Hakuna namna, Wamasai lazima wakubali kuondoka Ngorongoro kwa hiari yao

Hakuna namna, Wamasai lazima wakubali kuondoka Ngorongoro kwa hiari yao

1.Ngorongoro ni jina la wilaya
2 Ngorongoro ni jina la tarafa iliyopo ndani ya wilaya ya Ngorongoro yenye tarafa tatu
3.Ngorongoro ni jina la kreta iliyomo ndani ya tarafa ya Ngorongoro
4.Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro ni eneo lote la tarafa ya Ngorongoro
Wafugaji wanaohamasishwa kuhamia Msomera ni wale wanaoishi ndani ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro(Tarafa ya Ngorongoro )na kwamba si Wafugaji wote katika eneo hilo wanatakiwa kuhama
5.Si mara ya kwanza serikali kuchukua hatua ya kupunguza idadi ya wafungaji ndani ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro (tarafa ya Ngorongoro)kwani serikali iliwahi kuwahamisha wafungaji wa jamii ya kabila la wamag'hati au Watatoga kwenda maeneo mengine nje ya hifadhi hatukusikia kelele
Mkuu hongera kwa kutuelimisha, wengi wanaopinga hawajui hicho ulichoandika. Kongole maalon
 
Mkuu hongera kwa kutuelimisha, wengi wanaopinga hawajui hicho ulichoandika. Kongole maalon
Nimeelezea upande mmoja tu wa eneo la hafadhi ya Ngorongoro lakini mgogoro uliopo kwenye headlines sasa ni eneo la pori tengefu la Loliondo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 4,000 eneo hili ni muhimu kwa ikolojia ya mbuga za Serengeti na Masai Mara ya Kenya na jamii ya eneo hilo kiini (centre)cha mgogoro ni kwenye eneo la kilomita za mraba 1,500 ambazo serikali inataka wafugaji waondoke na wasiingize mifugo huko ili kulinda ikolojia ya Serengeti na bahati mbaya eneo hilo wakati wa utawala wa awamu ya pili walipewa waarabu kuwa eneo lao la uwindaji (sielewi walipewa kwa mkataba gani,wa miaka mingapi) hayo ni maelezo kwa lugha nyepesi kuhusu mgogoro uliopo Loliondo kati ya serikali,muwekezaji na jamii,Serikali inasema wanahifadhi eneo hilo kwa manufaa ya Serengeti na jamii inayozunguka eneo hilo wakati jamii inaona inaondolewa kwenye eneo hilo ili waachiwe waarabu na wanaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa eneo hilo limeuzwa kwa waarabu
 
Okay. Kwanini sasa Wakenya na NGOs zao ndiyo wamekaza mishipa kuifokea Serikali ya Tz?
 
Wamasai wako zaidi ya laki 2 huko Ngorongoro sasa hizo nyumba walizojengewa Handeni ni ngapi?
Acheni propaganda!
Hao laki mbili hawako kwenye takwimu za NCAA. Na ndio tunaowalenga maana walijificha nyuma ya wale halali.
 
Watanzania wenzangu, Ngorongoro ni lazima ilindwe kwa nguvu zote.

Japo Wamasai hawataki kuondoka Ngorongoro kwa hiari yao kama maeneo mengine ambapo paliwahi kufanyika operation kama hii lakini ni lazima waondoke ili nia njema ya serikali ya kuilinda na kuhifadhi ngorongoro yafanikiwe.

Hatuwezi kuchekea kundi dogo la watanzania wenzetu kutuharibia rasilimali yetu, wametengewa maeneo mazuri kabisa kwa ajili ya shughuli zao, wamejengewa makazi na huduma Bora za kijamii Kama maji, shele na hospital zinapatikana lkn wanaigomea serikali kwa hoja za kipuuzi kabisa.

Pia Wamasai hawana ubavu wa kushindana na serikali wasidanganywe na hizi kelele za wapingaji ambao ni waoga, wanafiki na watakaa pembeni wamasai wabishi watakapoanza kushughulikiwa.

Kwa hili la Ngorongoro naiunga mkono serikali ya Mama Samia, kwamba kuongoza nchi sio kuchekeana chekeana.
Akili yako haina akili! wewe ungekubali kuhamishwa kwenu huko Nakapanya na Kintinku?! Wamasai wako malaki ya binadamu, makazi nyumba 100 ndio kitu gani? Na kwa nini sasa, sio katika awamu ya 5?! uharaka ni wa nini, kwa nini tusitoe muda wa majadiliano na kuafikiana! Ngorongoro ni "multiple land use area", samahani kama nimekuacha wewe kayumba skuli! Ni eneo la matumizi mchanganyiko, binadamu na wanyama, leo kwa nini unawasukuma binadamu waondoke, wakati kuna zuio la mahakama ya afrika mashariki?! Ubabe wa nini? Ubabe ulimfikisha wapi magufuli? mbona kaacha kila kitu, uraisi uliokuwa unampa kiburi, familia yake, mali zake zote za halali na za dhuluma!
Maasai ni binadamu sio bidhaa, za kutumia na kutupa isipokufaa, Something needs to change in our politics; and that is The race for money and glory, and to focus on human governance. Nonsense!
 
Okay. Kwanini sasa Wakenya na NGOs zao ndiyo wamekaza mishipa kuifokea Serikali ya Tz?
Maasai wengi wa Ngorongoro na Maasai wa Narok Kenya ni jamii moja inayoitwa Loita hawa hawajui habari ya mpaka wa nchi na pengine wamaasai wa Narok Kenya wanafaidika zaidi kuchungia mifugo yao eneo la Loliondo kuliko wamaasai wa Loliondo kuchungia mifugo yao Narok.Hii inaweza kuwa sababu mojawapo
 
ila hata hivyo ukiacha na hizo tetesi za mwarabu kupewa ngorongoro, hifadhi haipo salama kama wataendelea kuishi himo. watanzania tuache ushabiki wa kijinga

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu huu ushabiki unasababishwa na kikundi cha watu kukataa KUELEWESHWA WAKAELEWA. Kwa sabab zao za MAPENZI au CHUKI BAINIFU ya VYAMA vya KISIASA. Wanaeneza Ujinga Kwa ajenda zao za kutaka kuitoa CCM sijui na kuipaka shombo.

Mimi hata kama si mpenzi au mshirik wa siasa moja Kwa moja siwez kukubali wenezi huu. Ile idadi inayoongezeka pale mbugani (Kam ulivyosema) si rafiki Kwa Ecology. Hawa Wamasai sio tu kula wanyama ushujaa wao wanaumalizia Kwa simba mkuu.

Fikiria hii Kasi baada ya miaka 20!. Ukisimama na mitazamo ya uchama hapo huwez kuona, hata ukioneshwa hutaki kuelewa. Sasa ndo tujiulize Kwa nini hawatak kukubali? Hawan hoja za kuelweka utasikia sijui mababu! Mara kuuzwa! [emoji3064] Kile sio Chama kama kinalisha watu unga wa NDELE

Sent from my VTR-L29 using JamiiForums mobile app
 
Acha nikwambie ukweli uliojificha sasa. Jambo hili lina pande mbili: Mosi, ongezeko la watu na mifugo ni hatari kwa uhifadhi, hii nadhani inatokana na wenyeji kutokua waminifu na wazalendo.

Wamekaribisha mifugo ya Wakenya na wanafanya siasa hifadhini, na ndiyo unaona leo kelele zinapigwa sana Kenya. Hatujiulizi maeneo yale yana Wabunge na Bunge lipo on! Kwanini wabunge hawasimami? Ila Kenya wanamuomba Mh Uhuru aje aongee na Rais Samia. Kwa lipi? Wote tujiulize.

Pili, uhifadhi wa mazingira wa Ngorongoro ni mkubwa sana, na ndiyo maana kila mfugaji tajiri awe Kenya au Tanzania atapeleka mifugo kule kwani nyasi ni nyingi sana kwa ajili ya wanyama pori na maji yapo throughout the year, na ndiyo ugomvi, wameharibu mazingira katika maeneo yao wanaingiza mifugo yao kwenye hifadhi.

Hifadhi ni km 1500 za mraba, eneo la wamasai wamepewa km 2500 za mraba kwa ajili yao na mifugo. Sasa wanataka zile km 1500 za mraba na wao wawepo! Kama umefuatilia jana yupo mkenya ametoa kauli ya serikali kuacha mara moja uwekaji wa alama za mawe kuzunguuka hifadhi.
 
Acha nikwambie ukweli uliojificha sasa. Jambo hili lina pande mbili: Mosi, ongezeko la watu na mifugo ni hatari kwa uhifadhi, hii nadhani inatokana na wenyeji kutokua waminifu na wazalendo.
Hujui unalozungumza we mwanamke. Ongeza utafiti wako.
 
Hakuna kitu inaitwa makazi ya kudumu ya Kabila fulani hapa nchini, Serikali ina mandate ya kubadilisha matumizi ya ardhi yake wakati wowote inaona inafaa. Ilitokea kwa wakazi wa Kakola (Kahama) enzi hizo ilipokuwa inaingia Barrick kuchimba dhahabu. Wenyeji walihamishwa. Kuna ugumu gani kwa wamasai?
Hata ikitokea Wachaga wanaingilia hifadhi ya mlima Kilimanjaro watahamishwa mara moja.
Uhuni mtupu. Muwape tu waarabu ardhi na huko muwauzie pembe zote zilizooneshwa royal tour.
 
Back
Top Bottom