Mkuu 'Allen Kilewella'; hivi kweli una hakika hututoi kwenye reli wakati huu na mada ya aina hii?Hawa ni Marais wa nchi tangu Tanzania ianzishwe
1. Julius Kambarage Nyerere 1965 - 1985 (miaka miaka 20)
2. Ali Hassan Mwinyi 1985 - 1995 (miaka 10)
3. Benjamini William Mkapa 1995-2005 ( miaka 10)
4. Jakaya Mrishi Kikwete 2005 - 2015 ( Miaka 10)
5. John Pombe Magufuli 2015 - 2021 (Miaka 5 na miezi 5)
6. Samia Suluhu Hassan 2021 hadi Sasa.
Kati ya hawa Marais hakuna rais hata mmoja aliyefikia viwango vyq Julius Kambarage Nyerere kwenye nyanja mbali mbali kuanzia uchumi, demokrasia, diplomasia, na maendeleo ya jamii.
Usinielewe visivyo, sisemi kuwa mada yako si sahihi; lakini lengo lake kwa wakati huu ni lipi hasa?
Pengine labda ingependeza, kama mada ingejikita kwenye hizi tawala na HAKI za wananchi wao!
Tunajuwa nyakati ni tofauti, lakini nadhani kwa mtu mwenye mawazo huru angeweza kuona kuwa mTanzania wa wakati huo wa Mwalimu, pamoja na kuwa na chama kimoja cha siasa, alikuwa HURU na HAKI zaidi ya huyu wa leo; pamoja na kuwa huyu wa leo amekuwa nazo fursa za kupata elimu pana zaidi ya kujuwa UHURU, na HAKI zake; vitu muhimu zaidi kupigania haki zake.
Sasa unatupeleka kwenye viwanda, wakati 'critical' kama huu tusahau kabisa hata hilo tegemeo dogo la "NORNOE"?
Hili na mengine tuyafanye lini, au ndiyo tumekwisha salimu amri kimoja?