Hakuna watu wajinga kama watu wanaoamini habari za kichawi

Kabisa,japo upo
 
Weka majina yako watu wakuoneshe demo ,Kama hujawahi kukutwa na Jambo Kaa kmya,sisi wengine yametukuta ,Ni watu wapuuzi tuu ndio wanajaribu kupuuza juu ya uwepo wa Mungu na ulimwengu wa rohoni
Kama kweli we mchawi basi utatambua majina yangu na nilipo, siyo mpaka nikutajie.
 
Hakuna watu wajinga kama wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya. Hao wanaoamini uchawi hawawakuti hawa wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya
 
Hili ni tukio lililotokea jana tu, tarehe 06 Nov 2022 huko Kenya



Your browser is not able to display this video.


ambiele kiviele Mshana Jr, ukikaidi utapigwa2,
 
Halafu Mimi kubishana na mpuuzi anayejifanya anajua sana, kumbe hana alijualo na bado anakuwa mbishi, huwa sipendi na Mara nyingi naishia kumpuuza.

Labda nijaribu kumfanya mleta mada ajitafakari upya yeye na uzi wake kwa kumuuliza maswali machache:

1.Iliripotiwa kule Rukwa mwanzoni mwa mwaka huu,mgonjwa mmoja aliyepelekwa hospitali ya mkoa akisumbuliwa na tumbo.Alipofanyiwa upasuaji alikutwa na bisibisi,wembe,nywele na vifaa kadhaa vya kielekroniki (kumbuka:Mganga Mkuu alithibitisha jambo hilo,kama huamini ingia mtandaoni).We msomi mzamifu unaweza kutuambia vile vitu viliingiaje tumboni mwa mgonjwa yule na kumfanya Mganga Mkuu akose majibu?

2.Kuna akina mama wajawazito wamekuwa wanajifungua kuku au kuishia kutoa moshi tu during delivery, ilhali walihudhuria clinic miezi yote na waliambiwa watoto walikuwa wanaendelea vizuri tumboni. Tuseme ni matokeo ya mutation? Labda matako ya mutation.

3.Pale Iringa kuna kaburi (jina la aliyezikwa mle nimelisahau,ila alikuwa mganga maarufu Iringa)limegoma kupisha ujenzi wa barabara.Greda zilizojaribu kulifukua/kulihamisha ziliishia kuharibika zote na madereva wake kufa ghafla au kujeruhiwa na kundi la nyuki.Ikabidi Tanroads wasalimu amri kwa kuipindisha barabara kando ya kaburi. Tanroads walishindwa wewe mleta mada na sayansi/teknolojia yako uchwara ungeweza?

Kisa kama hicho kilitokea Mwanza miaka ya nyuma.Bibi Nyau aligoma kuhamishwa ili kupisha ujenzi wa barabara iliyokuwa inaelekea Bugando Refferal Hospital.Utaalamu wote wa kuibomoa ulifeli vibaya,Mwl.Nyerere alijulishwa na katika moja ya ziara zake mkoani Mwanza alimtembelea 'Bibi Nyau' kumbembeleza akubali kupisha ujenzi,bado bibi akatia ngumu. Nyerere akawa mpole akaagiza barabàra impishe (ipindishwe kumkwepa) bibi. Tunajua Nyerere alikuwa anakuzidi vitu vingi: maarifa,exposure na mamlaka.Unasemaje kuhusu jambo hilo kwa mujibu wa usomi wako?
 
Unaamini hizo habari zilitokea kweli? Unatia huruma sana. Kwa hiyo na habari ya Rukwa mwewe kubeba ng'ombe hewani na kumtafuna uliamini? Acha ujinga.
 
U
Unaamini hizo habari zilitokea kweli? Unatia huruma sana. Kwa hiyo na habari ya Rukwa mwewe kubeba ng'ombe hewani na kumtafuna uliamini? Acha ujinga.
Ujinga hata mama yako na baba yako wanao, sasa mimi nauachaje?

By the way,Mhe.Mizengo Pinda mwenyewe alishakiri kule kwao radi (kwa ajili ya kumtumia mbaya wako) inauzwa openly kwa bei chee, Mimi ni nani nipinge?

Wenzako UDSM wameamua kuyafanyia utafiti mambo hayo, ila wewe unakuja kuharisha hapa bila utafiti wowote.
 
Yaani sababu kasema Pinda?!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…