Hakuna watu wa ovyo kama wakosoa imani za wengine hapa JF

Hakuna watu wa ovyo kama wakosoa imani za wengine hapa JF

Ikija huku kwenye jukwaa huru lazima tuhoji ,humu hakuna ulinzi wa kiimani.
HISTORIA YA KANISA LA KILUTHERI (LUTHERAN / KKKT)

1. CHIMBUKO LA KANISA LA KILUTHERI (ULAYA – KARNE YA 16).

Kanisa la Kilutheri lilianza karne ya 16 (mwaka 1517).

Mwanzilishi wake alikuwa Martin Luther, Mjerumani.

Martin Luther alikuwa padri wa Kanisa Katoliki.

Aliona mafundisho mengi hayakuwa sawa na Biblia.

Mojawapo lilikuwa kuuza msamaha wa dhambi (indulgences).

Alisisitiza wokovu hupatikana kwa imani, si kwa matendo.

Aliandika hoja 95 (95 Theses).

Alizibandika kwenye mlango wa kanisa Wittenberg.

Lengo lake halikuwa kuanzisha dhehebu jipya mwanzoni.

Hii ilisababisha kile kinachoitwa Mageuzi ya Kanisa (Reformation).

Warumi 1:17 – “Mwenye haki ataishi kwa imani.”

2. MISINGI YA MAFUNDISHO YA KILUTHERI
Biblia pekee (Sola Scriptura) msingi wa mafundisho.

Imani pekee (Sola Fide) huleta wokovu.

Neema pekee (Sola Gratia), si matendo.

Yesu Kristo ndiye mpatanishi pekee.

Hakuna maombezi ya watakatifu.

Wanakubali ubatizo wa maji.

Wanakubali Meza ya Bwana kwa ratiba

Wanakubali utatu wa Mungu.

Wanatumia Agano la Kale na Jipya.

Wanasisitiza mahubiri na mafundisho ya Biblia.

3. KUJITENGA NA KANISA KATOLIKI
Martin Luther alikataa mamlaka ya Papa.

Alikataa mapokeo yasiyoandikwa kwenye Biblia.

Alifukuzwa (excommunicated) mwaka 1521.

Wafuasi wake waliitwa Walutheri.

Kanisa la Kilutheri likajitegemea.

Likaanza Ujerumani, Skandinavia, na Ulaya Kaskazini.

Tafsiri ya Biblia kwa lugha za watu ilipewa kipaumbele.

Ibada zilianza kufanywa kwa lugha za watu.

Makanisa yaliondoa baadhi ya desturi za Kikatoliki.

Lakini walihifadhi baadhi ya muundo wa ibada.

4. KANISA LA KILUTHERI KUINGIA AFRIKA
Karne ya 19 wamisionari kutoka Ulaya.

Walitoka Ujerumani na Skandinavia.

Walikuja kwa lengo la kuhubiri Injili.

Pia walileta elimu na huduma za afya.

Walitafsiri Biblia kwa lugha za Kiafrika.

Walijenga shule na hospitali.

Walifundisha kusoma na kuandika.

Walibatiza waumini wapya.

Kanisa likaanza kukua Afrika Mashariki.

Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi muhimu.

5. KUINGIA TANZANIA (WAKATI WA UKOLONI)

Kilianza karne ya 19 na 20.

Wamisionari Wajerumani walifika Tanganyika.

Maeneo ya kwanza: Kilimanjaro, Arusha, Mbulu.

Kabila la Wachagga lilikuwa miongoni mwa wa kwanza.

Shule za misheni zilianzishwa.

Hospitali za misheni zilijengwa.

Lugha ya Kiswahili ilitumika kufundishia.

Waafrika walianza kufundishwa kuwa wachungaji.

Kanisa likajitegemea polepole.

Likaenea nchi nzima.

6. KUZALIWA KWA KKKT (1963)

Mwaka 1963 makanisa ya Kilutheri yaliungana.

Yakaunda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

KKKT si dhehebu jipya bali umoja wa majimbo.

Linaongozwa na Askofu Mkuu.

Lina dayosisi nyingi nchini.

Linatambuliwa kisheria Tanzania.

Lina katiba na kanuni zake.

Linaendesha shule, vyuo, hospitali.

Lina waumini mamilioni.

Ni moja ya makanisa makubwa Tanzania.

7. MUUNDO NA UTARATIBU WA IBADA.

Ibada huwa na liturujia (mpangilio maalum).

Mahubiri ni sehemu kuu.

Nyimbo hutumika sana.

Wanatumia ala za muziki.

Wanavaa mavazi maalum ya uchungaji.

Hutumia kalenda ya kanisa kama mwongozo.

Meza ya Bwana hufanywa kwa utaratibu wa ratiba.

Watoto hubatizwa mara nyingi.

Wana shule za Jumapili.

Wanaheshimu sana utaratibu wa ibada.

8. MAFANIKIO YA KANISA LA KILUTHERI .

Kueneza Injili kwa mamilioni.

Elimu (shule za msingi hadi vyuo).

Huduma bora za afya.

Uongozi wa maadili.

Tafsiri za Biblia.

Kuinua viongozi wa Kiafrika.

Kupinga ujinga na mila kandamizi.

Maendeleo ya jamii.

Amani na mshikamano.

Mchango mkubwa Taifa la Tanzania.

9. MAMBO YASIYO FUATA KANISA LA KWANZA YANAYOZUNGUMZIWA (KIHISTORIA)

Kuhifadhi baadhi ya mapokeo.

Ubatizo wa watoto.

Muundo wa uaskofu.

Liturujia nzito kwa baadhi ya watu.

Kuwepo kwa tofauti za kitheolojia ndani ya kanisa.

Mavazi ya kiibada.

Wengine huona kama baadhi ya sheria za Katoliki zinaendana japo sio zote.

Kutegemea sana kalenda.

Mamlaka ya sinodi.

Changamoto za kisasa.

NAPIA UELEWE JAMBI KUWA Haya ni maoni ya kielimu na kihistoria, si mashambulizi.

HITIMISHO
Kanisa la Kilutheri:

Lilitokana na mageuzi ya kihistoria

Lina mchango mkubwa Tanzania

Lina mafundisho mengi ya Biblia

Lakini pia lina mapokeo yake

1 Wakorintho 3:11
“Maana hakuna mtu awezaye kuweka msingi mwingine isipokuwa ule uliokwisha kuwekwa, nao ni Yesu Kristo.”

NDUGU ZANGU
sote tunajua hizi imani zimepokelewa toka kwa nchi za mbali na kutufikia Afrika lengo halikuwa baya bali lilikuwa wawafanya watu wamjue Mungu imesaidia sana hata kupunguza uasi kwa watu.

Lakini nia inaweza kuwa njema.lakini isipofuata mpango wa Mungu kiimani nikosa.

Kama kunasehemu unapenda uongezee unaweza ongezea maana hii ni historia.
Naweza kuwa baadhi ya mambo sijaandika.

[email protected]
NENO LA MUNGU #HAMASA#USHAURI#UJASILIAMALI..
 
Sisi tumeridhika na Manabii wetu na Mungu wetu aliyejitambulisha kwa majina mawili ya hapo juu:

Shida ya hao jamaa zetu wanatufosi tumtambue mtume wao Muhammadi na Mungu wao Allah:

Washike alicho waambia mtume wao kuwa hawa mwabudu tunaye mwabudu katika Sura ya Makafiri:
109 Surat Al-Kafirun
 
Dini haina mipaka kwa sababu nyingi zinaamini kuwa wenye imani tofauti, wapo katika upotofu kwa hiyo ni lazma kuwaokoa kwa kuwapa maarifa na njia mpya katika dini mpya.

Hapo ndipo linapokuja suala la "dini yangu ni bora zaidi, dini yenu inawapotosha kwa sababu A, B, C

Na hii ni kwa sababu wengi wanajua ni ngumu kumteka mtu kwa kumuambia mazuri ya dini yako, kwa sababu hata yao inayo kwa hiyo wanatumia kuichora dini nyingine kwenye ubaya ili mtu aone amepotea, aingiwe hofu ya kupotea zaidi na hapo inakuwa rahisi kuwabadili.

Kwa hiyo unachokitaka bro sio rahisi, ni ngumu watu ku_ deal na dini zao ilhali wameamrishwa kusambaza imani yao
 
Limekuja kama mjadala wa wote ndio maana pamoja na kuwa nami nina imani yangu lakini sikutaka kuisemea kuepuka mgongano wa kimaslahi kwenye andishi na mjadala huru

Maadam mazungumzo ya imani yamekuwa katika mjadala wa umma, yani yakishafanyika tu, ni vizuri kuruhusu yafanyike. Si vizuri kutaka kuzuia yasifanyike.

Kwa sababu.

1. Mazungumzo yana nafasi ya kufunua ukweli. Inawezekana una imani potofu na unahitaji kusikia mazungumzo zaidi kujua kuwa unaamini imani potofu.

2. Hata kama mazungumzo yenyewe ni ya kijinga, yana makosa, yanakosoa imani yako vibaya, hiyo pia ni nafasi ya kuyasikia na kujiimarisha katika imani yako ukijua kuwa ukosoaji wa imani yako haujaiteteresha imani yako. Ukiwa na imani isiyopewa mitihani, ukaendelea kuishikilia bila mitihani, utajuaje umeishikilia kweli hiyo imani na hujaishikikia tu kwa kukosa mitihani?

Kwa hivyo, ikiwa mazungumzo yataikosoa imani kwa haki, kimantiki, kikweli, utafaidika kwa kujua ukweli na mapungufu ya imani yako.

Na pia, ikiwa ukosoaji wa imani una upotofu, hapo napo pia una nafasi ya kuimarisha imani yako kwa kuona ukosoaji huo bado haujaiteteresha imani yako.

Na kama hutaki kushiriki mazungumzo haya, si lazima ushiriki, waachie wanaotaka.
 
Dini haina mipaka kwa sababu nyingi zinaamini kuwa wenye imani tofauti, wapo katika upotofu kwa hiyo ni lazma kuwaokoa kwa kuwapa maarifa na njia mpya katika dini mpya.

Hapo ndipo linapokuja suala la "dini yangu ni bora zaidi, dini yenu inawapotosha kwa sababu A, B, C

Na hii ni kwa sababu wengi wanajua ni ngumu kumteka mtu kwa kumuambia mazuri ya dini yako, kwa sababu hata yao inayo kwa hiyo wanatumia kuichora dini nyingine kwenye ubaya ili mtu aone amepotea, aingiwe hofu ya kupotea zaidi na hapo inakuwa rahisi kuwabadili.

Kwa hiyo unachokitaka bro sio rahisi, ni ngumu watu ku_ deal na dini zao ilhali wameamrishwa kusambaza imani yao
Imani!
IMG-20260120-WA0050.jpg
 
😁 kuna wagonjwa kichaa Chao kimelala ila wakikutana na wale chronic kinalipuka zaidi
Kukusanyika kwenye jumba kisha watu wazima kujiliza toka asubuhi hadi jioni ni wazimu,tuacheni tuseme
Kuamini jina la fundi seremala hutibu fangasi, malaria,saratani, ukimwi,umasikini,kufukuza wachawi ni matumizi batili ya akili
 
Back
Top Bottom