Hakuna watu wajinga kama watu wanaoamini habari za kichawi

Mkuu umemaliza kitu case closed kama hajaelewa huu ujumbe huyo jamaa atakuwa ni takataka ya kuzimu
 
Huyu jamaa atafika akiwa amechoka sana.
 
Daah watu wakisoma na kupata vyeti vya kucopy assignment na ufaulu wa mchongo hujifanya wanajua kila kitu, asee dunia imekutangulia, nikikumbuka tukio alilopigwa mpenzi wngu nachelea kusema ukue kwanza😭😭
Alikutapeli na kukudanganya huyo mpenzi wako
 
Ngozi nyeupe ilivyopumbaza akina sisi Hadi kuaminishwa matukio Fulani ni sayansi ila deep down Ni pure occultism.
Unataka kuuona vizuri nenda kwenye Soka,Mziki, Biashara na Siasa.
Kama tungekuwa kuna uchawi mpirani leo timu za Africa zingekuwa na mafanikio kuliko za ngozi nyeupe. Na hata kibiasharq na muziki weusi wangekuwa na mafanikio zaidi.
 
Kuna kanuni tano za ujinga. Moja inaeema kuwa ujinga wa mtu hautegemei status yake. Kuna wasomi, wazee na watu mashuhuri wajinga. Wajinga wametawanyika sawa sawa katika jamii.

Mengi yanayoitwa matukio ya kivhawi yanaitwa hivyo sababu ya kushindwa kuyaelewa. Na hawayaelewi sababu ya ujinga. Hata kuna madaktari wajinga, akishindwa jua ugonjwa utasikia anasema labda mambo ya kienyeji
 
Baada ya kugundulika yanatokana na mbu ndiyo mmekuja na explanation kuwa yako mawili. La kurogwa na la mbu?!!!! Ni kawaida kwa mtu mwenye imani ya kijinga anapoambiwa ukweli kutetea kwa nguvu zote. Upo kwenye denial.
kuja na explanation za kigunduzi siyo dhambi!!..... wala tusi!...Sasa km ni kawaida yetu kwa sababu tunajua tatizo letu ni nini, Ubaya wetu uko wapi hapo? ...hata ''Denial'' siyo tusi wala dhambi kasome tena!

tunatetea kwa nguvu zote kwa sababu sisi km sisi! tunajua kuwa tunajua! hakuna amri Duniani inayosema kujua ni dhambi!
 
Hata kipindupindu baada ya chanzo chake kujulikana watu wanasema, "Kuna cha kurogwa na cha kuumwa kweli." Hii hutokea sana wajinga wakikabili ukweli.
 
Wewe ni ng'ombe uliyetoroka zizini harafu unajifanya unajua wakati wewe ni mjinga wa kiwango Cha PhD
 
Hajui ya kwamba Uchawi sio ujinga bali ujinga uko kwenye kukosa maarifa juu ya uchawi
Inaonekana amejiaminisha kabisa-kabisa kwenye mambo ya Vinavyoonekana (Physics,Chemistry, Biology na Utendaji wake n.k.)lakini visivyoonekana(Ulimwengu wa Roho) anavikataa kataa-kata.. Sasa sijui kama anaamini uwepo wa mapepo, malaika, majini, Shetani, Mungu na Roho mbalimbali e.g. za mababu zake, marafiki, ndugu na jamaa waliotangulia mbele za Haki.
Amepungukiwa sana na uelewa juu ya Uwepo wa Upande wa pili na Utendaji wake.
 
Hata kipindupindu baada ya chanzo chake kujulikana watu wanasema, "Kuna cha kurogwa na cha kuumwa kweli." Hii hutokea sana wajinga wakikabili ukweli.
cholera, Hiv, kimeta, COVID nk, ni magonjwa yaliyo tengenezwa kwenye Maabara za kizungu! na bado mtegemee mengi zaidi ni wazi hukusoma!..wajua kwa nini walifanya hivo??
 
Kama ndio hivyo basi wewe utakuwa mjinga kuliko wale unaowaita ni wajinga kwa sababu umeshindwa kubaini ni kwa nini wao ni wajinga.
Madaktari wanalijua fika suala hilo na anapokuambialabda ni mambo ya kienyeji anamaanisha katumie tiba mbadala i.e. Mitishamba. Unaenda kuipata wapi hilo ni shauri lako. Zingatia hata pale Muhimbili kipo kitengo cha namna hiyo.
 
Kama ndio hivyo basi wewe utakuwa mjinga kuliko wale unaowaita ni wajinga kwa sababu umeshindwa kubaini ni kwa nini wao ni wajinga.
Mtu anayeamini kipindupindu kinatokana na kurogwa, au kuna majini huwa yanajibanza chooni siyo kazi kubwa kumtambua kuwa ni mjinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…