Mhhh. Nadhani ujinga uliokubuhu ni ule wa kuona kwamba wale wanaoamini uwepo wa Uchawi ni wajinga. (yaani wewe unajiona ndo una akili). Hebu jiulize kidogo; Hivi watu weeengi kiasi hicho(wazee,vijana, wasomi, viongozi wa kiimani, misahafu..) waseme uchawi upo halafu wewe mtu mmoja unanga'ngania kusema uchawi haupo na mbaya zaidi kuwaita watu hao ni wajinga inakuwaje? Mm nafikiri ungelitulia kwanza mahali, ukatafakari kwa kina kisha uanze kufuatilia ukweli wa hicho wanachokiamini(Uchawi) na kinatendaje kazi. Fanya marejeo katika vitabu/maandiko (hata kama vikiwemo vile vya dini), ongea au fanya utafiti na watu - wazee kwa vijana(hata kama ni viongozi wa dini au wasomi maarufu) halafu mwisho pitia matukio mbalimbali ya kweli yaliyotokea na visababishi vyake then Uje kutoa mrejesho hapa. Kwa mfano ni sawa na Ukiambiwa kuna simba Serengeti usiseme eti kwa kuwa hujamwona basi hayupo. Kutokuamini kwako hakutaondoa uwepo wa simba Serengeti. Vivyo hivyo kutokuamini kwako kwamba uchawi upo hakutabatilisha uwepo wa uchawi duniani. Siku ukikamatika ndio utajua ulikuwa hujui na hauamini. Hapo ndo itakuwa kusikia kwa kenge ni damu masikioni.