viumbe walioko kwenye kundi hili wanaume wanakuwa wachache kuliko wanawake kwa sababu mbalimbali za kabla ya kuzaliwa, wakati wa kuzaliwa na baada ya kuzaliwa. Hivyo wanaume wamepewa uwezo mkubwa wa kutamani Na Kumudu kutembea Na kuzaa Na wanawake wengi kwa wakati mmoja.

Kama mfugaji anavyohitaji majogoo, mabeberu, madume wachache kwa majike wengi bandani au zizini ndivyo hivyohivyo unavyohitaji mwanaume mmoja kwa wanawake zaidi ya mmoja, na hiki kinafanyika utake usitake, ujue usijue, uambiwe au usiambiwe.

Kiuhalisia wanyama wote akiwemo binadamu wana wivu mkubwa, hawapendi kuchanganywa, lakini kama kila mume angebaki na Mke mmoja yafuatayo yangetokea kwenye jamii:

1. Wanawake wengi wasingepata mabwana, wangebaki bikra.

2. Hasira na chuki kwenye jamii ingekuwa kubwa.

3. Sonona, depression ingekuwa kubwa. Kukosa bwana kunachanganya.

4. Population, idadi ya watu ingepungua. Wanawake wengi wasingezaa kwa kukosa mbegu.

5. Idadi ya watu wanaozaliwa na hitilafu ingekuwa kubwa sana. Wanawake wangetembea na mwanaume yeyote hata mwenye hitilafu kubwa za kurithi. No choice.

6. Wanawake wangebweteka sana hadi kuwa wachafu, wavivu, na wajeuri kupindukia.

7. Wanawake wangeuana wenyewe kwa wenyewe ili wapate nafasi itakayoachwa wazi.

Asitokee mwanamke atakaejigamba kuwa yuko peke yake, hata wanaume pia kwa kiasi Fulani.

Kinachotofautiana ni idadi ya wanawake alionao mwanaume na kiwango cha kujificha, usiri mkewe au mumewe alichokuwa nacho.

Jamii ihalalishe ndoa za wake wengi ili iwe huru badala ya kuendesha mambo kwa kificho.

1626245304669.png
 
Kwa hiyo umejichukulia kuwa hauwezi kuwa na mwanamke mmoja, hata pasipo na ulazima?
Niambie kama wewe tangu uzaliwe hujawahi kukwichi na Mke mwingine.

Kama sio Leo basi itakuwa kesho.

Kosa kubwa wanalofanya wanawake ni kudai talaka au kukimbia wanapoona mpenzi au mumewe ana MTU mwingine, hapana usiondoke kwakuwa hata unakokwenda mambo ni hayohayo. Ukiona mume anafanya kwa kujificha ujue kuwa anakupenda na kukuthamini sana, usiondoke.

Kosa lingine ni kumpekuwa mpenzi wako ujue anatembea na nani, usimfumanie mumeo/mkeo kwa makusudi.
 
Haijalishi kuwa wewe ni dini gani, kabila gani, una kazi gani Na cheo gani hapa duniani mfumo wa uzazi wa mwanaume unafanana Na mifumo ya uzazi
Yani ukijiona unaamini kwamba "hakuna mwanaume mwenye mke mmoja" basi jua wewe ni mjinga unaelazimisha watu waamini unachokifanya wewe.

Usitake kuwalisha sumu mbaya wanawake waanze kuwa na hofu na waume zao.

Kwani haitoshi kusema kwamba nature ni mwanaume anaweza kuwa na wake wengi lakini sio lazima kila mwanaume aishi kwenye nature hiyo.

Mnasambaza ujinga sana kwa wanawake.

Wapo wanaume hawana habari na kuwa na mademu wengi japokuwa wanawaona wazuri zaidi ya wake zao lakini hilo hata wanawake pia wanawaona wazuri zaidi ya waume zao.

Kama ambavyo nature ya mwanamke ni kuzaa lakini wapo ambao hawazai,sasa usilazimishe kusema kila mwanamke atazaa au anazaa wengiine hawazai eidha kwa dharura au kutaka wenyewe.

Kutaka kuwaaminisha kwamba kila mwanaume lazima awe na wanawake wengi ni ujuha unaopaswa kupigwa vita.

Hakuna anaekataa kwamba nature iko hivyo lakini kinachokataliwa ni kuwa sio kila mmoja kwamba lazima afuate nature hiyo.

Ziko nature nyingi sana lakini wengine hawaendi sambamba nazo,usijaze watu ujinga kwamba lazima "KILA MWANAUME"

Kuna wanawake wametulia na waume zao wakiinjoi maisha acha kuwa na negativity kiasi hiki.

Usilazimishe kwamba lazima kwa kkla mwanaume iwe hivyo,sema kwa wanaume wengi iiko hivyo,uwingi sio kwamba ni wote.

Badili mitazamo yako aisee.
 
Haijalishi kuwa wewe ni dini gani, kabila gani, una kazi gani Na cheo gani hapa duniani mfumo wa uzazi wa mwanaume unafanana Na mifumo ya uzazi ya wanaume wengingine wa viumbe vingine, hasa wale wenye uti wa mgongo (vertebrate) Na wanaonyonyesha (mamalia). Viumbe walioko kwenye kundi hili wanaume wanakuwa wachache kuliko wanawake kwa sababu mbalimbali za kabla ya kuzaliwa, wakati wa kuzaliwa na baada ya kuzaliwa. Hivyo wanaume wamepewa uwezo mkubwa wa kutamani Na Kumudu kutembea Na kuzaa Na wanawake wengi kwa wakati mmoja.
MKE au WANAWAKE?
 
Sio kweli kabisa unachosema, lazima wewe una kasoro ya kiume, tena kubwa. Walishindwa hata manabii, maaskofu, masheikh, marais wakubwa, nk, sembuse wewe?
Usiwe mbishi we jamaa.

Na huu ni udhihirisho wa ujinga ambao uko nao JUU YA JAMBO HILI.

Ishu ni tamaa zako za mwili.

Wanasema nature mwanamke akiwa katika siku zake za ovulation anakuwa na hamu sana na kuna watu wanaeneza propaganda kwamba hawezi kustahamili lazima atafute mtu ampige mshawasha tu.

Je unataka kutuambia kwamba kila ovulation ya mwanamke hapa duniani lazima atafute mtu ampige mshawasha sio ?
 
Haijalishi kuwa wewe ni dini gani, kabila gani, una kazi gani Na cheo gani hapa duniani mfumo wa uzazi wa mwanaume unafanana Na mifumo ya uzazi ya wanaume wengingine wa viumbe vingine, hasa wale wenye uti wa mgongo (vertebrate) Na wanaonyonyesha (mamalia). Viumbe walioko kwenye


Mungu ameruhusu ndani ya Qur'an kuoa mke zaidi ya mmoja (4), Mungu kisha amuru sasa unataka nani mwingine aamuru??---- Uisilamu raha sana.🤣
 
Back
Top Bottom