Halafu Mimi kubishana na mpuuzi anayejifanya anajua sana, kumbe hana alijualo na bado anakuwa mbishi, huwa sipendi na Mara nyingi naishia kumpuuza.
Labda nijaribu kumfanya mleta mada ajitafakari upya yeye na uzi wake kwa kumuuliza maswali machache:
1.Iliripotiwa kule Rukwa mwanzoni mwa mwaka huu,mgonjwa mmoja aliyepelekwa hospitali ya mkoa akisumbuliwa na tumbo.Alipofanyiwa upasuaji alikutwa na bisibisi,wembe,nywele na vifaa kadhaa vya kielekroniki (kumbuka:Mganga Mkuu alithibitisha jambo hilo,kama huamini ingia mtandaoni).We msomi mzamifu unaweza kutuambia vile vitu viliingiaje tumboni mwa mgonjwa yule na kumfanya Mganga Mkuu akose majibu?
2.Kuna akina mama wajawazito wamekuwa wanajifungua kuku au kuishia kutoa moshi tu during delivery, ilhali walihudhuria clinic miezi yote na waliambiwa watoto walikuwa wanaendelea vizuri tumboni. Tuseme ni matokeo ya mutation? Labda matako ya mutation.
3.Pale Iringa kuna kaburi (jina la aliyezikwa mle nimelisahau,ila alikuwa mganga maarufu Iringa)limegoma kupisha ujenzi wa barabara.Greda zilizojaribu kulifukua/kulihamisha ziliishia kuharibika zote na madereva wake kufa ghafla au kujeruhiwa na kundi la nyuki.Ikabidi Tanroads wasalimu amri kwa kuipindisha barabara kando ya kaburi. Tanroads walishindwa wewe mleta mada na sayansi/teknolojia yako uchwara ungeweza?
Kisa kama hicho kilitokea Mwanza miaka ya nyuma.Bibi Nyau aligoma kuhamishwa ili kupisha ujenzi wa barabara iliyokuwa inaelekea Bugando Refferal Hospital.Utaalamu wote wa kuibomoa ulifeli vibaya,Mwl.Nyerere alijulishwa na katika moja ya ziara zake mkoani Mwanza alimtembelea 'Bibi Nyau' kumbembeleza akubali kupisha ujenzi,bado bibi akatia ngumu. Nyerere akawa mpole akaagiza barabàra impishe (ipindishwe kumkwepa) bibi. Tunajua Nyerere alikuwa anakuzidi vitu vingi: maarifa,exposure na mamlaka.Unasemaje kuhusu jambo hilo kwa mujibu wa usomi wako?