mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 14,205
- 19,142
Same applies. Na hiyo ya muhula wa pili na hadi wamalize mitihani ya muhula wa kwanza.Kwani kuna watu walitaka walipe ada nusu? Mimi nililipa ada Januari ya miezi 6 nusu mwaka..mwezi wa tatu Covid 19 ikaingia sasa hivi nasubiria nilipe ya nusu mwaka uliobaki maisha yaendelee...
Wapo wenye shule wanaodai pamoja na hizo za chakula na usafiri kwa kipindi hicho.Gharama ambazo mzazi hapaswi kulipa ni gharama za chakula na usafiri kipindi Cha likizo ya dharula.
Kama unarisiti unawapelekea tuu kuwaonesha kuwa ushalipa.Kama nililipa ada yote ya muhula wa kwanza, hili unalizungumziaje?
Hadi sasa hakuna walichodai. Nilimuuliza mleta mada maana amegeneralise hajui kwamba kwa shule zenye mihula miwili ada huwa inalipwa mwanzoni mwa mwaka. Na COVD-19 imetokea ikiwa wanafunzi wanaendelea na masomo ya muhula kwa kwanza ambayo bado hawajafanya mitihani.Kama unarisiti unawapelekea tuu kuwaonesha kuwa ushalipa.
Hiyo ndiyo hekima inayopaswa kutumika. Si lazima azilipe zote kwa Mara moja Bali utaratibu wa kulipa kidogo kidogo kwa makubaliano. Cha msingi ni kwamba makubaliano yakulipa yaeleweke.Kulipa lazima,tulipe maana huduma itatolewa,hata kama imechelewa,
Ila lazima tuelewe kwamba,sio waalimu tu walioathirika na covid19,hata sie wazazi kuanzia march mpaka June,mapato yamepungua,kwahiyo ile ada ambayo,tulitakiwa kulipa April,ilitumika kuendeshea maisha,sasa ni busara tukiweka utaratibu ,while/walimu wapate mapato,na sie tuwe na ahueni ya kulipa,tutalipa ada yote,lakini ingekuwa vzr tulipe kidogokidogo
Hapo itakuwa huna deni. Utalipa tu mhula wa pili. Tatizo ni kwa wake ambao hulipa kwa awamu mbili kwa kila mihula. Alilipa awamu ya Kwanza Jan hadi March. Awamu ya pili April hadi June hakulipa na shule zikafungwa! Hao ndio wanataka wasilipe kwa kuwa watoto hawakufundishwa! Lakini like ambacho hawakufundishwa lazima kitafidiwa! Utata uko hapo!Kama nililipa ada yote ya muhula wa kwanza, hili unalizungumziaje?
Hayo ndiyo maneno ya kuzungumza! Hiyo ndiyo busara inayotakiwa!tutalipa tu, ila tupeane nafasi ya kulipa
Kama ulishalipa muhula wote wa Kwanza hapo haudaiwi.Kama unarisiti unawapelekea tuu kuwaonesha kuwa ushalipa.
Hapo haudaiwi!Kama nililipa ada yote ya muhula wa kwanza, hili unalizungumziaje?