Ndio maana kanisani ni kuamini tu , mnakosea sana kudai imani zenu ni kweli na hakika nnje na huko makanisani na misikitiniImani si kubishana, imani ni kuamini kile unacho kiamini.
Na huwa nawashangaa sana waislamu wanaojadiliana na hawa watu wanaojiita Walokole 🤔Waislamu wanaonewa sana humu. Wanatupiwa kashfa na matusi ya nguoni. Watu hawajui jinsi ya kufanya midahalo yenye afya.
Naamini ipo siku atatokea muislamu mmoja humu mwenye uelewa mpana na ataweka kila linalotakiwa sawa.
Imani ni suala la faragha, la binafsi.Mwanzoni kulikuwa na utaratibu mzuri kabisa! Kulikuwa na jukwaa la dini na si kila mtu aliruhusiwa kuingia huko! Hii ilisaidia kwa kiwango kikubwa kiwadhibiti hawa wapuuzi
Dini ni imani na ni jambo la kiroho lisilohitaji ithibati za kibinadamu
Dini jambo binafsi na kila mtu ana sababu zake za kuamini katika dini fulani
Dini ni njia ya mwanadamu ya kumtafuta Mungu asiyeonekana kwa macho ya nyama
Dini ni tokeo la kibinadamu kutafuta asili yake, chanzo chake, uhalisia wake wa jana leo na kesho
Kama watu wasivyofanana dini haziwezi kamwe kufanana
Kama ilivyo tofauti kwenye mambo mengi dini nazo zina tofauti zake
Kama mwanadamu asivyo mkamilifu, chochote kinachozalishwa naye si kikamilifu
Haitakaa itokee dunia nzima iwe na dini moja
Wewe amini unachoamini nami niache niamini ninachoamini
Elimu yako kwenye dini yako ni ya kuungaunga uliyofundishwa na wakufunzi wa kuungaunga, kutoka kwenye vitabu vilivyotokana na asili na tamaduni za wengine! Vena kukaa kimya
Bhavaghita waachie Wakrishna na ukiwa na lolote waone wao.. Maana ndio wenye msahafu wao
Biblia waachie wakristo wenyewe.. Hata kama ni malumbano waache walumbane wenyewe
Sutra waachie Mabudha maana wanaijua kuliko wewe.. Wanashinda nayo wanalala nayo
Quran vilevile.. Hakuna mjuzi wa Quran isipokuwa Muislam mwenyewe
Wenye imani zingine zikiwemo za asili na hata waabudu shetani.. Wapewe heshima yao
Kimbelenyuma kwenye imani za wengine ni ushamba, ni ujuha ni upuuzi kama upuuzi mwingine!
Huwezi kuyajua in deep ya w
Nyumba fulani kuliko wenye nyumba wenyewe!
Dini zenyewe zinazowafanya muwakashifu watu si zenyu wala hamna ufahamu za kutosha kuzijua.. Hata ukiulizwa undani wa dini yako utaishia kujibu yale uliyokaririshwa na si vinginevyo
Usitumie nguvu nyingi mpaka povu linakutoka mdomoni kutaka kuthibitisha kitu kisicho na ithibati za kisayansi
Amini unachoamini nami niache niamini ninachoamini.. Nitakuacha na mapungufu ya dini yako na ya kwangu niachie mwenyewe
Hakuna vita ya kidini iliwahi shinda.. Kinachoshinda siku zote ni ukimyaView attachment 3532754
Kila dini ina doctrine zakeWaislamu wanaonewa sana humu. Wanatupiwa kashfa na matusi ya nguoni. Watu hawajui jinsi ya kufanya midahalo yenye afya.
Naamini ipo siku atatokea muislamu mmoja humu mwenye uelewa mpana na ataweka kila linalotakiwa sawa.
Imani ibaki kuwa jambo la faragha na binafsi Sana bila kujali nani anaamini nini.. Kina kitu kaandika Kiranga hebu kipitieIla imeandikwa mahali hivi, kwenye kitabu chao kinasema;
Nyinyi mna dini yenu na mimi nina Dini yangu:
Siabudu mnaye mwabudu
Wala
Hamwabudu ninaye mwabudu:
Ingeishia hapa hakungekuwa na shida:
Kinachotokea sasa:
Haohao wanaosema hawaabudu tunaye mwabudu:
Wanageuka na kusema
"Tunamwabudu huyo huyo mnaye mwabudu nyinyi:
Sisi tunajitahidi sana kukubali walicho ambiwa na mtume wao ila wao hawakubali kabisa:
Na tumejitahidi kuwasisitiza waelewa mtume wao alivyo waambia na hawakubali kabisa:
Wanasisiza sana na kusema
Huyohuyo Mungu wenu Yehova na pengine anajiita jina lake NIKO AMBAYE NIKO ndio huyo tunaye mwabudu na sisi
Wanamtupa pembeni kabisa mungu wao Allah ambaye sisi hatumjui na wala hakuwahi kujitambulisha kwa Manabii wetu:
Sasa Profesa Mshana Jr
Unatushaulije hapo ?
Waulizeni kwanini wanaamini hivyo, halafu mjadili, sio kurushiana matusi tu.Ila imeandikwa mahali hivi, kwenye kitabu chao kinasema;
Nyinyi mna dini yenu na mimi nina Dini yangu:
Siabudu mnaye mwabudu
Wala
Hamwabudu ninaye mwabudu:
Ingeishia hapa hakungekuwa na shida:
Kinachotokea sasa:
Haohao wanaosema hawaabudu tunaye mwabudu:
Wanageuka na kusema
"Tunamwabudu huyo huyo mnaye mwabudu nyinyi:
Sisi tunajitahidi sana kukubali walicho ambiwa na mtume wao ila wao hawakubali kabisa:
Na tumejitahidi kuwasisitiza waelewa mtume wao alivyo waambia na hawakubali kabisa:
Wanasisiza sana na kusema
Huyohuyo Mungu wenu Yehova na pengine anajiita jina lake NIKO AMBAYE NIKO ndio huyo tunaye mwabudu na sisi
Wanamtupa pembeni kabisa mungu wao Allah, ambaye sisi hatumjui na wala hakuwahi kujitambulisha kwa Manabii wetu:
Sasa Profesa Mshana Jr
Unatushaulije hapo ?
Limekuja kama mjadala wa wote ndio maana pamoja na kuwa nami nina imani yangu lakini sikutaka kuisemea kuepuka mgongano wa kimaslahi kwenye andishi na mjadala huruImani ni suala la faragha, la binafsi.
Lina wakfu wake wa faragha, wa kuachwa liwe la binafsi. Hili ni suala la haki ya kikatiba, haki ya kibinadamu kuanzia December 8 1948 kwenye Universal Declaration of Human Rights.
Ndiyo maana ukiwa nyumbani kwako unasali, ukiwa msikitini, ukiwa kanisani, akija mtu kukusumbua huko, huyo tutamsema kuwa kakuvunjia faragha yako, tutamkemea, tutamsema kwa kukuvunjia haki yako ya kikatiba na kibinadamu.
Ila.
Ukileta suala la imani hapa JF, au ukishiriki kujadili mada ya dini hapa, hapa public square, umeshaliondolea suala hilo la dini wakfu wa faragha ya jambo la binafsi.
Umelifanya kuwa mjadala katika public square.
Umeliacha liwe suala la kuhojiwa, kujadiliwa, kudhihakiwa, kugonganishwa na dini nyingine.
Kwa sababu umelichukua suala la wakfu wa faragha ya kuwa la binafsi na kulifanya liwe jambo la kujadiliwa na umma.