Pia kwa hoja zako hizo hizo ,nitakuswalika maswali ,Kisha utagundua hiyo ni lugha ya picha tu
Kupitia Isaya 14 na Ezekieli 28,
1. Ni lini mfalme wa Babeli alijivunia na kusema kwamba atapanda juu ya mbingu na kuwa sawa na Mungu, kama inavyosema katika Isaya 14:13-14?
2. Je, mfalme wa Babeli aliwahi kutawala au kuwa na nguvu za kushindana na Mungu kama inavyoelezwa katika Isaya 14:14, au huu ni uhusiano wa mfano na uasi wa Lucifer?
Umeuliza swali zuri ila Umekosea mwishoni Kuweka Conlusion..
Kwanza naomba Nikukumbushe Hasira ya Mungu juu ya Hao wanaowachokoza Israel..
Zekaria 2:7-8
"Haya! Ee Sayuni, jiponye, wewe ukaaye pamoja na binti Babeli.
Kwa maana Bwana wa majeshi asema hivi, Ili nitafute utukufu amenituma kwa mataifa wale waliowateka ninyi; maana yeye awagusaye ninyi aigusa mboni ya jicho langu."
Sasa naomba Niingie kwenye historia Kidogo nikufundishe Waisrael waliingiaje Utumwani Babel..
Baada ya Uzao wa Suleiman Yohayakimu (Kizazi vha 16 kutoka kwa Suleiman na Kizazi cha 17 kutoka kwa Suleiman)
Kupokonywa Utawala wake Mikono mwake Yuda Ikawekwa Chini ya mtawala wa Babel Nebukandreza wa II ambaye anaweza Kuwa Mtawala wa Babeli mwenye Kiburi ambaye anakaribia Utawala wa belsheza ambaye ndo mtawala wa Mwisho wa Babel..
Ambaye baadae waisrael walpata Ruhusa ya Kuondoka Babel kupitia kwa Mfalme Koresh wa Uajemi..
Habari za Kutekwa kwa Babel na Kuanza kutawala Nebukandreza utazipata kutoka kwenye Daniel 1-3 na Vitabu vingine kama Wafalme,Mambo ya Nyakati..
tuendelee..
Nebukandreza alipoanza Kutawala alijifnya Mtu wa Mungu sana na kujenga Urafiki na Mkuu wa Matowashi watakatifu na Akamuamuru
Ashpenaz (ambaye alikuwa mkuu wa Matowashi nchi nzima) awalete Matowashi kila sehemu na Kurecruit vijana wacha Mungu Sana kutoka pande za nchi yote na wale waliotoka kwemye Koo za Kifalme na wale wasio na makosa waliochukuliwa ni pamoja na Kina
Daniel ambaye Mkuu wa matowashi aliwabadilisha majina Daniel akamwita
Belteshaza,
Hanania akamwita Shadraka, Mishaeli/Mikaeli akamwita Meshaki, Azaria akamwita Abednego...
Kwahyi Meshaki shadrak na Abedinego hayakuwa majina Yao halisi ni majina Waliobadilishwa na Mkuu wa matowashi..
Hawa walipewa kazi moja tu Kumfundisha Mfalme kuhusu Elimu Ya Torati na Elimu zingine ili mfalme awe na elimu ajue Lugha na Ajue vingi sana bila Kujua Walipomfundisha ndo ilikuwa Fimbo yao..
Na kama Unakumbuka Kuhusu Ndoto ya Mfalme Nebukadreza na Mpaka Kudondoka kwa Sanamu maana Yake ni Ufalme wa Babel utaanguka..
Kama unafahamu Kuwa Mfalme wa Babel alitaka Kuabudiwa Kama Mungu akajipandisha Na watu ambao hawakuabudi walipewa Adhabu Kubwa Sana Ikiwemo Kuchomwa kwenye Tanuli la Moto na Hata kina daniel Kutupwa kwenye Tundu la simba Lengo lilikuwa ni kuabudu Ile sanamu aliyoiota na Kujifanannisha na Mungu...
bado Unataka Kuniuliza Kuhusu Lini Mfalme wa Babel alijiinua?
Kweli?
au Niende mpaka kwa Mfalme Belshaza ambaye yeye alitumia mpaka Vyombo Vya hekali Kunywea Pombe na akajiona yeye ndo Mungu na Kutoa maneno ya Makufuru mpaka Akaona kidole Kikiandika Mene mene Tekeli na Peresi..
Hata hayo Huyajui kama Yalikuwa Kifuru...Kweli?
basi unahitaji Kusoma Tena Biblia kwa Utuliza Babeli ilifanya mambo mengi sana ya Kujiinua na Kumtukana mungu aliye juu rudi tena Kusoma kuhusu Utawala wote wa Babeli utaelewa
3. Katika Ezekieli 28:13-15, mfalme wa Tiro anatajwa kuwa aliishi katika Edeni. Je, mfalme huyu alikuwa na uhusiano gani na Edeni? Je, alikuwa akitekeleza majukumu ya kiroho au hapa kuna picha ya uasi wa Lucifer?
4. Ni vipi mfalme wa Babeli au mfalme wa Tiro walikufuru kwa kiburi cha aina hii wakati walikuwa wanadamu wa kawaida, ikilinganishwa na hadithi ya Lucifer aliyeanguka kutoka mbinguni?
5. Kwa nini Isaya 14 na Ezekieli 28 zimetumia picha za mfalme wa Babeli na mfalme wa Tiro kuonyesha uasi na kiburi, wakati pia zinafanana sana na picha ya Lucifer katika Biblia?
Utawala wa Tiro..
Kuhusu Edeni Nimewahi kueleza Vizuri sana humu ndani Kuwa Edeni inamaana Nyingi sana Ila kinachonishangaza kuwa Umeshindwa Kujua Kuwa hata Shetani unae sema alitajwa katika Ezekieli 28:13 Kuwa alikuwa Edeni na Utukufu uliotajwa hapo Umesahau wamba Shetani
hakuwahi kuwa edeni akiwa na Utukufu huo?
Ni kwamba Umesahau au umezibwa na Utetezi wa Doctrine uliyofundishwa kuwa unataka na Unatamani iwe kweli?
Au fungu la ufunuo hukulisoma jinsi shetani alivyotupwa na al8vyofika mpaka Kudanganya??
Ufunuo wa Yohana 12:7-9
[7]Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
[8]nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
[9]Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
Unasahau hata Makerubi kwenye Bustani ya Edeni walianza kuwekwa Baada ya Adamu kufanya Dhambi na sio kabla ya Adamu kufanya dhambi..
Mwanzo 3:24
[24]Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.
Kwahyo Unataka kusema Kuwa Shetani alianguka baada ya Adamu na Eva kufanya dhambi??
Au kabla ya kufanya dhambi..
Shetani hakuwa na Utukufu uliotajwa kwenye Ezekiel 28:13 Ila alikuea na Hasira na Watu wa Mungu iliotajwa kwenye Ufunuo 12:12..
Ninataka Kuamini kuwa kuamini Doctrine ya Ezekiel 28:11-19 Kuwa mazungumzo ni Shetani utakuwa Umeteleza vinginevyo utanipa Wakati wa Kulufundisha Nini maana Ya Edeni kwa Lugha ya Kinabii...
Edeni inayozungumziwa hapo sio Edeni halisia ambayo wewe unadhani kuwa mfalme wa tiro alikuwa Edeni..
Kama nilivyokupa maana ya Key-rabiya au Cherubi nyingine ni Mtu mkamilifu au Mnyenyekevu..
Unashindwa Kuelewa kama Alikuwa Mfalme aliyepakwa mafuta alikuw Akiishi Kwa amani na Katika misinginya Furaha aliyoamuru Mungu??
Edeni maana Yake ni Sehemu kamilifu na Sehemu yenye Raha na Sehemu Hiyo inayotajwa ndiyo hasa Sehemu ambayo mfalme Anaishi kwa hyo kukaa kwenye Raha hizo kama mfalme kiburi chake kikainuka ...
Ni kama Nikisema Rais ramia kwa sasa anaishi Edeni simaanishi kwamba Samia Yupe Edeni na Adamu na Hawa..
Mkuu soma maandiko ukiwa hauko Pre-Indoctrine utaelewa maandiko mengi sana..
Nahisi hata Roho mtakatfu anashindwa kukuelekeza kwa sababu tayari unakuwa na Maana yako ya MaaNdiko unayo kichwani na akiluelekeza Unabisha huku ukiona wewe huko sahihi kuliko yeye Jaribu Kumruhusu roho mtakatifu akuelekeze Bila kuwa na PRE Doctrine..
Kuhusu Mfalme wa Tiro
Mfalme wa Tiro alikuwa na Urafiki Mkubwa sana na Suleman
Mfalme Hiramu wa Tiro na Sulemani kama Utasoma Katika 1 Wafalme 5:1-12, Hiramu, mfalme wa Tiro, alishirikiana na Sulemani katika ujenzi wa Hekalu la Yerusalemu.
Kwahyo naweza nikasema miongoni mwa waliojenga Hekalu la Sulemani Ni Hiramu Mfalme wa Tiro.. yeye Alitoa mbao za mierezi, wasafiri wa baharini, na mafundi. Ushirikiano huu ulionyesha uhusiano wa kiuchumi na kisiasa kati ya Tiro na Israeli...
Baadae Mfalme wa Tiro alibadilika na Kuwa na Kiburi Na kuanza kuwatesa waisrael ikiwa ni pamoja na Kuwaonea soma
Amosi 1:9-10, Tiro inalaumiwa kwa kuvunja agano la kindugu na kuuza watu wa Israeli kama watumwa kwa Edomu. Mungu alitoa unabii wa hukumu dhidi ya Tiro kwa uhalifu huu. Nashangaa Unabii Huo wewe Unaita Ni Shetani ndo kaandikiwa
Dhihaka ya Kuanguka kwa Yerusalemu ilimla sana Mfalme wa tiro Katika Ezekieli 26:2, Tiro ilifurahia kuanguka kwa Yerusalemu, ikiona tukio hilo kama fursa ya kunufaika kibiashara. Furaha hii ya Tiro ilimkasirisha Mungu, na unabii wa adhabu kali ulitolewa.
Namaliza nakusuburi bado uthibitishe kuhusu Lucifer