Hakuna Wakili anayedharaulika Tanzania nzima kama Alex Mgongolwa

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Hakuna Wakili anayedharaulika Tanzania nzima kama Alex Mgongolwa (Mkuu wa Jopo la Mawakili) wa hovyo hovyo waliojitutumua Kupambana na Wakili Msomi Mmoja tu Raia wa Ghana huko CAS Bernard Morrison na leo Kawaumbua.

Kuna Wakili Msomi Mmoja (tena Mwandamizi tu) aliwahi kunipa Takwimu za Kesi alizoshinda Wakili wa hovyo hovyo Alex Mgongolwa ambapo alisema ameshinda Kesi 1 tu kati ya Kesi 133 alizowahi Kukabiliana nazo.

Nilijiuliza Maswali mengi sana pale niliposikia Yanga SC wakimtumia huyu katika Rufaa yao dhidi ya Kesi yao kwa Wakili Msomi wa Ghana Bernard Morrison na huku wakimpamba kila Kona na Yeye pia 'akijimwambafai' katika Vyombo vya Habari mbalimbali nchini Tanzania kuwa Yanga SC watashinda.

KEROZENE najua Tanzania Mawakili Wasomi na Werevu (Intelligent) hasa wapo Wengi (lakini siyo Alex Mgongolwa) ila Kwangu Mimi hawa Wafuatao ndiyo nawaheshimu na nawakubali japo kuna wengine wameshatangulia tayari mbele za Haki....

1. Mzee Nimrod Mkono
2. Masumbuko Lamwai
3. Marehemu Mzee Kapinga
4. Mabere Marando
5. Peter Kibatala
6. Jebra Kamboole
7. Bernard Morrison

Leo mtanikoma hakyanani mvumilie tu!!
 
kwa kukuthibitishia tu ni kwamba, Mgongolwa ni wakili mzuri kuliko hao vijana kina kibatala. na kati ya wooote uliowataja hapo, marando tu ndio namkubali, wengine wote haman kitu.

kwa criminal hapa dsm, mgongolwa na Magafu ndio mawakili thabiti ambao hata kesi ya kina mbowe wangepewa wangeshinda. sema labda kwasababu huwa hawapendi mambo ya kisiasa, but kwa criminal wana uwezo na uzoefu mkubwa sana.

Mgongolwa pia amejiimarisha tangu zamani sana na kapiga sana hela za barrick, pesa anayo.
 
popoma unatisha watu ushubwada kachunge mbuzi kwenu
 
Jiulize kitu hiki kwa makini,kama kesi hii ilikuwa ni straight forward kuwa huyo morrison ana haki,wangejibu mapema,lakini kwanini walikuwa wanaahirisha?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Ongea kwa takwimu tafadhali. Ameshinda kesi ngapi?
 
Kwaiyo kila wakili anaesimamia kesi imeandikwa ni lazima ashinde iyo kesi?

Ata uliowataja awajawai kushindwa kesi? Kesi ni sawa na matokeo ya mpira uwanjani kuna kushinda na kushindwa ivyo akuna anaekwenda mahakamani ili akashindwe kilichotokea akiwezi kumuondolea usmart mgongolwa wala akiwezi kumshushia heshima yake aliyoijenga miaka mingi kwa sisi tunaomuelewa, mambo ya kisheria yana njia zake sio siasa ile ya ushabiki maandazi uliyonayo wewe, endelea kupayuka humu jf ukichoka utakaa kimya
 
ID nyingine ya GENTAMYCINE
 
Nashangaa anamtaja kibatala Kama wakili mzuri wakati kibatala ni Media Lawyer,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila wakili ni mzuri kulingana na Angle yake, hakuna wakili ambae anashinda Kila kesi. Elewa TU kwamba mawakili hawalinganishwi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaendelea kuwapiga za uso Utopolo/Vyura FC. Na kweli watakukoma leo.😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…