Hakuna ubishi, bila biblia, hakuna uislam. Kama ukristo ungedukua na kukopi na kupaste quran, hali ingekuwaje?

Bila biblia na ukristo, hakuna quran wala uislam. Quran na uislam vimejengwa kwenye torati ambayo ilianzia kwenye ukristo. Hadithi zake kuu kama vile uumbaji wa Adam na Hawa, ukuu wa Ibrahim kama baba wa wote, sharia, tabia na mengine vina asili kwenye torati. Najiuliza. Kama ukristo ungedukua quran, ingekuwaje?
Bila ya mtu wa kunyoosha watanzania amchomoki, you have so much time for a majority to think on this religious nonsense.

Umejifunza wapi bible imeanzwa kuandikwa kabla ya torat.

Unajua hata tofauti ya torat na biblia.

Sidhani hata kama unajua agano la kale ndio torat, wanachopishana kwenye Jews na Christianity ni uwepo wa new testament.

Kwenye kufanya ibada na culture. Jews na Islam wanafanana kushinda Christianity.

Kosher kwa Jews ndio kitu icho-icho kwa waislamu, Halal. Nyama za Jews unajuwa zinachinjwa na waisalamu. Jews hawali nyama inayochinjwa na mkristo.

Mambo ni mengi serikali, inatakiwa kuingilia kati. Watanzania hata hizi dini wanazozifuata hawazielewi.

What do you period (learn to understand things)
 
It’s just a sad society

Why would someone in his right mind want to live in a country like this.

Nchi maskini inashida kibao, you have time to split society on religious grounds.

Wewe na akili zako timamu unataka kwenda kuishi kama hii.

I don’t think I could cope kuishi na watu kama hawa.

Aargh the nonsense, hivi aina matatizo ya kutosha kuangaika na chuki za udini,

Shitty country
 
Bila ya mtu wa kunyoosha watanzania amchomoki, you have so much time for a majority to think on this religious nonsense.

Umejifunza wapi bible imeanzwa kuandikwa kabla ya torat.

Unajua hata tofauti ya torat na biblia.

Sidhani hata kama unajua agano la kale ndio torat, wanachopishana kwenye Jews na Christianity ni uwepo wa new testament.

Kwenye kufanya ibada na culture. Jews na Islam wanafanana kushinda Christianity.

Kosher kwa Jews ndio kitu icho-icho kwa waislamu, Halal. Nyama za Jews unajuwa zinachinjwa na waisalamu. Jews hawali nyama inayochinjwa na mkristo.

Mambo ni mengi serikali, inatakiwa kuingilia kati. Watanzania hata hizi dini wanazozifuata hawazielewi.

What do you period (learn to understand things)
Wewe ni muongo mkubwa

Ibada za kiyahudi tofauti na waislamu

Wayahudi: Wana ibada kama sherehe za Pasaka, Shabati, na Sikukuu nyingine ambazo ni maalum kwa utamaduni wa Kiyahudi. Katika ibada zao, kuna sheria za kutii Torah na Talmud.

Waislamu: Waislamu wana ibada kama Salah (sala), Hajj (hija), na Zakat (sadaka). Waislamu wana sheria kali za kufunga mwezi wa Ramadhani na sherehe za Kiislamu.
 
Yesu hakuwahi Kuwa Muislamu wala Mkristo..
Yesu alikuwa myahudi na Ushahidi Usio na shaka kuhusu Hilo upo wazi..

Kama Yesu dini yake ilikuwa Uyahudi wewe ukristo umeupata wapi?

Yesu alikuwa myahudi wa kabila sio dini

Hivi wewe unazijua core believe za dini ya Uyahudi?
Ili dini yako iwe Uyahudi lazima umkane Yesu

so unataka kusema Yesu alijikana mwenyewe ndio akawa muumini wa dini ya kiyahudi?

Kama Uyahudi ni dini vipi Isaka na Yakobo dini Yao ni ipi?
Maana mtoto wa Yakobo aliyeitwa Yuda na watoto wa Yuda wakaitwa Wayahudi na baadae ndio Kuna watu hilo kabila la wayahudi wakalifanya ndio dini yao

Wakristo na Wayahudi wote mmepotea
 
Wewe ni muongo mkubwa

Ibada za kiyahudi tofauti na waislamu

Wayahudi: Wana ibada kama sherehe za Pasaka, Shabati, na Sikukuu nyingine ambazo ni maalum kwa utamaduni wa Kiyahudi. Katika ibada zao, kuna sheria za kutii Torah na Talmud.

Waislamu: Waislamu wana ibada kama Salah (sala), Hajj (hija), na Zakat (sadaka). Waislamu wana sheria kali za kufunga mwezi wa Ramadhani na sherehe za Kiislamu.
Nimeongelea tamaduni zao; waislamu na Jews.

Kosher na Halal inatofauti gani.

Jew anaweza kula nyama iliyochinjwa na mkristo?

Jibu hilo kwanza, kukusaidia hawezi,

Uchinjaji ni sawa-sawa na waislamu (Kosher-Halal ni kitu kimoja).
 
Mwanamke wa kiyahudi mwenye imani kali anaweza tembea mtaani bila ya kufunika kichwa.
 
Wewe unafananisha tu, ila ni tofauti kabisa ,mm Nina marafiki wayahudi hawawezi kula nyama ya muislamu au mkristo maana haijafata Sheria zao ,

Kosher ipo hivi labda hujui kosher ni nini , ni seti ya sheria za kidini zinazotumika kwa Wayahudi ili kuongoza kula chakula kinachokubalika kisheria.

Sheria hizi zinatokana na Torah, kitabu takatifu cha Wayahudi, na zinahusisha mambo ya kuchinja wanyama, aina za vyakula vinavyokubalika, na mchanganyiko wa chakula.

Kwa mfano, nyama lazima ichinjwe kwa njia maalum inayoitwa shechita, ambapo mnyama lazima achinjwe kwa kumtaja jina la Mungu(YWHW )na kwa kutumia kisu kilichosafishwa.

Wanyama lazima wawe na magoti, vidole, na mifupa ya mguu. Vyakula vya nyama na maziwa haviwezi kuliwa pamoja (kwa mfano, haziwezi kuliwa katika mlo mmoja).

Nyama ya Kosher ni ile inayozingatia sheria hizi za kiTorah. Nyama ya wanyama kama ng'ombe, kondoo, na mbuzi inaweza kuwa kosher, lakini wanyama kama nguruwe na samaki wenye magamba ya chini ya maji hawawezi kuwa kosher.

Kwa waislamu wao Halal ni sheria za kidini katika Uislamu ambazo zinahusu aina ya chakula na vinywaji vinavyoruhusiwa.

Sheria za Halal zinatokana na Quran na Hadith (maneno na matendo ya Mtume Muhammad).

Kama Kosher, Halal pia inahusisha kuchinja wanyama kwa njia maalum, inayojulikana kama dhaka. Wanyama wanahitaji kuchinjwa kwa jina la Mungu (Allah), na mnyama lazima awe msafi.

Waislamu hawaruhusiwi kula wanyama kama nguruwe, pombe, na nyama ya mnyama aliyejifia mwenyewe.,lakini wanakula wanayama wengi ambao ni wachafu kwa mujibu wa Torah kama Ngamia, Bata , n.k

Wayahudi hawaruhusiwi kula nyama iliyochinjwa na watu wasiokuwa Wayahudi (ikiwa ni pamoja na Waislamu na Wakristo) , wewe unasema ya Mkristo tu, kwa sababu hawana uhakika kama sheria za shechita zimefuatiliwa kikamilifu.

Wayahudi lazima wajue kwamba nyama inayoliwa imechinjwa kwa njia ya Kosher. Hii inamaanisha kwamba, ingawa nyama ya Halal (iliyochinjwa na Muislamu) inaweza kufuata baadhi ya kanuni zinazofanana na Kosher, kwa Wayahudi, ni lazima kuwa na uhakika kwamba mchakato wa kuchinja umefuata sheria za Kosher., Je muislamu ametaja jina YWHW kwenye uchinjaji?

Kwa hiyo, Myahudi hawawezi kula nyama ya Muislamu au Mkristo, kwa sababu hawawezi kuthibitisha kama sheria za Kosher zimefuatwa katika kuchinja nyama hiyo.

Waislamu wao wanaruhusiwa kula nyama ya Kosher ikiwa imetolewa na Myahudi ambaye amechinja kwa mujibu wa sheria za Kosher na ikiwa mchakato wa kuchinja umefuata utaratibu wa kidini.

Quran 5:5 inawaruhusu ambapo inasema:

"Leo tumekupeni vyakula vilivyohalalishwa kwenu, na vyakula vya wale waliokubali Kitabu vimehalalishwa kwenu..."

Hii ina maana kwamba Waislamu wanaweza kula nyama iliyochinjwa na Myahudi au Muislamu, kwa sababu Kosher na Halal zote zinazingatia utaratibu wa kidini wa kuchinja.
 
Maandishi ya Torat na Quaran yote ni right to left.

Jews na Islam wote ibada zao popote walipo duniani ibada lazima zielekee Middle East.

Hujui dini wewe, ni matahiira tu mliojijaza ujinga.

Jewish na Islam kwenye culture na waislamu tofauti yao ni ndogo sana; kuliko ukristo.
 
Hoja yako imefanya nipate maswali mengi zaidi

1. Kwa nini tamaduni za kufunika kichwa zipo pia katika dini na makabila yasiyo ya Kiyahudi au Kiislamu, kama vile Wahindu, Wakristo wa Orthodox, na baadhi ya makabila barani Afrika?

2. Je, unakubaliana kwamba kufunika kichwa kwa wanawake kulikuwepo hata kabla ya dini ya Uyahudi na Uislamu, kama sehemu ya mila na heshima katika jamii mbalimbali za kale?

3. Kwa nini baadhi ya wanawake wa Kiislamu na Kiyahudi walio na imani kali hawaoni kufunika kichwa kuwa lazima, ilhali wanafuata misingi mingine ya dini yao kwa uaminifu?

4. Kwa nini wanaume wa Kiyahudi na Waislamu pia huvaa mavazi ya kichwa (kama vile kippah kwa Wayahudi na kufi kwa Waislamu), ikiwa kufunika kichwa ni jambo la kidini la wanawake tu?

5. Kama kufunika kichwa ni sababu ya msingi ya kiimani, kwa nini wanawake wa Kiyahudi na Kiislamu wenye imani kali wapo pia ambao hawafanyi hivyo na bado wanahesabika kuwa waumini wa dini zao?
 
Taahira wewe sijasoma post yako ya upuuzi.

Mimi ninawajua waislamu wanaochinja butcher za Jews,
 
Huna unachokijua mluga luga tu mwenye chuki za kidini,

Hiyo community ya Jews hiko wapi Tanzania hadi uwajue zaidi ya kuandika ujinga tu humu.

Butcher za Jews zote ulaya wachinjaji ni waislamu, kosher/halal.
 
Maandishi ya Torat na Quaran yote ni right to left.

Jews na Islam wote ibada zao popote walipo duniani ibada lazima zielekee Middle East.

Hujui dini wewe, ni matahiira tu mliojijaza ujinga.

Jewish na Islam kwenye culture na waislamu tofauti yao ni ndogo sana; kuliko ukristo.
Acha kupaniki basi ,twende taratibu Tena kwa upole tutaelewana tu

Maandishi right to left hiyo ni tabia ya lugha, si ya kiimani. Lugha ya Kiebrania (Torah) na Kiarabu (Quran) zinashirikiana historia ya kijiografia na kitamaduni, lakini hii haimaanishi kwamba Uyahudi na Uislamu ni karibu zaidi kiimani kuliko Ukristo.

Wayahudi huabudu wakiwa na mwelekeo wa Yerusalemu (Hekalu la Kale), lakini Waislamu huabudu wakiwa na mwelekeo wa Kaaba huko Makka. Japokuwa wote wanatazama Mashariki ya Kati, sababu na historia za kiibada ni tofauti kabisa.

Ukristo hauna mwelekeo maalum wa ibada kwa sababu imani ya Kikristo inalenga kuabudu "katika roho na kweli" (Yohana 4:24).

Tamaduni za Wayahudi na Waislamu huchangia baadhi ya mambo ya kihistoria na kijiografia, lakini Ukristo pia ulikuwa sehemu ya jamii ya Kiyahudi kabla ya kuenea ulimwenguni. Tofauti za kiimani (mfano: fundisho la Yesu Kristo kama Masihi) ni kubwa zaidi kati ya Uyahudi na Uislamu kuliko ukaribu wao wa kitamaduni.

Na maswali kwako

1. Je, una ushahidi kwamba mwelekeo wa ibada (kuelekea Yerusalemu au Makka) una uhusiano wa moja kwa moja wa kuonesha imani zao zinashabihiana zaidi kuliko Ukristo?

2. Kwa nini lugha ya maandishi (kulia kwenda kushoto) itafsiriwe kama kipimo cha ukaribu wa kiimani, ilhali ni tabia ya lugha tu?

3. Je, unakubaliana kwamba tofauti za kimsingi za kiimani (kama fundisho la Masihi katika Ukristo na kukosekana kwa hilo katika Uyahudi au Uislamu) ni kubwa zaidi kuliko kufanana kwa tamaduni?
 
Huna unachokijua mluga luga tu mwenye chuki za kidini,

Hiyo community ya Jews hiko wapi Tanzania hadi uwajue zaidi ya kuandika ujinga tu humu.

Butcher za Jews zote ulaya wachinjaji ni waislamu, kosher/halal.
Mbona unapaniki na maneno makali ,tatizo nini ?

kwa kawaida, nyama ya kosher inachinjwa na mashochat (wachinjaji wa Kiyahudi) walioidhinishwa na mamlaka za kidini za Kiyahudi. Hii ni kwa sababu sheria za kosher zinahitaji uchinjaji kufanywa na mtu anayefuata taratibu maalum za kidini na mwenye ujuzi wa sheria hizo.
 
Pia kwa hoja zako hizo hizo ,nitakuswalika maswali ,Kisha utagundua hiyo ni lugha ya picha tu

Kupitia Isaya 14 na Ezekieli 28,

1. Ni lini mfalme wa Babeli alijivunia na kusema kwamba atapanda juu ya mbingu na kuwa sawa na Mungu, kama inavyosema katika Isaya 14:13-14?

2. Je, mfalme wa Babeli aliwahi kutawala au kuwa na nguvu za kushindana na Mungu kama inavyoelezwa katika Isaya 14:14, au huu ni uhusiano wa mfano na uasi wa Lucifer?
Umeuliza swali zuri ila Umekosea mwishoni Kuweka Conlusion..

Kwanza naomba Nikukumbushe Hasira ya Mungu juu ya Hao wanaowachokoza Israel..

Zekaria 2:7-8
"Haya! Ee Sayuni, jiponye, wewe ukaaye pamoja na binti Babeli.

Kwa maana Bwana wa majeshi asema hivi, Ili nitafute utukufu amenituma kwa mataifa wale waliowateka ninyi; maana yeye awagusaye ninyi aigusa mboni ya jicho langu."

Sasa naomba Niingie kwenye historia Kidogo nikufundishe Waisrael waliingiaje Utumwani Babel..

Baada ya Uzao wa Suleiman Yohayakimu (Kizazi vha 16 kutoka kwa Suleiman na Kizazi cha 17 kutoka kwa Suleiman)
Kupokonywa Utawala wake Mikono mwake Yuda Ikawekwa Chini ya mtawala wa Babel Nebukandreza wa II ambaye anaweza Kuwa Mtawala wa Babeli mwenye Kiburi ambaye anakaribia Utawala wa belsheza ambaye ndo mtawala wa Mwisho wa Babel..
Ambaye baadae waisrael walpata Ruhusa ya Kuondoka Babel kupitia kwa Mfalme Koresh wa Uajemi..

Habari za Kutekwa kwa Babel na Kuanza kutawala Nebukandreza utazipata kutoka kwenye Daniel 1-3 na Vitabu vingine kama Wafalme,Mambo ya Nyakati..

tuendelee..
Nebukandreza alipoanza Kutawala alijifnya Mtu wa Mungu sana na kujenga Urafiki na Mkuu wa Matowashi watakatifu na Akamuamuru Ashpenaz (ambaye alikuwa mkuu wa Matowashi nchi nzima) awalete Matowashi kila sehemu na Kurecruit vijana wacha Mungu Sana kutoka pande za nchi yote na wale waliotoka kwemye Koo za Kifalme na wale wasio na makosa waliochukuliwa ni pamoja na Kina Daniel ambaye Mkuu wa matowashi aliwabadilisha majina Daniel akamwita Belteshaza,
Hanania akamwita Shadraka, Mishaeli/Mikaeli akamwita Meshaki, Azaria akamwita Abednego...

Kwahyi Meshaki shadrak na Abedinego hayakuwa majina Yao halisi ni majina Waliobadilishwa na Mkuu wa matowashi..

Hawa walipewa kazi moja tu Kumfundisha Mfalme kuhusu Elimu Ya Torati na Elimu zingine ili mfalme awe na elimu ajue Lugha na Ajue vingi sana bila Kujua Walipomfundisha ndo ilikuwa Fimbo yao..

Na kama Unakumbuka Kuhusu Ndoto ya Mfalme Nebukadreza na Mpaka Kudondoka kwa Sanamu maana Yake ni Ufalme wa Babel utaanguka..

Kama unafahamu Kuwa Mfalme wa Babel alitaka Kuabudiwa Kama Mungu akajipandisha Na watu ambao hawakuabudi walipewa Adhabu Kubwa Sana Ikiwemo Kuchomwa kwenye Tanuli la Moto na Hata kina daniel Kutupwa kwenye Tundu la simba Lengo lilikuwa ni kuabudu Ile sanamu aliyoiota na Kujifanannisha na Mungu...

bado Unataka Kuniuliza Kuhusu Lini Mfalme wa Babel alijiinua?
Kweli?
au Niende mpaka kwa Mfalme Belshaza ambaye yeye alitumia mpaka Vyombo Vya hekali Kunywea Pombe na akajiona yeye ndo Mungu na Kutoa maneno ya Makufuru mpaka Akaona kidole Kikiandika Mene mene Tekeli na Peresi..

Hata hayo Huyajui kama Yalikuwa Kifuru...Kweli?

basi unahitaji Kusoma Tena Biblia kwa Utuliza Babeli ilifanya mambo mengi sana ya Kujiinua na Kumtukana mungu aliye juu rudi tena Kusoma kuhusu Utawala wote wa Babeli utaelewa
3. Katika Ezekieli 28:13-15, mfalme wa Tiro anatajwa kuwa aliishi katika Edeni. Je, mfalme huyu alikuwa na uhusiano gani na Edeni? Je, alikuwa akitekeleza majukumu ya kiroho au hapa kuna picha ya uasi wa Lucifer?

4. Ni vipi mfalme wa Babeli au mfalme wa Tiro walikufuru kwa kiburi cha aina hii wakati walikuwa wanadamu wa kawaida, ikilinganishwa na hadithi ya Lucifer aliyeanguka kutoka mbinguni?

5. Kwa nini Isaya 14 na Ezekieli 28 zimetumia picha za mfalme wa Babeli na mfalme wa Tiro kuonyesha uasi na kiburi, wakati pia zinafanana sana na picha ya Lucifer katika Biblia?
Utawala wa Tiro..

Kuhusu Edeni Nimewahi kueleza Vizuri sana humu ndani Kuwa Edeni inamaana Nyingi sana Ila kinachonishangaza kuwa Umeshindwa Kujua Kuwa hata Shetani unae sema alitajwa katika Ezekieli 28:13 Kuwa alikuwa Edeni na Utukufu uliotajwa hapo Umesahau wamba Shetani hakuwahi kuwa edeni akiwa na Utukufu huo?

Ni kwamba Umesahau au umezibwa na Utetezi wa Doctrine uliyofundishwa kuwa unataka na Unatamani iwe kweli?

Au fungu la ufunuo hukulisoma jinsi shetani alivyotupwa na al8vyofika mpaka Kudanganya??

Ufunuo wa Yohana 12:7-9

[7]Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

[8]nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.

[9]Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

Unasahau hata Makerubi kwenye Bustani ya Edeni walianza kuwekwa Baada ya Adamu kufanya Dhambi na sio kabla ya Adamu kufanya dhambi..

Mwanzo 3:24
[24]Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.

Kwahyo Unataka kusema Kuwa Shetani alianguka baada ya Adamu na Eva kufanya dhambi??
Au kabla ya kufanya dhambi..

Shetani hakuwa na Utukufu uliotajwa kwenye Ezekiel 28:13 Ila alikuea na Hasira na Watu wa Mungu iliotajwa kwenye Ufunuo 12:12..

Ninataka Kuamini kuwa kuamini Doctrine ya Ezekiel 28:11-19 Kuwa mazungumzo ni Shetani utakuwa Umeteleza vinginevyo utanipa Wakati wa Kulufundisha Nini maana Ya Edeni kwa Lugha ya Kinabii...

Edeni inayozungumziwa hapo sio Edeni halisia ambayo wewe unadhani kuwa mfalme wa tiro alikuwa Edeni..
Kama nilivyokupa maana ya Key-rabiya au Cherubi nyingine ni Mtu mkamilifu au Mnyenyekevu..

Unashindwa Kuelewa kama Alikuwa Mfalme aliyepakwa mafuta alikuw Akiishi Kwa amani na Katika misinginya Furaha aliyoamuru Mungu??

Edeni maana Yake ni Sehemu kamilifu na Sehemu yenye Raha na Sehemu Hiyo inayotajwa ndiyo hasa Sehemu ambayo mfalme Anaishi kwa hyo kukaa kwenye Raha hizo kama mfalme kiburi chake kikainuka ...

Ni kama Nikisema Rais ramia kwa sasa anaishi Edeni simaanishi kwamba Samia Yupe Edeni na Adamu na Hawa..

Mkuu soma maandiko ukiwa hauko Pre-Indoctrine utaelewa maandiko mengi sana..

Nahisi hata Roho mtakatfu anashindwa kukuelekeza kwa sababu tayari unakuwa na Maana yako ya MaaNdiko unayo kichwani na akiluelekeza Unabisha huku ukiona wewe huko sahihi kuliko yeye Jaribu Kumruhusu roho mtakatifu akuelekeze Bila kuwa na PRE Doctrine..

Kuhusu Mfalme wa Tiro

Mfalme wa Tiro alikuwa na Urafiki Mkubwa sana na Suleman
Mfalme Hiramu wa Tiro na Sulemani kama Utasoma Katika 1 Wafalme 5:1-12, Hiramu, mfalme wa Tiro, alishirikiana na Sulemani katika ujenzi wa Hekalu la Yerusalemu.

Kwahyo naweza nikasema miongoni mwa waliojenga Hekalu la Sulemani Ni Hiramu Mfalme wa Tiro.. yeye Alitoa mbao za mierezi, wasafiri wa baharini, na mafundi. Ushirikiano huu ulionyesha uhusiano wa kiuchumi na kisiasa kati ya Tiro na Israeli...
Baadae Mfalme wa Tiro alibadilika na Kuwa na Kiburi Na kuanza kuwatesa waisrael ikiwa ni pamoja na Kuwaonea soma Amosi 1:9-10, Tiro inalaumiwa kwa kuvunja agano la kindugu na kuuza watu wa Israeli kama watumwa kwa Edomu. Mungu alitoa unabii wa hukumu dhidi ya Tiro kwa uhalifu huu. Nashangaa Unabii Huo wewe Unaita Ni Shetani ndo kaandikiwa

Dhihaka ya Kuanguka kwa Yerusalemu ilimla sana Mfalme wa tiro Katika Ezekieli 26:2, Tiro ilifurahia kuanguka kwa Yerusalemu, ikiona tukio hilo kama fursa ya kunufaika kibiashara. Furaha hii ya Tiro ilimkasirisha Mungu, na unabii wa adhabu kali ulitolewa.

Namaliza nakusuburi bado uthibitishe kuhusu Lucifer
 
Kama Yesu dini yake ilikuwa Uyahudi wewe ukristo umeupata wapi?

Yesu alikuwa myahudi wa kabila sio dini

Hivi wewe unazijua core believe za dini ya Uyahudi?
Ili dini yako iwe Uyahudi lazima umkane Yesu

so unataka kusema Yesu alijikana mwenyewe ndio akawa muumini wa dini ya kiyahudi?

Kama Uyahudi ni dini vipi Isaka na Yakobo dini Yao ni ipi?
Maana mtoto wa Yakobo aliyeitwa Yuda na watoto wa Yuda wakaitwa Wayahudi na baadae ndio Kuna watu hilo kabila la wayahudi wakalifanya ndio dini yao

Wakristo na Wayahudi wote mmepotea
Yesu Dini Yake ilikuwa Uyahudi, Ni kweli kwamba Yesu alizaliwa katika jamii ya Kiyahudi na alifuata baadhi ya sheria za Kiyahudi. Hata hivyo, Ukristo ulianzishwa kutokana na mafundisho yake mapya, ambayo yalijumuisha mafundisho ya kiroho na maagizo mapya (Mathayo 5:17-18). Yesu hakuja kuvunja Sheria za Musa bali kuzitimiza.

Ukristo haukuwa kinyume na Uyahudi mwanzoni, bali ulikuwa maendeleo ya mafundisho ya kiroho ya Wayahudi kupitia Yesu kama Masihi.

Uyahudi wakati wa Yesu ulikuwa unaunganisha utambulisho wa kikabila na kidini. Kwa hivyo, Yesu alikuwa Myahudi kwa kabila na alizingatia baadhi ya mila za Kiyahudi. Lakini mafundisho yake yalihusu kuanzisha agano jipya kwa watu wote, si Wayahudi pekee (Mathayo 28:19).

Ni kweli kwamba Uyahudi haukubali Yesu kama Masihi. Lakini Ukristo ulikuja kutokana na mafundisho ya Yesu, ambayo yalitambua yeye kama Masihi. Wale waliomwamini Yesu walitoka kwenye Uyahudi wa asili na kuunda Ukristo kama imani mpya.

Isaka na Yakobo hawakuwa na "dini" kama tunavyofahamu leo. Walifuata agano na Mungu wa Ibrahimu, ambalo liliendelea kuwa msingi wa Uyahudi na Ukristo. Ukristo unatokana na agano jipya lililoletwa na Yesu.

Nina maswali kwako japo hujibu hata moja

1. Kama Uyahudi ni dini inayokana Yesu, kwa nini watu wa kwanza waliomfuata Yesu (mitume wake) walikuwa Wayahudi?

2. Je, mafundisho ya Yesu kuhusu agano jipya (Mathayo 26:28) hayaonyeshi kwamba Ukristo ulitokana na maendeleo ya kiimani kutoka Uyahudi?

3. Ikiwa Isaka na Yakobo walikuwa na uhusiano wa kipekee na Mungu bila dini rasmi, kwa nini iwe vigumu kuelewa kwamba Ukristo unatokana na agano jipya lililoanzishwa na Yesu?
 
Ndugu Mimi sishangai Yesu kuitwa Nyota ya Asubuhi, Yesu kaitwa Nyoka pia pale Musa alipoinua Fimbo yenye nyoka juu ili Wana wa Israel waiangalie ,lile tukio limefananishwa na Yesu juu ya msalaba na maandiko

Ni kweli kwamba mfalme wa Babeli alikuwa na utukufu mkubwa na alijivunia utawala wake kama inavyosema Isaya 14:13-14, lakini alijivuna kwa njia ya kiburi, ambayo ndiyo ilileta uasi wake dhidi ya Mungu. Alijaribu kujilinganisha na Mungu mwenyewe na hata kutaka kiti cha Mungu, akasema: "Nitapanda juu ya nyota za Mungu, nitainua kiti changu cha enzi juu ya nyota za Mungu".

Hii ni picha ya wazi ya Lucifer (Shetani) ambaye alijivunia na akaanguka kutoka kwa utukufu wake.

Hivyo, ingawa mfalme wa Babeli alikuwa na utukufu wa kibinadamu, uasi wake ulionyesha uasi wa kiroho ulioanzia kwa Shetani, ambaye alianguka kutokana na kiburi chake.

Katika Biblia, Mungu anasema kuhusu taifa la Israeli kuwa ni watoto wake wa kwanza (Kutoka 4:22), na alijali taifa hili kwa ajili ya mpango wake wa wokovu wa ulimwengu. Hivyo, mfalme wa Babeli alipoamua kuwatesa Waisraeli, alikataa mamlaka ya Mungu na alijivunia kwa njia ya kiburi. Hii ilikuwa ni dhambi kwa Mungu, kwa sababu aliwatendea vibaya watu waliokuwa wake, na hivyo alijiletea hukumu kutokana na kumwasi Mungu.

Kujipaisha kwa Waisraeli, kwa hiyo, ilikuwa ni kiburi cha mfalme wa Babeli ambaye alijifanya kuwa bora kuliko Mungu mwenyewe, na hii ilileta adhabu kubwa kutoka kwa Mungu.

Katika Biblia, Yesu anatajwa kama "Nyota ya Asubuhi" katika Ufunuo 22:16, ambapo Yesu mwenyewe anasema: "Mimi ni mzawa na uzao wa Daudi, nyota ya asubuhi." Hii ni sehemu ya unabii ambayo inarejelea mwangaza na utukufu wa Yesu, ambaye alikuja kuleta mwanga na wokovu kwa ulimwengu. Hapa, neno "nyota ya asubuhi" linatumika kumwonyesha Yesu kama mkombozi, na sio Shetani.

Kwa hiyo, Yesu anatajwa kama "nyota ya asubuhi", lakini ni kwa maana ya mwangaza wa wokovu, si kwa maana ya Lucifer aliyeanguka kutokana na kiburi. Hii ni tofauti ya msingi kati ya Yesu na Shetani (Lucifer).

Kwa mujibu wa Luka 10:18, Yesu anasema: "Nikaona Shetani akishuka kutoka mbinguni kama umeme." Hii inadhihirisha kwamba Shetani alishuka kutoka mbinguni baada ya kumwasi Mungu, na ndiyo maana ya kutajwa kwake kuwa akishuka kutoka mbinguni kama umeme. Hata hivyo, Shetani alikuwapo mbinguni kabla ya kuasi, lakini alikataa mamlaka ya Mungu na alijivuna, na kwa hivyo alifukuzwa.

Katika Yohana 8:44, Yesu anamtaja Shetani kama "baba wa uongo", na pia anasema: "Hakuwa na ukweli ndani yake", akikiri asili yake ya uasi kutoka kwa Mungu. Shetani alijivunia kwa kiburi chake na alijaribu kumwasi Mungu, jambo ambalo lilipelekea anguko lake.
Nimewahi Kueleza Humu Kuhusu Lucifer hamjui maana Yake..
Karibu Usome na Upitie Nilichoandika..

Na Kingine Hebu Niambie Uongo wa Shetanj Mpaka kumuita Baba Wa Uongo?
 
Mbona unapaniki na maneno makali ,tatizo nini ?

kwa kawaida, nyama ya kosher inachinjwa na mashochat (wachinjaji wa Kiyahudi) walioidhinishwa na mamlaka za kidini za Kiyahudi. Hii ni kwa sababu sheria za kosher zinahitaji uchinjaji kufanywa na mtu anayefuata taratibu maalum za kidini na mwenye ujuzi wa sheria hizo.
Wewe unaandika ujinga mimi nawajua watu wanaofanya hiyo kazi kweli ambao wanachinja kweli butcher za Jews, jamaa ni muislamu na butcher wachinjaji ni waislamu.

Butcher ipo Golders Green (London), wewe unabishia ujinga. Nitakachokwambia mchinjaji mmoja ni mtanzania na muislamu.

Huna unachokijua zaidi ya ujinga tu
 
Mbona unapaniki na maneno makali ,tatizo nini ?

kwa kawaida, nyama ya kosher inachinjwa na mashochat (wachinjaji wa Kiyahudi) walioidhinishwa na mamlaka za kidini za Kiyahudi. Hii ni kwa sababu sheria za kosher zinahitaji uchinjaji kufanywa na mtu anayefuata taratibu maalum za kidini na mwenye ujuzi wa sheria hizo.
Utabisha na kwamba Synagogue zote duniani zimeelekezwa Middle East kama ilivyo misikiti.

Hizo dini zenyewe hamjui kutwa kusambaza chuki.
 
Umeuliza swali zuri ila Umekosea mwishoni Kuweka Conlusion..

Kwanza naomba Nikukumbushe Hasira ya Mungu juu ya Hao wanaowachokoza Israel..

Zekaria 2:7-8
"Haya! Ee Sayuni, jiponye, wewe ukaaye pamoja na binti Babeli.

Kwa maana Bwana wa majeshi asema hivi, Ili nitafute utukufu amenituma kwa mataifa wale waliowateka ninyi; maana yeye awagusaye ninyi aigusa mboni ya jicho langu."

Sasa naomba Niingie kwenye historia Kidogo nikufundishe Waisrael waliingiaje Utumwani Babel..

Baada ya Uzao wa Suleiman Yohayakimu (Kizazi vha 16 kutoka kwa Suleiman na Kizazi cha 17 kutoka kwa Suleiman)
Kupokonywa Utawala wake Mikono mwake Yuda Ikawekwa Chini ya mtawala wa Babel Nebukandreza wa II ambaye anaweza Kuwa Mtawala wa Babeli mwenye Kiburi ambaye anakaribia Utawala wa belsheza ambaye ndo mtawala wa Mwisho wa Babel..
Ambaye baadae waisrael walpata Ruhusa ya Kuondoka Babel kupitia kwa Mfalme Koresh wa Uajemi..

Habari za Kutekwa kwa Babel na Kuanza kutawala Nebukandreza utazipata kutoka kwenye Daniel 1-3 na Vitabu vingine kama Wafalme,Mambo ya Nyakati..

tuendelee..
Nebukandreza alipoanza Kutawala alijifnya Mtu wa Mungu sana na kujenga Urafiki na Mkuu wa Matowashi watakatifu na Akamuamuru Ashpenaz (ambaye alikuwa mkuu wa Matowashi nchi nzima) awalete Matowashi kila sehemu na Kurecruit vijana wacha Mungu Sana kutoka pande za nchi yote na wale waliotoka kwemye Koo za Kifalme na wale wasio na makosa waliochukuliwa ni pamoja na Kina Daniel ambaye Mkuu wa matowashi aliwabadilisha majina Daniel akamwita Belteshaza,
Hanania akamwita Shadraka, Mishaeli/Mikaeli akamwita Meshaki, Azaria akamwita Abednego...

Kwahyi Meshaki shadrak na Abedinego hayakuwa majina Yao halisi ni majina Waliobadilishwa na Mkuu wa matowashi..

Hawa walipewa kazi moja tu Kumfundisha Mfalme kuhusu Elimu Ya Torati na Elimu zingine ili mfalme awe na elimu ajue Lugha na Ajue vingi sana bila Kujua Walipomfundisha ndo ilikuwa Fimbo yao..

Na kama Unakumbuka Kuhusu Ndoto ya Mfalme Nebukadreza na Mpaka Kudondoka kwa Sanamu maana Yake ni Ufalme wa Babel utaanguka..

Kama unafahamu Kuwa Mfalme wa Babel alitaka Kuabudiwa Kama Mungu akajipandisha Na watu ambao hawakuabudi walipewa Adhabu Kubwa Sana Ikiwemo Kuchomwa kwenye Tanuli la Moto na Hata kina daniel Kutupwa kwenye Tundu la simba Lengo lilikuwa ni kuabudu Ile sanamu aliyoiota na Kujifanannisha na Mungu...

bado Unataka Kuniuliza Kuhusu Lini Mfalme wa Babel alijiinua?
Kweli?
au Niende mpaka kwa Mfalme Belshaza ambaye yeye alitumia mpaka Vyombo Vya hekali Kunywea Pombe na akajiona yeye ndo Mungu na Kutoa maneno ya Makufuru mpaka Akaona kidole Kikiandika Mene mene Tekeli na Peresi..

Hata hayo Huyajui kama Yalikuwa Kifuru...Kweli?

basi unahitaji Kusoma Tena Biblia kwa Utuliza Babeli ilifanya mambo mengi sana ya Kujiinua na Kumtukana mungu aliye juu rudi tena Kusoma kuhusu Utawala wote wa Babeli utaelewa

Utawala wa Tiro..

Kuhusu Edeni Nimewahi kueleza Vizuri sana humu ndani Kuwa Edeni inamaana Nyingi sana Ila kinachonishangaza kuwa Umeshindwa Kujua Kuwa hata Shetani unae sema alitajwa katika Ezekieli 28:13 Kuwa alikuwa Edeni na Utukufu uliotajwa hapo Umesahau wamba Shetani hakuwahi kuwa edeni akiwa na Utukufu huo?

Ni kwamba Umesahau au umezibwa na Utetezi wa Doctrine uliyofundishwa kuwa unataka na Unatamani iwe kweli?

Au fungu la ufunuo hukulisoma jinsi shetani alivyotupwa na al8vyofika mpaka Kudanganya??

Ufunuo wa Yohana 12:7-9

[7]Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

[8]nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.

[9]Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

Unasahau hata Makerubi kwenye Bustani ya Edeni walianza kuwekwa Baada ya Adamu kufanya Dhambi na sio kabla ya Adamu kufanya dhambi..

Mwanzo 3:24
[24]Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.

Kwahyo Unataka kusema Kuwa Shetani alianguka baada ya Adamu na Eva kufanya dhambi??
Au kabla ya kufanya dhambi..

Shetani hakuwa na Utukufu uliotajwa kwenye Ezekiel 28:13 Ila alikuea na Hasira na Watu wa Mungu iliotajwa kwenye Ufunuo 12:12..

Ninataka Kuamini kuwa kuamini Doctrine ya Ezekiel 28:11-19 Kuwa mazungumzo ni Shetani utakuwa Umeteleza vinginevyo utanipa Wakati wa Kulufundisha Nini maana Ya Edeni kwa Lugha ya Kinabii...

Edeni inayozungumziwa hapo sio Edeni halisia ambayo wewe unadhani kuwa mfalme wa tiro alikuwa Edeni..
Kama nilivyokupa maana ya Key-rabiya au Cherubi nyingine ni Mtu mkamilifu au Mnyenyekevu..

Unashindwa Kuelewa kama Alikuwa Mfalme aliyepakwa mafuta alikuw Akiishi Kwa amani na Katika misinginya Furaha aliyoamuru Mungu??

Edeni maana Yake ni Sehemu kamilifu na Sehemu yenye Raha na Sehemu Hiyo inayotajwa ndiyo hasa Sehemu ambayo mfalme Anaishi kwa hyo kukaa kwenye Raha hizo kama mfalme kiburi chake kikainuka ...

Ni kama Nikisema Rais ramia kwa sasa anaishi Edeni simaanishi kwamba Samia Yupe Edeni na Adamu na Hawa..

Mkuu soma maandiko ukiwa hauko Pre-Indoctrine utaelewa maandiko mengi sana..

Nahisi hata Roho mtakatfu anashindwa kukuelekeza kwa sababu tayari unakuwa na Maana yako ya MaaNdiko unayo kichwani na akiluelekeza Unabisha huku ukiona wewe huko sahihi kuliko yeye Jaribu Kumruhusu roho mtakatifu akuelekeze Bila kuwa na PRE Doctrine..

Kuhusu Mfalme wa Tiro

Mfalme wa Tiro alikuwa na Urafiki Mkubwa sana na Suleman
Mfalme Hiramu wa Tiro na Sulemani kama Utasoma Katika 1 Wafalme 5:1-12, Hiramu, mfalme wa Tiro, alishirikiana na Sulemani katika ujenzi wa Hekalu la Yerusalemu.

Kwahyo naweza nikasema miongoni mwa waliojenga Hekalu la Sulemani Ni Hiramu Mfalme wa Tiro.. yeye Alitoa mbao za mierezi, wasafiri wa baharini, na mafundi. Ushirikiano huu ulionyesha uhusiano wa kiuchumi na kisiasa kati ya Tiro na Israeli...
Baadae Mfalme wa Tiro alibadilika na Kuwa na Kiburi Na kuanza kuwatesa waisrael ikiwa ni pamoja na Kuwaonea soma Amosi 1:9-10, Tiro inalaumiwa kwa kuvunja agano la kindugu na kuuza watu wa Israeli kama watumwa kwa Edomu. Mungu alitoa unabii wa hukumu dhidi ya Tiro kwa uhalifu huu. Nashangaa Unabii Huo wewe Unaita Ni Shetani ndo kaandikiwa

Dhihaka ya Kuanguka kwa Yerusalemu ilimla sana Mfalme wa tiro Katika Ezekieli 26:2, Tiro ilifurahia kuanguka kwa Yerusalemu, ikiona tukio hilo kama fursa ya kunufaika kibiashara. Furaha hii ya Tiro ilimkasirisha Mungu, na unabii wa adhabu kali ulitolewa.

Namaliza nakusuburi bado uthibitishe kuhusu Lucifer
Sipo hapa kutetea Doctrine,Mimi nimtu huru ninaye challenge mafundisho mbalimbali,Mimi sifungwi na dhehebu au dini ,na hii kupenda ku challenge ndio kulinifanya nitoke kwenye uislamu maana walikuwa wanakosa majibu

Hoja zako ni nzuri sana na zimekaa kimafundisho haya ya kiyahudi

Hoja kuhusu Mfalme wa Babeli na Tiro zinaweza kuwa za kweli kihistoria, lakini unabii wa Isaya 14 na Ezekieli 28 mara nyingi huchukuliwa kuwa na maana mbili (dual prophecy),zinalenga wafalme wa wakati huo, lakini pia zinaashiria tabia za Shetani. Kulinganisha kiburi cha wafalme hawa na kuanguka kwa Shetani ni dhana inayojadiliwa sana, na msingi wake uko kwenye mifano ya kiroho.

Neno "Lucifer" lina maana ya "nyota ya asubuhi" na lilipewa Shetani baada ya kuanguka kwake kwa sababu ya kiburi (Ezekieli 28:17). Ingawa halihusiani moja kwa moja na mfalme wa Babeli au Tiro, linaelezea hali ya kiroho ya kujiinua juu ya Mungu.

Edeni katika Ezekieli 28:13 inaweza kueleweka kama sehemu halisi au mfano wa neema ya kiroho aliyokuwa nayo Shetani kabla ya anguko lake. Wakati wa Adamu na Hawa, Shetani alikuwa tayari ameanguka na akatumia nafasi hiyo kumshawishi mwanadamu.

Tafsiri ya Biblia inategemea muktadha wa maandiko yote, si sehemu moja tu. Mwelekeo wa maandiko unaonyesha kuwa tabia za kiburi na dhambi zilizoonyeshwa na wafalme wa Babeli na Tiro ni vivuli vya tabia ya Shetani.

Na kwa maelezo yako ndio unazidi kuzalisha maswali mengi kichwani mwangu ,

1. Kama Mfalme wa Babeli na Tiro walikuwa wanajulikana kwa dhambi zao, kwa nini maandiko katika Isaya 14 na Ezekieli 28 yanatumia lugha inayoonyesha zaidi ya wanadamu wa kawaida (k.m., "ulikuwa Edeni" na "uliangushwa kutoka mbinguni")?

2. Je, inawezekanaje "mfalme wa Tiro" aliyeishi duniani kuwa Edeni, wakati maandiko yanaonyesha Edeni kuwa sehemu maalum ya mwanzo wa mwanadamu?

3. Kama Ezekieli 28:13 inamaanisha utawala wa mwanadamu, kwa nini inasisitiza maelezo yasiyo ya kawaida kama vile "uliwekwa jiwe la thamani"? Je, hii haiashirii viwango vya kiroho?

4. Ikiwa Lucifer haimaanishi Shetani, kwa nini tafsiri za kale za Kiebrania, Kilatini, na hata Kikristo zinaeleza neno hilo kama kiburi cha Shetani kabla ya anguko lake?

5. Je, kwa kuwa kiburi na dhambi ya Shetani zilikuwepo kabla ya wanadamu, unaweza kueleza ulinganifu kati ya tabia za Shetani na zile za wafalme wa Babeli na Tiro bila kumhusisha Shetani moja kwa moja?
 
Ufunuo 12:7÷10&12 unaielewaje?
Fungu lako Ni hili hapa..

Ufunuo wa Yohana 12:7-10, 12
7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.

9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku."

12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.

Andiko Lako nalijua sasa nataka Unijibu maswali yangu machache kabla Sijakujibu Mimi..

  1. Shetani aliasi Baada ya Binadamu Kuumbwa au kabla ya Binadamu Kuumbwa?
  2. Binadamu aliumbwa mbinguni akawekwa Ardhini chini au aliumbwa ardhini akawekwa Kwenye edeni ambayo iko mahali?
  3. Shetani alikuwa na Malaika wake? Maana alikuwa na Nguvu sawa na Mungu?
  4. Baada ya Adamu kufukuzwa Edeni alipelekwa Wapi
  5. Na Shetani alifanya kosa gani akafukuzwa Mbinguni
 
Back
Top Bottom