Hapo umeongelea na kuegemea zaid kwenye kumaliza maada zilizosalia kwa kipindi cha Corona na kujaribu kuonyesha ulazima wa kulipa pesa, lakini hujaonyesha uhalisia wa namna wanafunzi watakavyozielewa mada hizo katika uwingi wake! Hata kama walimu watazicover zote lakini uelewa wa wanafunzi hautakuwa sawa na ambavyo wangefundishwa mada hizo katika kipindi cha ile miezi ya March hadi June! Hapa shule zinaogopa tu gharama za kuwarudishia wazazi pesa ambayo haikuwa na matumizi , kwahiyo wanajaribu kujenga hoja ya kuwalazmisha wazazi wengine kulipa pesa hizo, lakini kiuhalisia pesa hizo si chumo halali kwa vyovyote itakavyokuwa! Wamiliki wengi wa shule binafs walikataa kuwalipa mishahara wafanyakazi wao kwa madai kuwa hawapo kazini sasa leo wanawadai wazazi pesa ya kazi ambayo walimu hawakufanya!?