Hakuna mwanaume mwenye mwanamke mmoja, mama usijidanganye

Usemapo neno,
Pasi ujuzi mtimilifu,
Utauma meno,
Ujaposutwa udanganyifu,
Nayo matukano,
Utukanayo na kukashifu,
Ndio msumeno,
Utakereza zako sharafu.
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Your browser is not able to display this video.
 
Mnajihangaisha kwelikweli na mwisho ni kujiongezea matatizo tu

Tangu muanze faida ipi mumepata?
Umekuja bila kitu utaondoka bila kitu, faida pekee ni kuzalisha watoto wanawake wengi kadiri utakavyojaliwa ili kwa jina la Mungu kizazi (mankind) kindelee kuwepo na Mungu apate watu wengi watakaomwimbia, kumpigia vinubi na kumwabudu. Usihangaike sana na kutafuta Mali nyingi za kuwaachia watoto, kufanya hivyo ni sawa na kuwaachia watoto wako samaki badala ya kuwaachia nyavu. Waachie maarifa yatakayowasaidia kutafuta maisha Yao wao wenyewe sio kuwaachia watoto maisha.

Alaaniwe yule mwanaume mwenye sifa, afya, nguvu na chakula Cha kutosha kulisha watoto 10 mwenye watoto 2 TU kwa makusudi.
 
Unadhani hawa wa hivi wako wangapi mtaani kwako, kitongojini kwako, kijijini, kata, tarafa, wilaya, mkoa, nchini, Afrika Mashariki, Sadc, Africa na duniani?

Wazungu wanakuja Afrika kutafuta wanaume wa kutembea na kuzaa nao huku, ukikutwa una Rasta umewarahisishia kazi. Nilitembea na mzungu kule Amerika akanifichia passport yangu nisirudi kwetu hadi nizae nae kwanza, wadaku wakanitonya kuwa ukishazaa nae utazuiwa usiridi utunze mwanao. Amerika wanaume ni wachache, wengi wako magerezani, jeshini nje ya nchi, wamekufa, mashoga, walevi na wagonjwa.

Jamani hali sio nzuri, hata huku kutembea Nusu uchi kwa dada zetu, au kuvaa nguo za kuwabana sana ni jitihada za kutafuta wanaume wa kuwasititiri. Hebu fikiria kuwa una dada yako, mtoto wako, mama mdogo wako anaezeekea nyumbani kwenu tena bila mtoto.
 
Mie kwa mume wangu nipo peke yangu!! Mtoe kwenye hiyo orodha yako. Sio kila mwanaume anaendekeza mihemko yake.
Maskini wee [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Anakupenda na anakuheshimu ndio maana hujamshika sisi wenyewe ndio tunajijua acha ubishi
 
Hii tabia wanaume tunaiendekeza sana, na inazidi kuharibu Jamii yetu kila leo, Dunia haina hitimisho moja kwa watu 20 au 1M ambao wameshindwa kuwaheshimu wapenzi wao kwa kuja na visingizo vya kijinga.

Tubadilike
 
Kajiangalie kwenye kioo, jipige kifuani mara tatu alafu sema kwa sauti, Hakika Mimi ni Mjinga.

Alafu kalie chumbani, uwezi kuja tetea kwenye kundi la wanaume alafu unashupalia mzee,daaah ht level yako ya kufikiria ni ndogo sanaa
 
Kajiangalie kwenye kioo, jipige kifuani mara tatu alafu sema kwa sauti, Hakika Mimi ni Mjinga.

Alafu kalie chumbani, uwezi kuja tetea kwenye kundi la wanaume alafu unashupalia mzee,daaah ht level yako ya kufikiria ni ndogo sanaa
Nakusikitikia, unadhani una chamaana unakifanya hapa duniani kabla hujafa. Unadhani Cha maana kwako ni kujenga majumba, kununua magari, kudanganya watu kwenye nyumba za ibada, kutafuta pesa na vitu vingine vya aina hiyo. Kitu Cha maana kwako ni kuwa mtu na kuwa mwanaume au mwanamke na kazi zake baasi, nyingine ni nyongeza TU.

Umeumbwa na kuitwa mwanaume kwa kazi moja TU ya kuzalisha wanawake. Uanaume wako utapimwa kwa idadi ya watoto uliozaa kabla hujafa (uzao wako hapa duniani). Dunia inafaidika kwa kuacha watoto kuliko kuacha magari, majumba na makampuni ambayo yanachakaa, yanabomoka, yanafilisika na kuchafua mazingira.

Wewe huna akili kabisa, huangalii, huoni wala hujui kwanini uliumbwa hivyo ulivyoumbwa.
 
Kumbe akili ni umalaya ambao ww ndio umejua ndio umeumbiwa kusex hovyo?? Ikiwa umeshindwa hata kung'amua hilo dogo, pole sana ila sina neno zaidi ya kukwambia amini unachoamini, ila sio kila unachoamini ni sahihi..

wanyama wenyewe wanafanya mapenzi siku wakiwa tayari kwa ajili ya kushika mimba, wewe ukiwa ndio kiongozi wa Wanyama Ulipewa mamlaka hayo, unakuja leta mada za aina gani hizi, unataka uaminishe watu ujinga huu kweli??

Uliandika ukiwa sawa au hasira au K veve ilikua imeshika hatamu??
 
Wacha ni mwambie kitu hapa, binadamu sio kiongozi wa wanyama wote. Binadamu ni kiumbe sawa na viumbe wengine ambao kiongozi wao na muumba wao ni MwenyeziMungu pekee. Kilichofanyika ni Mungu kuvipa viumbe sifa, afya, nguvu na maarifa tofauti ili tusigombanie mahitaji yetu kwenye mazingira tunamoishi. Kama binadamu angekuwa kiongozi wa wanyama na viumbe vingine wote tusingesumbuliwa na hata kuuawa na mbu, nge, nyoka, manyigu, nyuki, Simba, inzi, bacteria, viruses, fungus, minyoo, protozoa, nk. Uongozi wake uko wapi hapo?

Kunguru anaweza kuruka lakini binadamu hawezi, mchwa anatengeneza vichuguu binadamu hawezi, nyuki anatengeza asali binadamu hawezi, fisi na tai wanakula mizoga hawafi binadamu hawezi, samaki anaishi majini wewe huwezi..

Binadamu anatengeneza ndege ambayo ataanguka nayo kwa ujinga wake, anatengeneza gari ambalo atapata ajali nalo na kufa, anatengeneza gorofa litakalomuangukia, nk. Hivyo kaka hakuna kiumbe ambacho ni dhaifu au imara au superior au inferior kuliko kingine mbele za Mungu. Kila kiumbe kimepewa sifa, afya, nguvu, uhodari na kazi maalum kwaajili ya viumbe wengine. Mfano, bila mchwa hakuna mimea wala kilimo. Lakini, pamoja na tofauti zote hizo viumbe wote akiwemo wewe wanahitaji hewa, maji, kupunzika, chakula, kuzaa, kujisaidia, kuhisi (iritability), kutembea, nk. Kusema binadamu ni kiongozi wa wengine ni kumkufuru Mungu.

Ila Ila Ila, kusema ukweli Kuna wanaume ambao wameruhusiwa kuzaa watoto wachache sana au kuacha kuzaa kabisa. Wanaume hawa ni wale ambao:
1. Hawana nguvu za kiume za kutosha.
1. Miili Yao imebeba vinasaba (genes) za magonjwa ya kurithi to kama vile sickle cells, Kansa, kifafa, ukichaa, magonjwa ya moyo na damu, kisukari, pumu, makengeza, albino na magonjwa mengine ya kurithi ambayo yatawasumbua watoto watakapo zaliwa na vizazi vyao. Kila mtu awaepuke kuzaa nao watu wanaotoka kwenye familia zenye magonjwa haya ili kupunguza kuendeleza vizazi vyenye magonjwa haya.
3. Wazee: wazee Wana mbegu mbovu zisizofaa kuwa mbegu. Unaweza kuzaa mtoto kituko
4. Magonjwa ya kuambiza kama HIV, kaswende, gonorea,

Je, wewe kaka uko kwenye makundi haya?
 
Kwa hiyo umejichukulia kuwa hauwezi kuwa na mwanamke mmoja, hata pasipo na ulazima?
Sio hiari, ulazima lazima uwepo. Hii ni kanuni ya viumbe vyoote chini ya jua. Kila kiumbe (species) inafanya kila liwezekanalo kizae na kuacha watoto wake wengi kabla yakutoweka duniani. Yaani hakuna kiumbe makini kinachokubali kufa bila kuzaa watoto wengi kupitiliza. Hii inasaidia kutunza kizazi chake kisipotee duniani. Ndio maana hana wadudu wa magonjwa kuna wakati wanakwepa(resistance) dawa na chanjo zenye lengo la kukatisha kizazi chao. Leo hii unalikuta dume la binadamu eti lina watoto 2 tu, ukiliuliza eti linakwambia maisha magumu, shenzitype, hivi kama babu yako angezaa mtoto mmoja tu kwenye mazingira yaliyojaa magonjwa ya malaria, minyoo, kuumwa na nyoka, kifaduro, polio, ndui, tetanus, surua, ajali, TB, ukoma, nk unadhani ingekuwaje kwenye ukoo wenu?

Kama huwezi kufanya kile tu alichofanya babu na baba yako, utawezaje kufanya yale anayotaka Yesu na Mungu uyafanye?
 
Vitu muhimu vyote ni lazima kwa jambo fulani. Mfano, Kupumua ni muhimu lakini sio lazima kama unataka kufa. Kuzaa watoto wengi ni muhimu lakini sio lazima kama hutaki kizazi chako kibaki duniani milele, yaani unataka mtoto mmoja tu ambae akifa kwa malaria au ajali basi na mbegu yako imeishia hapo.
 
Nina Mke 1 Na nimeridhika kabisa. Sasa ukware ulionao usifikiri wote ni wakware, tuombe radhi isee!
Hakuna wa kukuomba radhi hapo, wewe ni mgonjwa. wanaume hawako hivyo, nenda kamuulize babu yako akwambie. Kwakuwa watu wote wako hivyo ndio maana yule mwanafalsafa alikuja na amri kumi (ten commandments) ikiwemo ya usizini. Mtu hawezi kutungia sheria watu 3 tu wanaofanya kosa hilo. Ina maana karibu watu wote wenye akili na afya timamu wanatembea na wake na waume wengi ndio maana akajaribu kutunga sheria hizi kama anaweza. Lakini tangu Musa atoe hizi amri zake 10 miaka maelfu yaliyopita unaona mabadiliko yoyote? ni mataahira tu ndio wanaozifuata. yaani kila watu 20,000,000 unapata mtu mmoja tu mwenye mke mmoja (abnormal). Na huyo mwanaume anachapiwa mke wake na wenzie. Hakuna mwanamke anapenda mume kama huyo, variety is the spice of life.
 
Hakuna kusex hovyo kama unavyosema, sex sio starehe bali kwaajili ya kuzaa (reproduction) TU. Unapokaa na mbegu kwenye makende yako huku kuna wanawake mahali ambao wanataka kuzaa lakini hakuna wa kuwazalisha hio sio sawa. Badala ya kupeleka mbegu zinakohitajika wewe unammiminia mwanamke (mkeo) ambae hataki kuzaa (anableed, au ana mimba tayari, au ananyonyesha, au anaumwa au ana huzuni fulani eti kwakuwa umeambiwa na wapuuzi kuwa uwe na Mke mmoja, huko ni kuingilia mipango ya Mungu na makusudi ya kukuumba uwe mwanaume mwenye mbegu zinazotosha kuzalisha wanawake wengi. Kama unavyotaka uwe na jogoo wachache kwa mitetea mingi ndivyo Mungu anataka kwa viumbe vyote.

Kuwa na Mke mmoja tuu maana yake unamsex hata anapobleed, anapokuwa na mimba, anaponyonyesha, anapoumwa na anapokuwa hajisikii vizuri. Hii sio sawa kama unafanya hivyo, maana hata mbwa hasex na mbwa mwenye mimba au mwenye watoto wachanga, hata mbweha hawafanyi hivyo.

Mpuuzi mmoja amekufundisha kuwa eti Mke na mume ni mwili mmoja, upuuzi kabisa huo, pale mezani kila mtu anatia chakula mdomoni kwake, mwanaume anampiga mwanamke, maumivu ya mmojawapo ni yake TU vipi uwe mwili mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…