Hakuna watu wajinga kama watu wanaoamini habari za kichawi

Sasa wachawi wanafanyaje mambo yao kama si kuatamia mayai ya radi? unaleta magonjwa ya mlipuko? wanavuta pesa kwa uchawi? wanafanya dhahabu zitokee? wanazuia na kuleta mvua? wanawasha moto nyumba, kuna mmama south nyumba yake iliungua akasema amepigwa juju na anashangaa hana ubaya na mtu. Huo uchawi unaoamini unafanyaje kazi?
 
Duh basi itakuwa maajabu ya dunia mtu kuibiwa Instagram account kwa uchawi huu wa kiswahili.
Hii nitabisha hadi mwisho..

Nikutajie account yangu ukawaambie wachawi waiibe.
Sijasema kuibiwa insta kwa uchawi, bado unakaza ubongo tatizo watu kuelewa ni wagumu, wewe ili uamini si mpaka uone au umemaanisha nini uliposema wachawi waibe bank si ina maana haujawahi kuona si ndio? Nimekuuliza umewahi kuibiwa insta a/c ukasema hujawahi inamaana hauamini km mtu anaweza akaiba a/c mpaka ujionee kwa macho yako mawili yaan hadi uibiwe si ndio?
 
Mmh ipo yaja utaamini uchawi upo
 
Wewe emu nitolee ujinga wako, kamuulize aliekulisha huo ujinga, huo sio uchawi hizo ni simulizi za kusadikika
 
Fafanua hapahapa usijali
 
Wewe ndo hutoi maelezo ya kuridhisha unategemea mimi nitaelewa?
Wizi wa account za insta unahusika vipi na uchawi si utoe maelezo ya kuridhisha, au unadhani mimi ni mchawi naweza kusoma mawazo yako?

Bado sijaweza kuunganisha uhusiano wa kuibiwa account na uchawi.

Tatizo umejaa makasiriko zaidi badala ya kutoa hoja inayoeleweka na kuelimisha.
 
Hapana mkuu. Mjadala ni kuamini uchawi unafanya kazi na unaamini mambo yanayodaiwa unafanya. Kama kutuma mamba, kutuma nyuki, kuleta magonjwa ya kuhara, kuingilia watu kimwili nk
Ikawaje Daktari akaitwa daktari bila kutibu, Mwalimu aitwe mwalimu na hajawahi kufundisha, Mkulima vilevile.

Aitweje sasa mchawi bila vitendo vya kichawi? Kwa nini unaitwa uchawi?
 
Hahahaaa, na wanaamini mchawi anaweza kusoma mawazo yako. Good one.
 
Uchawi ni Imani
Umewahi kusikia wakisema Imani za kishirikina?

Sasa uchawi sio ushirikina ila ushirikina hauwezi kuwepo bila uchawi kuwepo, hadi hapo ushanielewa au bado umekaza ubongo?

Maana watu km nyinyi ili muelewe inabidi mpelekwe slow mkipelekwa mputamputa mnatoka kapa

Umeelewa?
 
Nimeelewa endelea...
 
Ikawaje Daktari akaitwa daktari bila kutibu, Mwalimu aitwe mwalimu na hajawahi kufundisha, Mkulima vilevile.

Aitweje sasa mchawi bila vitendo vya kichawi? Kwa nini unaitwa uchawi?
Watu wanaweza amini uwepo wa matendo ambayo hayapo. Na wakaamini mtendaji wa matendo hayo yupo. Akili ya binadamu ikifika ukomo wake inaweza amini habari za ajabu kabisa.
 
Nimeelewa endelea...
Sawa saaasa kuhusu swala la insta haiibwi kwa kutumia uchawi wa kiimani ila ni uchawi wa technology,

Kwa hio nilikupa mfano wa kuibiwa a/c ya insta nikijaribu kukuonyesha jinsi inavyokua na matokeo yanavyokua linapokuja suala la uchawi,

Kuhusu kuiba bank haiwezekani kwa sababu, utajiri wa wachawi sio pesa hizi tunazozitumia mimi na wewe,

Ushaelewa au bado umekaza ubongo?
 
Mimi ni MKRISTO, tena ni MKRISTO KWELI KWELI (sijisifu hata kidogo) lakini sio tu kwamba naamini uchawi upo bali nafahamu kwa dhati kabisa kuwa "uchawi" upo na unafanya kazi!

Wewe usiyeamini kuwa uchawi upo basi wewe ndio mjinga wa mwisho hapa duniani.
 
Na hapa tunazungumzia uchawi wetu huu wa kiafrika.
Nilikuelewa tangu mwanzo ndio maana nikakasema labda ni uchawi wa kizungu (technology) ndo unaweza kuiba account.
Turudi kwenye uchawi wetu huu tunaoujua sisi...Acha kuchanganya mambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…