Hakuna watu wa ovyo kama wakosoa imani za wengine hapa JF

Hakuna watu wa ovyo kama wakosoa imani za wengine hapa JF

Nakikumbuka vizuri sana. Walikua wakjiitwa wasabato masalia

Hoja yangu kwa kisai ilikua yeye asifikiri kwenye uislam hakuna uongo. Watu wanaongopewa.
Pastor Tony kapola anawaambia waumini wake alipuliza gesi ikajaa, mtu wa akili timamu anaona kabisa huu ni uongo.
Inaitwa the opium of religion...mass hallucinations.! Taiwan ni taifa la wabuddhist.. Hiyo imani imewakolea mpaka kuna wakati wanapitiliza
Kuna sanamu (statue) Mona kubwa sana katikati ya mji.. Sass kila mwaka kuna sherehe za kwenda kuishangaa ikigeuka
In fact ile sanamu ya Budha haigeuki ila kulinganq na urefu wake kwenda juu zaidi ya mita 20 ukiiangalia utadhani inageuka !!! minds tricks
 
Mwanzoni kulikuwa na utaratibu mzuri kabisa! Kulikuwa na jukwaa la dini na si kila mtu aliruhusiwa kuingia huko! Hii ilisaidia kwa kiwango kikubwa kiwadhibiti hawa wapuuzi

Dini ni imani na ni jambo la kiroho lisilohitaji ithibati za kibinadamu
Dini jambo binafsi na kila mtu ana sababu zake za kuamini katika dini fulani
Dini ni njia ya mwanadamu ya kumtafuta Mungu asiyeonekana kwa macho ya nyama
Dini ni tokeo la kibinadamu kutafuta asili yake, chanzo chake, uhalisia wake wa jana leo na kesho

Kama watu wasivyofanana dini haziwezi kamwe kufanana
Kama ilivyo tofauti kwenye mambo mengi dini nazo zina tofauti zake
Kama mwanadamu asivyo mkamilifu, chochote kinachozalishwa naye si kikamilifu
Haitakaa itokee dunia nzima iwe na dini moja

Wewe amini unachoamini nami niache niamini ninachoamini
Elimu yako kwenye dini yako ni ya kuungaunga uliyofundishwa na wakufunzi wa kuungaunga, kutoka kwenye vitabu vilivyotokana na asili na tamaduni za wengine! Vena kukaa kimya

Bhavaghita waachie Wakrishna na ukiwa na lolote waone wao.. Maana ndio wenye msahafu wao

Biblia waachie wakristo wenyewe.. Hata kama ni malumbano waache walumbane wenyewe

Sutra waachie Mabudha maana wanaijua kuliko wewe.. Wanashinda nayo wanalala nayo
Quran vilevile.. Hakuna mjuzi wa Quran isipokuwa Muislam mwenyewe

Wenye imani zingine zikiwemo za asili na hata waabudu shetani.. Wapewe heshima yao
Kimbelenyuma kwenye imani za wengine ni ushamba, ni ujuha ni upuuzi kama upuuzi mwingine!

Huwezi kuyajua in deep ya w
Nyumba fulani kuliko wenye nyumba wenyewe!

Dini zenyewe zinazowafanya muwakashifu watu si zenyu wala hamna ufahamu za kutosha kuzijua.. Hata ukiulizwa undani wa dini yako utaishia kujibu yale uliyokaririshwa na si vinginevyo
Usitumie nguvu nyingi mpaka povu linakutoka mdomoni kutaka kuthibitisha kitu kisicho na ithibati za kisayansi

Amini unachoamini nami niache niamini ninachoamini.. Nitakuacha na mapungufu ya dini yako na ya kwangu niachie mwenyewe

Hakuna vita ya kidini iliwahi shinda.. Kinachoshinda siku zote ni ukimyaView attachment 3532754
Asante kwa picha
 
Yah ilibidi wakristo wapeleke watu kuisoma Quran ,vitabu vya Hadith vikatafsiriwa

Waislamu wakazidiwa wakaweka mpira kwapani, mihadhara ikapigwa marufuku enzi za JK, imerudi juzi juzi

Nakumbuka tukiwa Mlandizi ,tuliwapelekea moto waislamu,

Tukiwabatiza ,wakaenda kuleta polisi wakaja na defender

Awali Hawa jamaa walikuwa waisoma biblia kwa njia hasi, halafu wakristo hawawezi kuisoma Quran maana ni kiarabu hata vitabu vya Hadith ilikuwa kiarabu

Mpaka Leo wanawalaani waliotafsiri Quran hasa Baruan kwa kiswahili, walikuwa wanazinunua ili zipotee ,vitabu vya Hadith navyo hivo hivo


Kwasasa ngoma ishakuwa ngumu kwao maana kama Hadith tunazo kwa kiswahili , Quran tunayo ya Farsy, Baruani n.k
kuna wanamihadhara wa kiislam walizunguka nchi nzima kuukashifu ukristo, kana ustaadh mazinge, ustaadh kinyogoli na wenzao wengi, walikuwa wakizidiwa wanaleta fujo na mhadhara wao unaishia hapohapo. Ilifika muda mihahadhara ikafungiwa na serikali
 
Ile mihadhara waliyoianzisha wao wenyewe dhidi ya ukristo ingeendelea wangejimaliza wenyewe na dini yao kufutika katika tanganyika. Wakristo walifunuliwa vioja vya quran, ilikuwa ni kucheja tu mwanzo mwisho katika ile mihadhara ya kiislam kutaka kuudhalilisha ukristo ikaishia uislam kudhalilika! Wasoma quran wa kikristo waliidadavua quran ikabaki uchi na kuonekana ni kituko
 
wanaokwenda kuangamia hapa ni Christians wa tanzagiza hao ndiyo wakuuhurumia kwa maana wanajaribu kuwa fair lkn wasichokijua ni kwamba muslims wako vitani na wala hawaioni dunia jinsi Christians na watu wengine normal jinsi wanavyoiona, na wamekuwa wakijipanga for total take over tangia uhuru, wanakaribia ushindi, mtakuja kushangaa hamtakuja kupata raisi Christian tena na soon tutakuwa kama nigeria, wameshabadilisha mambo mengi sana mengi hamyaoni, ndani ya miaka 4 kuanzia ku-inflate number of muslims na de-flate number of Christians sasa hivi officially Christians < 50% ambapo siku zote ilikuwa ni >65% , na hii ni ndani ya miaka 4 tu, wameiingiza nchi kwenye islamic banking ambapo ni moja kati ya hatua za awali za kuingiza tanzagiza oic (organization of islamic cooperatrion) bila kuwauliza Christians kama wanataka kuwa na islamic banking, wameleta sharia banking bila ya rizaa ya Christians na wengineo, uwekezaji wote wa rasilimali umekwenda kwa muslims na mengineyo.

mlishajiuliza kwa nini raisi wa tanzagiza amekataa kuwatakia Christians heri ya Christmas, hata ya kuzuga tu?
the game is rigged, endeleeni kulala na kuongelea fairness ...


1769119079037.png
 
Imani ni suala la faragha, la binafsi.

Lina wakfu wake wa faragha, wa kuachwa liwe la binafsi. Hili ni suala la haki ya kikatiba, haki ya kibinadamu kuanzia December 8 1948 kwenye Universal Declaration of Human Rights.

Ndiyo maana ukiwa nyumbani kwako unasali, ukiwa msikitini, ukiwa kanisani, akija mtu kukusumbua huko, huyo tutamsema kuwa kakuvunjia faragha yako, tutamkemea, tutamsema kwa kukuvunjia haki yako ya kikatiba na kibinadamu.

Ila.

Ukileta suala la imani hapa JF, au ukishiriki kujadili mada ya dini hapa, hapa public square, umeshaliondolea suala hilo la dini wakfu wa faragha ya jambo la binafsi.

Umelifanya kuwa mjadala katika public square.

Umeliacha liwe suala la kuhojiwa, kujadiliwa, kudhihakiwa, kugonganishwa na dini nyingine.

Kwa sababu umelichukua suala la wakfu wa faragha ya kuwa la binafsi na kulifanya liwe jambo la kujadiliwa na umma.
Umeeleza vizuri sana
 
Wakiristo ndio huwa wanapoteza mida yao kuuelezea Uislam vibaya na hata kumkashifu Mtume wetu (S.A.W) na hata Mwenyezi Mungu....na ati wajifanya kuijua dini kutuzidi😂😂😂
 
kuna wanamihadhara wa kiislam walizunguka nchi nzima kuukashifu ukristo, kana ustaadh mazinge, ustaadh kinyogoli na wenzao wengi, walikuwa wakizidiwa wanaleta fujo na mhadhara wao unaishia hapohapo. Ilifika muda mihahadhara ikafungiwa na serikali
Hawa watoto wa juzi hawajui haya
 
Ukiona mtu kashikilia sana dini basi tambua kuwa amechanganyikiwa kupitiza, na anahitaji msaada mkubwa, na mirembe ndipo panapomfaa, na siyo lazima umsaidie.
 
Back
Top Bottom