kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Simba na Yanga walimsajili Bernard Morrison wote walikiona cha mtema kuni. Faisal anaonekana kuwa ana kipaji kama Morrison lakini hana akili timamu na hatakuwa na akili timamu hata aendako. Timu inayomshawishi Fei Toto afanye hivi anavyofanya isichekelee sana kumchukua Fei Toto, maana atawaudhi hata wao na kujutia muda na fedha zao.
Sio kwamba Fei toto ni mchezaji mzuri sana, ni mchezaji wa kawaida tu bali anachokifanya uwanjani pale Yanga kinachangiwa kwa kiasi kikubwa na kocha Nabi, wachezaji anaocheza nao na mazingira yaliyoko Yanga.
Hebu mwangalie Fei kabla hajakuja Yanga, kabla hajakuja Prof. Nabi Yanga, anapocheza timu ya taifa na anapochezea timu ya taifa ya Zanzibar ni vitu tofauti kabisa. Hata Saido alikuwa mzuri alipokuwa Yanga chini ya Prof. Nabi.
Ni Nabi tu anaejua namna ya kumtumia Fei hadi Fei akapandisha mabega na kama yuko mtu atabisha hiki ninachokisema ahifadhi huu uzi pahala pema kabisa ili aje aurejelee siku chache zijazo baada ya Fei kufanikiwa kuondoka yanga. Fei ataungana na Saido, Donald Ngoma, Obre Chirwa, Niyonzima, Frank Domayo na Morrison kwenye safari yake ya kuondoka Yanga kwa mbwembwe.